Seif Tumekusikia; Sasa jiuzulu na iondoe CUF kwenye SUK!

Bado sijaona jipya hapa...Nataka kusikia mtanganyika angalau mmoja anatamka hadharani kama na yeye hautaki Muungano...Sio kujificha hapa JF na kujifanya mchambuzi mashuhuri.

Wakati unakaribia ule mrija wa unyonyaji tanaukata....

Watanganyika wanaaamini katika Muungano kwani ndivyo taifa letu lilipoanzia. We are by the very founding of our nation pro-African union. Tatizo ni kuwa Muungano na Zanzibar labda haukutakiwa kuwepo in the first place hasa kwa vile toka mwanzo imekuwa ni kulalamika tu. Wakishatoka Tanzania bara wala haitakwazika kama nchi nyingine inataka kuungana na labda tutaungana vizuri zaidi baada ya kujifunza somo la Zanzibar. Lakini siamini kama kuna nchi yoyote itakayotaka kuibeba Zanzibar mgongoni namna Tanganyika ilivyoibeba na kuidekeza Zanzibar.
 
  • Thanks
Reactions: FJM

Humuwezi kuukata mkiwa katika mkataba.
Kwani sheikh ni mrija gani? Mbona husemi nini ZNZ inanyonywa kwa bajeti ya bilioni 120 kwa mwaka pungufu ya bajeti ya soko la kariakoo?
 
Barubaru; kuna swali nimeshakuuliza (wewe na wenzako wenye mawazo yanayowiana kuhusu muungano) mara kadhaa lakini hujawahi kunijibu hata mara moja (na niseme hata wenzio hawajajitokeza kulijibu).

Narudia tena: Kinachowazuia Wazanzibari kujiondoa kwenye huu muungano wasioutaka ni kipi, ukichukulia wana baraza la kutunga sheria, wana bendera na raisi wao? Huo muungano wa mkataba mnaoutaka, kwa nini msiufanye na Kenya, Msumbiji, Comoro n.k, n.k. Ni lazima iwe na Tanganyika?[....../QUOTE]

Mtoboasiri,

nafikiri mara kwa mara nimekuwa nakujibu suala lako hili lakin kwa kuwa unajifanya kipofu hivyo unalipotezea. naona sasa ngoja nikujibu kwa mara ya mwisho.

Znz haina ubavu wa kujitoa kwa sababu NGUVU KUBWA ZA KIJESHI (kwa maana majeshi, Polisi na Usalama na zana zao zipo Tanganyika) na Amiri jeshi mkuu wa majeshi yaho ya ulinzi na Usalama ni Rais wa JMTz. Hivyo chochote kikitendeka Znz basi nguvu za kijeshi kutoka Bara zitaidondokea Znz.

Lakin kama nguvu hizo zingekuwa Znz basi saa hizi tunazungumzia mengine kabisa.

Kwa mantiki hiyo Znz imeshika makali ya Muungano lakin Tanganyika ndio wameshika MPINI. Suala la kuiuliza kwanini mnaing'ng'ania Znz? kwanini wasiachiwe waende zao? Je Tanganyika haiwezi kujiendesha yenyewe bila Znz?

naomba majibu yako hapo

Barubaru, hizo ni hisia tu. Siamini kuwa kuna hoja ya kuwa na hofu ya nguvu za kijeshi kutumika. Kwani Zanzibar wakiamua (kwa kutunga sheria) Tanganyika watakuwa na uhalali gani wa kuwazuia? Sudan ya Kusini mbona walijitoa na Sudan (yenye nguvu kubwa zaidi kijeshi) hawajawalazimisha kubaki nao?
 
Naona wewe huiujui kabisa katiba ya Muungano na ile ya Znz.

Kwa kukusaidia tu ni kuwa mambo ya ulinzi na usalama ni mambo ya muungano. na vile vile Raisi wa muungano ndio amiri jeshi mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi na Usalama.

sasa labda utubainishie upenyo upo wapi hapo kwa Znz?
 
Barubaru; Muungano (na katiba yake) upo tu kwa hiari ya pande mbili. Moja ikijitoa muungano na hivyo katiba yake vinakosa uhalali. Ina maana Tanganyika nayo haiwezi kujitoa kwa kuhofia majeshi ya muungano? Au Tanganyika ndio muungano wenyewe?
 
