Segerea ndio hii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Segerea ndio hii

Discussion in 'Jamii Photos' started by MaxShimba, Jul 17, 2012.

 1. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Inaitwa nchongoma!!kazi ipo hapo kama unaumwa kuhara!!hatari sana aisee duu!pia DRC nasikia kuna hali kama hii huko magerezani!!hawa watakuwa mahabusu
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Hizi ndio Jela za Kibongo? Ahhhhh si kuuwana huko? si watapata maradhi hao? Si akijamba mmoja si harufu itakuwa ni mbaya sana? Haya tutaendelea kweli? Mbuzi Mzee?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. mgodi

  mgodi JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,309
  Likes Received: 974
  Trophy Points: 280
  Hapo usiombe uwe umekutana na kesi ya kusingiziwa, kisha hakimu akakupa mvua kadhaa.
   
 5. Yegomasika

  Yegomasika JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2012
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 7,131
  Likes Received: 23,744
  Trophy Points: 280
  Hivi hawa watu wapo hai kweli, isije kuwa lile kasheshe lililotekea Haiti, na hao wote ni maiti.
   
 6. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Huwezi kucomfirm kwamba ni Segerea hapa mkuu, picha haitoshi kuthibitisha.
   
 7. Mmasihiya

  Mmasihiya JF-Expert Member

  #7
  Jul 17, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 368
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Hivi wakati wa kulala wanalala na pamba za kiraia sio zile pamba zao?
   
 8. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #8
  Jul 18, 2012
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,900
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Kama hali ndio hii basi ni vema polisi wakasitisha zoezi la kukamata wahalifu mpaka zitakapojengwa mahabusu nyingine,huu ni uuaji wa watuhumuwa....
   
 9. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #9
  Jul 18, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mkuu umena vyema sana, nakumbuka ilinikuta huko DRC hadi kuna mmoja alizimia kumwambia polisi eti akaona kelele akachukua maji akamwaga dah, watu walilala wima mpaka asubuhi.
   
 10. grafani11

  grafani11 JF-Expert Member

  #10
  Jul 18, 2012
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 15,534
  Likes Received: 342
  Trophy Points: 180
  Kwani maendeleo yanapatikana jela?
   
 11. grafani11

  grafani11 JF-Expert Member

  #11
  Jul 18, 2012
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 15,534
  Likes Received: 342
  Trophy Points: 180
  Waambie na hao wahalifu wenzio na wao waache kwanza mpaka napo zitakapojengwa mpya na kubwa za kukutosha.
   
 12. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #12
  Jul 18, 2012
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,900
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145  Eh nimekuwa mhalifu tena..??
   
 13. 1

  19don JF-Expert Member

  #13
  Jul 18, 2012
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 572
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  hapa ndio jf kila kitu raha
   
 14. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #14
  Jul 18, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  wewe hujuwi kuwa jela za ulaya Watu wakitoka ndani ya jela wanakuwa na pesa ? kuna kazi unafanya na unalipwa pesa nzuri kuliko ulivyokuwa nje upo huru jela za ulaya kuna shule ndani unajifunza mambo mengi tu hata ukitaka kujifunza computer waweza jela za kiafrika ni mateso ukitoka jela uu mgonjwa wa TB au ukimwi kutakuwa na maendeleo kweli katika nchi yetu kweli? Mkuu grafani11 Tembea ujionee wewe mwenyewe usingoje kuambia.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #15
  Jul 18, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [h=2]Magereza, Polisi wana hali ngumu sana: Wabunge[/h]
  Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe, amependekeza Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu wake wawekwe gerezani kwa muda wa miezi sita ili wapate uzoefu wa hali ilivyo mbaya kwenye magereza mbalimbali nchini.

  Aliyasema hayo jana wakati akichangia hotuba ya Wizara ya Mambo ya Ndani iliyowasilishwa bungeni na Waziri Dk. Emmanuel Nchimbi.

  Filikunjombe alisema iwapo mawaziri hao watawekwa gerezani basi wawe kwenye magereza ya Ludewa ambayo yanahali mbaya sana ili wakitoka wajue hali halisi inayozungumzwa na wabunge.

