Secret lover huyu mmhh!!

Mkunde Original

JF-Expert Member
Jul 20, 2013
807
645
Habari zenu wapendwa,
Hope mko salama na mnaendelea na shuhuli zenu. Mie bana mwezi wa saba mwaka huu ni nilifanya interview kampuni flani hivi na mwezi wa tisa nilipigiwa simu kuwa nimepata kazi na niliripoti ofisi mpya kuanza kazi mara moja. Ofisi mpya iko advanced yaani wanaishi kizungu zungu sharing and caring kwa sana. Sasa tangu nimeripoti mie nasoma mazingira na tabia za watu kwanza. Two weeks later nikaanza kukuta message kwenye dawati langu na parcels from secret lover kumuuliza secretary na staff wengine wakaniambia hiyo ni kawaida ya hiyo ofisi kumkaribisha mgeni na huwa kuna mtu akikupenda basi huwa anaanza kujiintroduce kwa kushow care kisha mwisho wa siku atajitokeza na kukuomba muende wote lunch au evening tea.
Muda wote huo nilikuwa nakuta fresh flowers na kimessage kikinitakia siku na kazi njema, siku ingine nakuta piece of cake au biskuti au juice ilikuwa ni vitu vidogovidogo vya kutafuna. Nilikuwa nafungua na tunagawana na wenzangu pale ofcn kujiridhisha kama kina madhara kitudhuru wengi.
Sasa bana jana ile nafika asubuhi secret lover akaniwekea fresh flowers na message kuwa anaomba tutoke lunch atakuja kunipick saa saba mchana. Ilipofika saa saba akaja loohhh!!! nilishindwa kunyanyuka kwa dakika kama 3 hivi naduwaa..........!!! Kumbe ni kaka mmoja hivi sikuamini hata akaniomba twende lunch, nikamwambia naomba dakika tano anisubiri nje akasema hapana nakusubiri hapahapa. Nilitaka nipige simu ila nikaghairi nikanyanyuka tukaenda watu wengine ofisini kila mtu yuko busy. Tulipofika nje akanifungulia mlango kwenye gari yake tukaenda lunch and within the lunch tukaongea meeengi ila aliloniambia ''TANGU UMERIPOTI HAPA OFISINI NILIKUPENDA NAKUFANANISHA SANA NA DADA YANGU TULIZALIWA MAPACHA NA YEYE ALIOLEWA HUKO RUSSIA ILA HAJARUDI TANZANIA TANGU AENDE HUKO WALA MAWASILIANO HAYAPO TENA. NILIPOKUONA NILIFURAHI KUWA MUNGU KANILETEA PACHA WANGU NIKASIKIA KUKUPENDA KAMA PACHA MWENZANGU HIVYO NAOMBA UWE PACHA WANGU TAFADHALI.''
Nilitabasamu nikamwambia pole kuhusu dada yako hope siku moja atarudi nyumbani kuwasalimu alinionesha passport picha ya dada yake kweli tulifanana hasa tabasamu nami nikamjibu usikute na mie ni dada yako wa damu tunashea baba huwezi jua labda baba yako alipata kufahamiana na mama yangu miaka hiyo. Nikamwambia hivyo mie ni dada yako uwe na amani, akafurahi akanikumbatia tukarudi ofcn.
Secret lover huyu kaniacha na maswali kichwani............................... anaweza kuwa kaka yangu kweli lakini ntaanzaje kumuuliza mama?
Nimeshare na nyie maana kimenikaa kooni siwezi mwambia mtu yeyote, ukiona nimekupotezea muda kusoma ulichoandika nipotezee kwangu mie nimerelease moyo wangu na sasa naweza endelea na kazi.
Always
Mkunde Originale.
 
hizo swagger zake.....eti umefanana na dada yke lol???labda na hv umeoneshwa picha ukajiona kama ww basi umeingiwa na imani hyo........wanaume wana mbinu ukae ukijua!!!

asubiri tu siku atakayopigwa na dushelele
chezea wanaume weye
 
Mkunde Original,

Acha fix bana we bishost.......

wewe umetongozwa na huyo mkaka,

sema unatuletea swaga zako tu hapa.....

kama vipi, we msikilize tu....ndo mapito yenyewe hayo!
 
mhhhh mtu ashakolea hapo,wewe usishangae kutongozwa unashangaa undugu?kweli hii imekaa sawa wachambuzi wenzangu?au haya tunayoletewa hapa ni manyoyaa...kuku kashaliwa......................!!
Ehhh..... back tu Mkunde original swali muhimu vipi umeshamkubalia au ndo unamfikiria??
 
anataka uwe dada ake........mie hapo nahisi kama anakupenda vile

anajua that your married.....but I know this can not stop him from loving you
mimi ndo maana sitaki kuoa kama wanawake wenyewe shobo hivi.....unashikwa mahala bado unachekelea tu mke wa mtu..au na wewe baby wakikuletea maua unapokeaga huko ofisini kwako?
 
Back
Top Bottom