Seif Tumekusikia; Sasa jiuzulu na iondoe CUF kwenye SUK!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,342
38,995

Kulikuwa na utata mwanzoni - na kwa baadhi ya watu - juu ya msimamo wa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) ambaye pia ni Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Bw. Seif Sherrif Hamad hususan suala la kile kinachojulikana kama "Muungano wa Mkataba". Katika clip hii (ambayo labda tayari imeshaonekana) Bw. Seif ametangaza bila ya utata kuwa yeye ni "Muumini wa Muungano wa Mkataba".

Kuwa muumini wa Muungano wa "Mkataba" ni kutokuwa Muumini wa Muungano wa sasa kwani katika Muungano wa Mkataba unaopendekezwa na waumini wake Zanzibar inarudi na kuwa nchi huru ikiwa na hakimiya kamili (full sovereignty) na inahusiana na Tanganyika kwenye mambo kadhaa ya kimkataba badala ya ilivyo sasa ambapo nchi mbili ziliamua kusalimisha hakimiya zao kwenye Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kuwa muumini wa Muungano wa namna hii ni kuwa muumini wa kupigania uhuru wa Zanzibar kutoka kwenye Muungano wa sasa; lakini zaidi ni kuwa muumini kuwa Muungano wa sasa ni wa kikoloni ambapo Tanganyika inainyonya Zanzibar. Lakini zaidi ni kuamini kuwa Muungano wa sasa siyo halali.Sasa kama Seif anaamini yote mawili - kwamba Tanganyika inaikalia Zanzibar kama Koloni na kuwa Muungano wa sasa siyo halali basi yampata aendelee mbele kwenye hitimisho la kimantiki - kujiuzulu Umakamu na kukiondoa CUF kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).

Afanye hivi ili chama chake kifanye harakati ya kuiondoa Zanzibar kutoka kwenye Muungano na Wazanzibar wakikubali kwenye kura ya maoni yao basi CUF ikishika madaraka Zanzibar ifikirie namba ya kuingia kwenye "muungano wa Mkataba' na nchi yoyote nyingine (si lazima iwe Tanganyika). Kwa kufanya hivi Seif ataonesha mfano kwa viongozi wengine wote wa Zanzibar wenye kuamini Muungano wa Mkataba kutoka kwenye nafasi zao na pia wale Wazanzibari walioko kwenye huduma ya Muungano wa sasa watoke. Lakini zaidi sana Seif akiamua kujiuzulu nafasi hizo wabunge wake wa CUF walioko kwenye Bunge la Muungano nao waamue kufuata mkumbo ili harakati za Uhuru wa Zanzibar (secession) zianze rasmi zikiongozwa na Seif.
 
Last edited by a moderator:

Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
4,872
4,530
Seif hana ubavu wa kujiuzulu. Tangu alipogeuzwa nyumba ndogo ya CCM na kuwasaliti wazanzibar amekuwa mtu wa ajabu karibu sawa na Cheyo na Mrema. Tamaa yake ya madaraka itamtokea puani. Sasa anapima aendelee miaka mitatu iliyobaki au alikoroge ili agombee mwaka 2015 anajikuta msambweni. Seif hana udhu wala mvuto tena kwani ni kigeugeu na mchumia tumbo wa kawaida sawa na Amani Karume anayeongelea Muungano baada ya kuzuiliwa kugombea urais wa muungano. Mbona hakuyasema hayo wakati akiwa madarakani. Heri ya mzee Aboud Jumbe alijaribu ingawa wenzake walimgeuka akiwamo Seif kabla ya kuonyeshwa mlango baadaye.
 

mpemba mbishi

JF-Expert Member
Nov 27, 2011
1,132
183
...Afanye hivi ili chama chake kifanye harakati ya kuiondoa Zanzibar kutoka kwenye Muungano na Wazanzibar wakikubali kwenye kura ya maoni yao basi CUF ikishika madaraka Zanzibar ifikirie namba ya kuingia kwenye "muungano wa Mkataba' na nchi yoyote nyingine (si lazima iwe Tanganyika). Kwa kufanya hivi Seif ataonesha mfano kwa viongozi wengine wote wa Zanzibar wenye kuamini Muungano wa Mkataba kutoka kwenye nafasi zao na pia wale Wazanzibari walioko kwenye huduma ya Muungano wa sasa watoke. Lakini zaidi sana Seif akiamua kujiuzulu nafasi hizo wabunge wake wa CUF walioko kwenye Bunge la Muungano nao waamue kufuata mkumbo ili harakati za Uhuru wa Zanzibar (secession) zianze rasmi zikiongozwa na Seif.

Chuki dhidi ya Wazanzibari at work practically!!! Kimenuka kwenu katu hamuwezi kutufitinisha tena. Wacheni majungu yatawamaliza tumieni muda kuitafuta Tanganyika yenu.
 

