Secret lover huyu mmhh!!

Secret lover huyu mmhh!!

mkunde my dear usipende kuintatein kila kitu maishani! wewe ni mke wa mtu una mume na mtoto..haya maisha ya matongozo ulishatoka huko..labda uniambie kitu upo tayari kumdate mtu! wanaume ni watu wa ajabu huyo mbaba hana adabu hata tano...mke wa mtu unaweza kumfanyia huo udaku kweli ooh my sister my sister kama ana dada aliepotea akatoe tangazo kipindi cha bango tbc one1! pls kimbia maisha ni haya haya atakumega hapo atatangaza ofisi nzima ..yatafika kwa mumeo na jamaaa utabaki alone hujui pa kutokea!
Smile nawe umeolewa kama mkundeoriginal ? Hata mie nimekupenda bila kumsahau miss strong na kama kawa Madame B .
Naombeni urafiki.
 
Habari zenu wapendwa,
Hope mko salama na mnaendelea na shuhuli zenu. Mie bana mwezi wa saba mwaka huu ni nilifanya interview kampuni flani hivi na mwezi wa tisa nilipigiwa simu kuwa nimepata kazi na niliripoti ofisi mpya kuanza kazi mara moja. Ofisi mpya iko advanced yaani wanaishi kizungu zungu sharing and caring kwa sana. Sasa tangu nimeripoti mie nasoma mazingira na tabia za watu kwanza. Two weeks later nikaanza kukuta message kwenye dawati langu na parcels from secret lover kumuuliza secretary na staff wengine wakaniambia hiyo ni kawaida ya hiyo ofisi kumkaribisha mgeni na huwa kuna mtu akikupenda basi huwa anaanza kujiintroduce kwa kushow care kisha mwisho wa siku atajitokeza na kukuomba muende wote lunch au evening tea.
Muda wote huo nilikuwa nakuta fresh flowers na kimessage kikinitakia siku na kazi njema, siku ingine nakuta piece of cake au biskuti au juice ilikuwa ni vitu vidogovidogo vya kutafuna. Nilikuwa nafungua na tunagawana na wenzangu pale ofcn kujiridhisha kama kina madhara kitudhuru wengi.
Sasa bana jana ile nafika asubuhi secret lover akaniwekea fresh flowers na message kuwa anaomba tutoke lunch atakuja kunipick saa saba mchana. Ilipofika saa saba akaja loohhh!!! nilishindwa kunyanyuka kwa dakika kama 3 hivi naduwaa..........!!! Kumbe ni kaka mmoja hivi sikuamini hata akaniomba twende lunch, nikamwambia naomba dakika tano anisubiri nje akasema hapana nakusubiri hapahapa. Nilitaka nipige simu ila nikaghairi nikanyanyuka tukaenda watu wengine ofisini kila mtu yuko busy. Tulipofika nje akanifungulia mlango kwenye gari yake tukaenda lunch and within the lunch tukaongea meeengi ila aliloniambia ''TANGU UMERIPOTI HAPA OFISINI NILIKUPENDA NAKUFANANISHA SANA NA DADA YANGU TULIZALIWA MAPACHA NA YEYE ALIOLEWA HUKO RUSSIA ILA HAJARUDI TANZANIA TANGU AENDE HUKO WALA MAWASILIANO HAYAPO TENA. NILIPOKUONA NILIFURAHI KUWA MUNGU KANILETEA PACHA WANGU NIKASIKIA KUKUPENDA KAMA PACHA MWENZANGU HIVYO NAOMBA UWE PACHA WANGU TAFADHALI.''
Nilitabasamu nikamwambia pole kuhusu dada yako hope siku moja atarudi nyumbani kuwasalimu alinionesha passport picha ya dada yake kweli tulifanana hasa tabasamu nami nikamjibu usikute na mie ni dada yako wa damu tunashea baba huwezi jua labda baba yako alipata kufahamiana na mama yangu miaka hiyo. Nikamwambia hivyo mie ni dada yako uwe na amani, akafurahi akanikumbatia tukarudi ofcn.
Secret lover huyu kaniacha na maswali kichwani............................... anaweza kuwa kaka yangu kweli lakini ntaanzaje kumuuliza mama?
Nimeshare na nyie maana kimenikaa kooni siwezi mwambia mtu yeyote, ukiona nimekupotezea muda kusoma ulichoandika nipotezee kwangu mie nimerelease moyo wangu na sasa naweza endelea na kazi.
Always
Mkunde Originale.