Humuwezi kuukata mkiwa katika mkataba.
Kwani sheikh ni mrija gani? Mbona husemi nini ZNZ inanyonywa kwa bajeti ya bilioni 120 kwa mwaka pungufu ya bajeti ya soko la kariakoo?

Mkataba utawashinda ,kwasababu ule unyonyaji hamtaweza tena kuendelea na unyonyaji wenu...Mwisho wa yote mtakubali kuuvunja Muungano...
Zanzibar nje ya Muungano ina uwezo, itaweza kuwa na njia nyingi za kukuza uchumi wake. Muhimu kwanza kuondoa jinamizi hili la Muungano.
 
Watanganyika wanaaamini katika Muungano kwani ndivyo taifa letu lilipoanzia. We are by the very founding of our nation pro-African union. Tatizo ni kuwa Muungano na Zanzibar labda haukutakiwa kuwepo in the first place hasa kwa vile toka mwanzo imekuwa ni kulalamika tu. Wakishatoka Tanzania bara wala haitakwazika kama nchi nyingine inataka kuungana na labda tutaungana vizuri zaidi baada ya kujifunza somo la Zanzibar. Lakini siamini kama kuna nchi yoyote itakayotaka kuibeba Zanzibar mgongoni namna Tanganyika ilivyoibeba na kuidekeza Zanzibar.

Nakubaliana na wewe unaposema kama Muungano haukutakiwa kuwepo in the first place. Zanzibar haikuomba isaidiwe,ibebwe au idekezwe na Tanganyika. Kinyume chake, Zanzibar ilikuwa na uwezo mzuri na ikijitosheleza wakati inaungana na Tanganyika.

Muungano na tamaa ya Nyerere ndio imetufikisha hapa tulipo. Kama mzigo mumejibebesha wenyewe na kwanini hamtaki kuutua? Pro-African Union sawa, lakini isiwe sababu ya mmoja kumuamulia mwengine masuala ya nchi yake. Hakuna nchi itakayo ungana na Tanganyika baada ya Muungano huu kuvunjika. Hakuna nchi itakayo kubali kupoteza mamlaka yake kwa watangayika. Hamtapata tena wa kuwachezea...
 
Mkataba utawashinda ,kwasababu ule unyonyaji hamtaweza tena kuendelea na unyonyaji wenu...Mwisho wa yote mtakubali kuuvunja Muungano...
Zanzibar nje ya Muungano ina uwezo, itaweza kuwa na njia nyingi za kukuza uchumi wake. Muhimu kwanza kuondoa jinamizi hili la Muungano.
Mkutano wa Bwawani Oktoba 6.
Mansour Himid (Waziri)
Jusa Ismail ( Mwakilishi, Uamsho, CUF)
Nasor Hassan Moyo (mjumbe BLM, waziri JMT, waziri SMZ, Mwenyekiti kamati GNU maridhiano)

Wote hao kwa kutumia vinywa vyao na akili zao wamesema wanataka muungano! Je hawakuliona hilo jinamizi?

Takashi, weka substance once and while ahli wangu! Matusi kila uchao utaitwa Ustadhi Matusi. Shauri yako! Vijana wa JF hawana dogo sheikh wangu watakutengua udhu!

Vipi watoto chei chei lakini, Shem kifanahali! wajulie hali inshallah!
 
Nimekuacha upambane na kijana mpya Bw,Foum Jnr naona umekibia mbio na MMKJ na yeye katoweka...Nilikuambia tumewashika pabaya . Zanzibar huru ,haizuiliki tena...

Nashukuru Mungu familia yote tupo wazima...ila mwenzi miwili nyuma nilipata msiba wa mzee wangu (father) ametangulia. Mungu amrehemu.
 
Nipo na Foum vema sana! sichagui kijana au mzee naangalia hoja.
 
duh yes; Zanzibar haijawahi kufanikiwa bila kutegemea bara.

Naomba unielezee ilikuwa ikiwategemea kivipi? Nielimishe nijue.
Mana naona zanzibar ilikuwepo mbele kwa hatua mia zaidi ya bara! Magorofa, umeme, tv ya rangi, mataa barabarani, lift..... Ebu nipe elimu kidogo ni vipi tulikuwa tunawategemea?
 
Back
Top Bottom