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,114
7,210
Hawa jamaa wa cuf kumbe watakuwa wanawaunga mkono uamsho! Abatoba! Basi kazi ipo.sasa mimi nashauri wakishavunja muungano wa taifa moja wakaja kwenye mambo ya mikataba,watakuwa hawana jipya kwani mikataba ya kimataifa ikiwemo ile ya nchi na nchi iko mingi tu.kwa hiyo mimi nawashauri badala ya kusaini mkataba na tanganyika,sasa wanaweza kusaini mkataba na mataifa mengine kwa sababu mimi naona kama wanaleta unafiki tu hapa.
 

Indian

JF-Expert Member
Oct 27, 2012
822
705
huu sio wakati wa seif kujiuzuulu,unataka ajiuzulu ikisha akizungumza mambo ya muungano mumtie ndani hujui kamaa ss iv analindwa na katiba, hiv sasa ni wakati wake wa kuongeza sauti dunia nzima wasikie kilio hiki cha waznz.
 

Pakacha

JF-Expert Member
Apr 15, 2008
821
32
Hakuwezi kuwa na Muungano huo wa MKATABA hata siku moja. Kuna taifa moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lenye mamlaka kamili ya dola. Hakuna mbadala wa hili. Zoezi la sasa ni kuandika tena katiba ya Jamhuri hii ya Muungano. Seif na Jussa waache wahubiri uumini wao kwa amani tuione sura yao halisi.
 

Shibalanga

Senior Member
Mar 1, 2011
179
93
Seif hana ubavu wa kujiuzulu. Tangu alipogeuzwa nyumba ndogo ya CCM na kuwasaliti wazanzibar amekuwa mtu wa ajabu karibu sawa na Cheyo na Mrema. Tamaa yake ya madaraka itamtokea puani. Sasa anapima aendelee miaka mitatu iliyobaki au alikoroge ili agombee mwaka 2015 anajikuta msambweni. Seif hana udhu wala mvuto tena kwani ni kigeugeu na mchumia tumbo wa kawaida sawa na Amani Karume anayeongelea Muungano baada ya kuzuiliwa kugombea urais wa muungano. Mbona hakuyasema hayo wakati akiwa madarakani. Heri ya mzee Aboud Jumbe alijaribu ingawa wenzake walimgeuka akiwamo Seif kabla ya kuonyeshwa mlango baadaye.


Mapambazuko mapya....! kikwetu hapo kwenye RED tunawaita "SUMILINDA" ngoja tuone au ni upepo tu utapita?
 

SMU

JF-Expert Member
Feb 14, 2008
9,611
7,788
Hakuwezi kuwa na Muungano huo wa MKATABA hata siku moja. Kuna taifa moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lenye mamlaka kamili ya dola. Hakuna mbadala wa hili.
Kwa nini? Wananchi wakiamua haliwezekani?

Mimi naamini ni suala la hoja tu, hakuna haja ya "kuwalazimisha" wananchi muundo ambao "watawala" wanaona unafaa na wananchi hawautaki.
 

Akthoo

JF-Expert Member
Nov 5, 2007
954
933
hivi we mzee mwanakijiji zile harakati zako za ccj,cck,ccx na cheche zimeishia wapi?!!!
 

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
25,051
36,857
Kwani wazanzibar anaewazuia kuvunja muungano nani? au mnasubili aje kuwavunjia nani.?...
 

Newcastle

Senior Member
Oct 11, 2012
142
15
Mbona wananchi wamenyamaza viongozi wanabwatuka?wakivunja mungano na bara watavunja na wa pemba.naomba muungano uvunjike kesho,wanatuibia mchele wetu kahama kwenda znz
 

Bobuk

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
5,870
3,262
Chuki dhidi ya Wazanzibari at work practically!!! Kimenuka kwenu katu hamuwezi kutufitinisha tena. Wacheni majungu yatawamaliza tumieni muda kuitafuta Tanganyika yenu.

Uliwahi kuona/kusikia wapi MKOLONI (Tanganyika) akianzisha harakati za kuliachia KOLONI (Zanzibar) lake.

Kama ingekuwa hivyo basi hadi hii leo Tanganyika ingekuwa chini ya Malikia (UK). Ua Zanzibar ingekuwa chini ya SULTAN.
 

sinshoo

Member
Oct 13, 2012
50
14
To be honest naipenda Zanzibar iwe huru wawe na uhuru wao kamili wajiamulie mambo yao wenyewe na sisi Tanganyika yetu Irudi tutakuwa kama Russia na Zanzibar ni Georgia tutaishi bega kwa bega TUTASHIRIKIANA KAMA KAWAIDA KIUCHUMI NA KIBIASHARA KAMA ILIVYO sOUTH AFRIKA NA LESOTHO
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

31 Reactions
Reply
Top Bottom