Si.mgefanana majina au na wewe umeshaanza kumpenda mzinifu mwenzio?
 
Dada yake wa hadithini kwi kwi kwi kwi in brackets isomeke "ex mupenzi"

Ni pacha wake bwana na shemeji wa abroad kataifisha!
Hiyo kwenye brackets ndio mmeshasoma between the lines?
Watu wabaya!!!
 
Chezeya njemba weye!! Wanapokuwa wanamsamrandia mrembo....baadhi huingia kwa gia yoyote ile bila kujali athari zake.

Ni pacha wake bwana na shemeji wa abroad kataifisha!
Hiyo kwenye brackets ndio mmeshasoma between the lines?
Watu wabaya!!!
 
...aonywaye mara nying akishupaza shngo huvunjika... Smile ashasema yote.
 
Last edited by a moderator:
Yanini kumstua bana!!! Anaenda naye mdogomdogo huku akifurahia maua mazuri na vitafunwa toka kwa njemba lol!!

he! kumbe ni mke wamtu, kwanini hukumwambia huyo msiri?
 
Hivi inakuwaje unafahamu fika ni mke wa mtu. Inakuwaje unajichekesha kwa wanaume? hujui ndio mwanzo wataanza kukudharau na matokeo yake unaishia kushikwa shikwa. aaawww
 
duuh hata mbuyu ulianza kama mchicha,mchekee tu uje kuharibu ndoa yako.muhurumie mumeo yaani nilivyosoma post yako nimepata hasira balaa nikajiona mm ndiye mumeo uliyeniaga unaenda kazin kumbe umetolewa offer na mchizi mwingine.ukija kuachwa utamlaumu mumeo?? umepata bahati ya kuolewa jiheshimu wengi wanaillia hyo chance.nataman ningekuwa mumeo then nasoma hii post yako au namjua mumeo ningemwambia aiseee
 
mkunde my dear usipende kuintatein kila kitu maishani! wewe ni mke wa mtu una mume na mtoto..haya maisha ya matongozo ulishatoka huko..labda uniambie kitu upo tayari kumdate mtu! wanaume ni watu wa ajabu huyo mbaba hana adabu hata tano...mke wa mtu unaweza kumfanyia huo udaku kweli ooh my sister my sister kama ana dada aliepotea akatoe tangazo kipindi cha bango tbc one1! pls kimbia maisha ni haya haya atakumega hapo atatangaza ofisi nzima ..yatafika kwa mumeo na jamaaa utabaki alone hujui pa kutokea![/QUOTE
Smile nimekupenda bure vile hauko mvivu kufikiria naomba uwe rafki yangu khaa..
shost mi na wewe si dam dam ! au hili tongozo limekuchanganya
 
Hivi inakuwaje unafahamu fika ni mke wa mtu. Inakuwaje unajichekesha kwa wanaume? hujui ndio mwanzo wataanza kukudharau na matokeo yake unaishia kushikwa shikwa. aaawww
umeona eeeh yaani sipati picha mke wa mtu unavosogezewa kiti ukae ! mara umeletewa maua na choklate..yaani ni vile huyu mkunde original naheshimiana nae hapa jf ..ningetukanaje! nimeumia utadhani ni mimi
 
Ana shida zake kiswahili rahis kakutamani ningalikuwa mim nisingali. Kula vya watu mana mwishowe uliwe nawe japo vyako
 
Back
Top Bottom