WEKENI PROTECTOR SIMU ZENU, NARUDIA WEKENI PROTECTOR SIMU ZENU!
Wakuu ninaandika hapa ni kijana mwenye uzoefu wa kupasua vioo vya simu zake, mpaka sasa nimepasua vioo vinne vya Samsung tofauti sababu kuu ni kudharau kazi ya PROTECTOR niliamini ni Upigaji na kuharibu Muonekano wa simu.
Nilishauriwa sana lakini nilikaza kichwa na kukaidi ushauri lakini nikajionea jamani,
10,000 ya PROTECTOR ilinigharimu Malaki ya Pesa.
Niliangusha NOTE 5, toka juu ya kitanda mpaka chini (kitanda cha Dabo Deka), asee ilizima palepale nilihisi uchungu wa kufa mtuu nikaapa sitarudia kudharau PROTECTOR. Nikaenda dukani kuulizia bei ya kioo ikanishinda nikaona heri ninunue Simu mpya.
Nikajiseti nikanunua SAMSUNG S6, kalikua na muonekano mzuri Wallahi kasimu kametuliaaa Mang'anyuu na karangi ka Gold, nilizidi kuipenda ile simu kila nilipoitazama yani hapa sikuweka PROTECTOR wala COVER, niliamini ningeharibu muonekano wa kasimu kangu.
Ikatokea siku iso na jina Ikaanguka ikiwa na wiki 3 tu au 4 toka ninunue, aseeeeeeeeeee niliumia sana. Lakini nikaapa sitanunua simu nyingine nitatengeneza ile na nitadumu nayo.
Kuulizia kioo nikaambiwa 160K kariakoo, siku hiyo rafiki yangu akaninunulia PROTECTOR kwa pesa yake akiamini ningeangusha tena. wakaniwekea kioo FEKI, aseeeeeeeeeee simu ilipoteza muonekano wadau wakawa wananicheka eti walidai hawaielewi simu yangu sio Tecno, Sio Samsung.
Nikatoa PROTECTOR, hatukukaa muda nikapasua kioo kwa kuegemeza kitu juu ya simu, wino ukivuja simu ikawa haieleweki tena, nikakomaa nikaenda k/koo nikatafuta kioo OG mpaka nikakipata fundi akafunga nikadunda nayo huku nikiapa kuwa Nitaitunza, nitailinda na kuitetea S6 yangu siku zote za maisha yangu. Bado sikuweka PROTECTOR ila nashukuru ilidumu mpaka nikaiuza.
Kwa mafunzo nlopitia nawasihi ndugu zangu muweke PROTECTOR simu zenu.
Nimalize kwa kusema 'Simu bila PROTECTOR ni sawa na kufanya Mapenzi bila KONDOM'
KAMA UNAIPENDA UTAILINDA!