Security Notice: Fanyeni haya Kujilinda!

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,520
86,081
Wakuu, Nakumbuka niliwahi kuandika kitu kama hiki iwakati wa Uchaguzi uliopita lakini kwa bahati mbaya sana sana Ndugu yangu, Rafiki yangu Mohamedi Mtoi alipata ajali siku chache baadae, ajali ambayo haikuacha jereha mwili mwake ilikua mwezi wa tisa mwaka 2015. Pumzika kwa amani Kaka Chabebi.

Leo hii napenda tuangazie mambo mawili matatu ambayo huenda yakatusaidia kupunguza au at least kujiweka salama kidooogo kutokana na hali kuwa mbaya zaidi, si vibaya kuyaangalia kwa ufupi tu;
  • Hakikisha unapeleka gereji gari yako mahali ambapo ni salama, waweza kumtuma kijana wako wako akafanya usimamizi au mtu wa karibu sana ili kuhakikisha matengezo au service iliyokusudiwa unafanyika kwa usahihi, hii itapunguza uwezekano wa mambo mawili ya haraka haraka, MOJA, kulegezewa baadhi ya spare na hivyo kuongeza uwekezano wa kupata ajali ukiwa safarini, PILI, kupunguza uwezekano wa kufungiwa "Tracking device" na ukawa tracked kwenye mizunguko yako yote.
  • Hakikisha hupeleki gari service kisha ukasafiri muda huo huo yaani unatoka gereji unaingia barabarani na kuanza safari ndefu, at least jipe muda wa kuweza kui-monitor gari yako na ikiwezeakana ipeleke kwa mtu mwingine aikague pia.
  • Funga Camera, mbele na nyumba na hakikisha zinafanya kazi kwa kila wakati, niliwahi kuangalia kipindi kinaitwa "The Witness that never Lies" huyu shahidi ambaye sio muongo ni CCTV. inasaidia sana jitahidi sana kufunga iwe ni camera kwenye gari au mahali pako pa kazi au nyumbani.
  • Jitahidi kuwa na vifaa vidogo vidogo vya usalama kama kalamu zenye camera, saa, miwani n.k hivi vinasaidia sana sana kurekodi baadhi ya matukio, ni nani anajua lini kitatokea wapi na kwa jinsi gani??
  • Jitahidi sana sana kuitumia simu yako vizuri, kwa mfano baadhi ya Simu "Smartphone" zina ile huduma ya dharura ambayo ukiwa kwenye dharura unaweza kui-command let us say, una press One kwa sekunde kadhaa kisha inarekodi vidio na kuzituma kwa namba ambazo utakua umezihifadhi na kuomba msaada, hii inatakiwa pia uwe umeiwezesha GPS kwahio mtumiaji au rafiki yako atapata picha au vidio na GPS location ulipo kwa muda huo. Ina uwezo wa kutuma kwa kipindi kirefu tu. Hivyo simu inaweza kuwa kombozi pia
  • Je, unapenda kutembelea wapi? hakikisha eneo unalotembelea ni salam kwako, hakikisha unaweza kuangalia mazingira ambayo risk ni ndogo. Usiende kila mahali, usikubali kuitikia kila wito.
  • Je marafiki zako ni akina nani? mnahusianaje? Mna muda gani katika urafiki wenu? Ni kipi hasa kinawaunganisha? Hapa angalia sana sana unaweza kutengenezewa rafiki kwa miezi sita. Kwa mfano, mmekutana JF kwenye PM kisha faster faster urafiki usio na kichwa wala miguu unashamiri, mnapanga kuonana, kisha.....nani anayejua???
  • Mwisho, acha kumakinikia (Concentrate) kwenye simu au laptop ukiwa safarini; jitahidi sana kuangalia watu unaopishana nao njiani, nani anakufuata njiani, anakupitaje, speed yake ikoje? Kisha hakikisha kila mara uko suspicious
Get well Tundu Lissu
 
Kwa ' Mafia ' na ' Majasusi ' waliobobea na kutukuka hakuna ambalo litaweza kuwazuia Wao kutekeleza walitakalo kulingana na hayo maelekezo yote ya ' Kiusalama / Kiulinzi ' uliyoyatoa hapo. Usijidanganye wakikutaka wanakupata muda wowote, mahala popote na siku yoyote. Kila la kheri.
 
Najua sana ndio maana nikatumia neno "Kupunguza" hahahahah ungesoma ungeona na kuelewa Mpwa, usisome ili kujibu soma ili kuelewa. Blessed
 
Unapaparika kujipa ulinzi woote huo,watu wanamtumia mkeo anakumaliza,dunia duara
 
Kwa ' Mafia ' na ' Majasusi ' waliobobea na kutukuka hakuna ambalo litaweza kuwazuia Wao kutekeleza walitakalo kulingana na hayo maelekezo yote ya ' Kiusalama / Kiulinzi ' uliyoyatoa hapo. Usijidanganye wakikutaka wanakupata muda wowote, mahala popote na siku yoyote. Kila la kheri.
Angalau inapunguza risk
 
Najua sana ndio maana nikatumia neno "Kupunguza" hahahahah ungesoma ungeona na kuelewa Mpwa, usisome ili kujibu soma ili kuelewa. Blessed

Chezea wote duniani ila siyo ' Mafia ' na ' Majasusi ' kwani huwa hawakosei kwa wakitakacho kwani umakini wao ni wa Kutukuka.
 
Kwa ' Mafia ' na ' Majasusi ' waliobobea na kutukuka hakuna ambalo litaweza kuwazuia Wao kutekeleza walitakalo kulingana na hayo maelekezo yote ya ' Kiusalama / Kiulinzi ' uliyoyatoa hapo. Usijidanganye wakikutaka wanakupata muda wowote, mahala popote na siku yoyote. Kila la kheri.
Shetani anabishana na Mungu kwa jambo la Ayubu.
 
Hakuna chochote ni upumbavu tu, si kila mtu unayempangia mission unaweza kukamilisha mission yako salama, mara nyengine utakumbana na vikwazo vikubwa tofauti na ulivyotarajia.
kweli kabisa
 
Back
Top Bottom