  Filikunjombe alisema mawaziri wa wizara hiyo kabla ya kuteuliwa wawekwe magerezani angalau kwa miezi sita hali itakayowawezesha kujua hali mbaya iliyoko magerezani na kutafuta ufumbuzi wa matatizo hayo.

  "Waziri akifungwa naomba afungwe gereza la Ludewa ili ajue mazingira magumu ya kule maana inafika wakati huwezi kutofautisha mfungwa ni yupi na askari magereza ni yupi, mheshimiwa Spika hali ni mbaya sana magerezani, sitaunga mkono hoja hii hadi nipate maelezo ya kuridhisha," alisema.

  Kuhusu Jeshi la Polisi, mbunge huyo ambaye aliwahi kufanyakazi katika jeshi hilo, alisema lina vifaa duni na halina uwezo wa kukabiliana na wahalifu ambao wanatumia teknolojia ya kisasa kutekeleza uhalifu wao.

  "Nilikuwa askari nayajua fika mazingira ya jeshi hilo, hawana vifaa vya kutosha, vifaa vingi walivyo navyo ni virungu tu sasa sijui kwa ajili ya kuwapiga wanafunzi wa vyuo vikuu wanapoandamana au kuwapiga Chadema," alisema.

  Alisema ni heri kuwa na Jeshi lenye askari wachache lakini wenye tija kuliko kuwa na jeshi kubwa linalojiendesha kizamani na ambao wanashindwa kupambana na wahalifu.

  Mbunge wa Mwibara (CCM), Kangi Lugola, alisema ndani ya Jeshi la Polisi kuna mtandao mkubwa wa uhalifu na ana ushahidi wa baadhi ya askari walioko kwenye mtandao huo.

  Lugola ambaye alianza kwa kutangaza kutoiunga mkono bajeti hiyo, alimtaja askari Fadhil Kweka kuwa mmoja wa wanamtandao huo na amekuwa akiwasaidia majambazi kwa kuwatajia majina ya wananchi wenye silaha ili wakawapore.

  Alisema udhaifu wa utendaji wa polisi unachangiwa sana na vifaa duni na kwamba angalau vifaa vingi ambavyo jeshi hilo wanavyo ni filimbi na virungu.

  "Mheshimiwa Spika wahalifu ni wadau wakubwa sana wa wizara hii, hivi sasa wanasikiliza kwa makini tunapanga bajeti kiasi gani kwa ajili ya kupambana nao, wao wanajipanga kufanya uhalifu kwa teknolojiaa ya kisasa, sisi jeshi letu la filimbi na virungu hatuwezi kufika," alisema.

  Alishauri viwekwe vifaa vya kisasa zikiwemo kamera kwenye miji mikubwa ya Dar es Salaam ili askari wazitumie kuangalia mwenendo wa matukio ya uhalifu.

  Wabunge wengi waliochangia hotuba hiyo walieleza namna ambavyo Polisi wanafanyakazi katika mazingira magumu ikiwemo ukosefu wa nyumba za kuishi pamoja na vifaa.

  CHANZO: NIPASHE ​


  :msela:
   
 16. steveachi

  steveachi JF-Expert Member

  #16
  Jul 18, 2012
  Joined: Nov 7, 2011
  Messages: 4,128
  Likes Received: 1,726
  Trophy Points: 280
  kighetghetoo ,enzi zileee nahustle about lyf now i own vogue,banglou la maana,ngada ndo mpango,
   
 17. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #17
  Jul 18, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,966
  Likes Received: 1,858
  Trophy Points: 280
  namia pia naona kama ni maiti mkuu.
   
 18. F

  Fofader JF-Expert Member

  #18
  Jul 18, 2012
  Joined: Sep 28, 2011
  Messages: 838
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 45
  Angalia mmoja mguu uko juu. Mwingine ana dalili ya kuvimba.
   
 19. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #19
  Jul 18, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  mboni wapo sawa kabisa..
   
 20. grafani11

  grafani11 JF-Expert Member

  #20
  Jul 20, 2012
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 15,534
  Likes Received: 342
  Trophy Points: 180
  Mkuu ungeleta hoja ya Jela moja huko Majuuu wala nisingesema chochote, lakini hoja hapa ni Gereza la Segerea Mkuu, hapo hakuna kujifunza chochote zaidi ya kuwa mende tu.
   
Loading...