Tanga; Kila Mzazi Mwenye Mwanafunzi Kutozwa Tshs. 1,000 ya Chakula Cha Mtoto Akiwa Shuleni

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,128
49,863
Hata kama jambo Lina nia njema kiasi ,Je ni lini wazazi walishirikoshwa kama utaratibu unavyotaka?

========

Muktasari:
Kindamba alizitaka halmashauri zote 11 za Mkoa wa Tanga kutekeleza kwa ukamilifu azimio la kuchangia Sh1,000 kwa kila mtoto kwa ajili ya kupata lishe shuleni ili kuimarisha juhudi za kujenga kizazi bora.

Tanga. Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Waziri Kindamba ameeleza umuhimu wa viongozi kusimamia utekelezaji wa maazimio juu ya kuimarisha lishe kwa watoto hasa wenye umri chini ya miaka mitano na kuendelea ili kujenga kizazi kijacho ambacho ni bora.

Kindamba alizitaka halmashauri zote 11 za Mkoa wa Tanga kutekeleza kwa ukamilifu azimio la kuchangia Sh1,000 kwa kila mtoto kwa ajili ya kupata lishe shuleni ili kuimarisha juhudi za kujenga kizazi bora.

“Jambo la ukuaji na suala la lishe ni muhimu sana. Tunatengeneza kizazi kizazi kijacho. Lazima tutengeneze kizazi cha watu walio bora kuliko sisi na wao watafanye hivyo hivyo,” amesisitiza.

Kindamba amesema kuwa Watanzania wasiliangalie suala la lishe kwa mtazamo finyu bali kwa mtazamo mpana kwa sababu nchi inataka kujenga kizazi ambacho kinaweza kushindana katika majukwaa ya kimataifa na watoto wa mataifa makubwa.

Hivyo, alisema, lazima viongozi na Watanzania kwa ujumla kuhakikisha kuwa wanalipa suala la lishe kipaumbele. “Tusipofanya hvyo tunajitengezea bomu ambalo litatulipukia ikifika wakati kwa kutozingatia maeneo yanayogusa ukuaji wa mtoto,” amesema.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa hata Rais Samia Suluhu Hassan vipaumbele vyake vyote vimelenga katika suala la kuhakikisha mtoto anakuwa katika mazingira mazuri kwa kutoa fedha katika sekta za maji, afya na elimu.

Aliwataka viongozi kushirikiana kuondoa udhaifu katika utekelezaji wa viashiria vilivyowekwa kama vile suala la uundaji wa klabu za lishe shuleni, asilimia ndogo ya viwanda vidogo vinavyoongeza virutubisho katika chakula na asilimia ndogo ya shule zinazotoa lishe shuleni.

Aizungumza katika kikao hicho, Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Pili Mnyema alisema kuwa pamoja na changamoto zilizojitokeza kiujumla, halmashari nyingi zimefanya vizuri katika utekelezaji wa mipango yakuimarisha lishe ya mtoto.

Alisema kuwa hali ya udumavu katika mkoa wa Tanga imepungua kutoka asilimia 34 mwaka 2018 hadi kufikia asilimia 21.4 mwaka 2022 kwa watoto walio katika umri kuanzia sifuri (0) hadi miaka 8 wakati ambapo hali ya uzito pungufu imepungua kutoka asilimia 15.6 hadi kufikia asilimia 11.2 mwaka 2022.

“Kama halmashauri zitaendelea kutekeleza afua za lishe kama vile utekelezaji wa azimio la kutenga Sh1,000 kwa kila mtoto hali ya udumavu na ukosefu wa lishe kwa ujumla itaendelea kupungua hususan kwa watoto walio katika umri kuanzi miaka 0 hadi 8,” alisema Mnyema.

Mapema, Ofisa Lishe Mkoa wa Tanga, Sakina Mustafa alisema kuwa utendaji wa fedha kwa ajili watoto, utoaji wa chakula shuleni na kutoadhimisha Siku ya Lishe katika vijiji ni changamoto zinazokabili mkoa katika mkakati wa kuboresha lishe ya watoto mkoani Tanga.

Aliwataka viongozi wote kushirikiana kuhakikisha watoto wanapata chakula shuleni ili waweze kusikiliza masomo yao vizuri. Pia alizungumzia hali ya utoaji matone ya Vitamini A kwa watoto walio umri wa mwa 0 hadi miaka 8 alisema kuwa utekelezaji hadi hivi sasa umefikia asilimia 82.

My Take
Je Michango ya hovyo hovyo mashuleni iliyopigwa marufuku imerejeshwa?
 
Acha ujinga. Tsh 1000 ya mwanao kula unakuja kuiandikia uzi huku? Jadili mambo ya msingi kama kondi ya pango kupandishwa kwa mujibu wa dokta mwigulu mbobezi wa uchumi.
Mbona mumeambiwa mtoe buku Kwa Mfuko wa saruji Ili Watoto Hadi wa diploma Wapewe mikopo wasome hamtaki?

Mbona mumeambiwa mlipe sh.100 Kwa Kila Lita ya mafuta Ili mujengewe Barabara Vijijini hamtaki?

Buku na mia ipi kubwa?

My Take
Lini Mkuu wa Mkoa aliwwka kikao na wazazi kupanga hiyo buku kama utaratibu unavyotaka?

Punguza ujinga Mzee ,kama buku ndogo Kwa nini Serikali isitoe yenyewe?
 
Waache wale shule vijijini kuna wanafunzi wanasafiri umbali mrefu kufuata Elimu,huku wakiwa hawana uhakika wa kupata chakula cha asubuhi na mchana.
Hiyo 1,000 kwa wazazi Masikini katika shule za kata zitasaidia kuwapunguzia gharama.
Kama wazazi ni maskini Kwa nini Serikali isitoe hizo hela?
 
Mkuu acha ujinga,unataka sisi walimu tukatwe hiyo buku buku tuwalipie watoto wenu ili wale chakula!? Kuna watu Sera ya elimu bure imewapumbaza sana,imagine kinachofanyika ni kwa manufaa ya mtoto harafu mtu anakuja kulia lia mitandaoni kutaka huruma ya watu wa mitandaoni kisa 1000.

Mimi kama itatokea siku moja nikawa kiongozi mkubwa katika nchi hii wanaume wanaozalisha wake zao na kutelekeleza majukumu yao kama wazazi ni fimbo tu,ngono ufanye wewe harafu kuhudumia kiumbe chako uje ulie mitandaoni,
!?
Watoto wanapitia magumu sana ,hebu fikiria mtoto kala usiku muda wa saa mbili ,kuja kula tena ni kesho yake saa mbili,tunatengeneza taifa gani la watu wajinga wajinga wasioweza timiza majukumu yao kwa watoto wao?

Hongera mkuu wa mkoa kwa kuliona hilo,ikiwezekana niite nije nikusaidie kuwatia bakora watu wa jamii ya mtoa hoja watakao shindwa kulipa hiyo sh 1000.

Nashauri rais wetu atoe neno juu ya elimu bure kuwa watu wasibweteke na wakubali kuchangia panapohitajika.

Nani kasema kuwa serikali inatoa chakula bure kwa watoto wa shule za day!?
 
Mkuu acha ujinga,unataka sisi walimu tukatwe hiyo buku buku tuwalipie watoto wenu ili wale chakula!? Kuna watu Sera ya elimu bure imewapumbaza sana,imagine kinachofanyika ni kwa manufaa ya mtoto harafu mtu anakuja kulia...
Uko tayari kutoa buku Kwa Kila Mfuko wa saruji Watoto wapate mikopo wasome?
 
Back
Top Bottom