Scorpion anayetoboa watu Macho Buguruni, akamatwa

Scorpion anayetoboa watu Macho Buguruni, akamatwa

Huyu Mjinga hafai hata kurudi Uraiani wamfunge hata miaka 100 afie jela.
 
Kamanda wa polisi kanda maalum ya mkoa wa Dar es Salaam, Simon Sirro amesema jeshi lake limemkamata mtuhumiwa ‘Scorpion’ anayetuhumiwa kuhusika katika tukio la kumtoa macho, kumchoma visu na kumpora mfanyabiashara Said Ally katika maeneo ya Buguruni Sheli.
Kamanda Sirro ametoa kauli hiyo Jumapili hii Buguruni kwa Mnyamani, jijini Dar es Salaam, wakati wa mkutano wa kujadili usalama katika eneo hilo ulioandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Video ya mtuhumiwa akielezea kisa chake

Alisema mtuhumiwa huyo anayejulikana kwa jina maarufu kama ‘Scorpion’ alikamatwa baada ya polisi kupewa taarifa za matukio ambayo ameyafanya ikiwemo la kumchoma kisu, kumtoa macho na kumsababishia upofu, Said Ally.

“Nimesikia wananchi wanalalamika hapa kuwa tumeshindwa kumkamata Scorpion, ni nani kwa Jeshi la Polisi asikamatwe? Tayari tumemkamata na sheria itachukua mkondo wake, hakuna mtu anayeweza kushindana na jeshi,” alisema Kamanda Sirro.

Aidha Sirro alisema baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo na kuhojiwa aliutaja mtandao wake wote na tayari wameukamata. Awataka wakazi wa eneo hilo kutokuwa na hofu kwani mtuhumiwa huyo hayupo tena katika eneo hilo.

“Najua suala hili bado lipo mahakamani hatuwezi kulizungumzia sana, bahati nzuri alipokamatwa alieleza aliyoeleza na tukafanikiwa kuukamata mtandao wote, hivyo hakuna haja ya kuwa na uwoga eneo hili lipo salama,” aliongeza.
 
duuuuh hivi ni kweli wananchi walikuwa kimya bila kumsaidia? basi buguruni kuna wakatili sana
 
Wanajamvi tuache sheria ichukue mkondo wake na kuhamasisha wananchi wakatoe ushahidi ili apatikane na hatia huyo asiye na tofauti na gaidi
Hakuna hapa.......yeye alifuata sheria wakati anamfanyia mwenzake ubaya........huyo ni wakumpeleka buguruni pale watu wanashika magongo wanaanza kutembeza kichapo..........piga huyo mbwa hadi awe nyama ya kusaga.......halafu hiyo maiti yake wanakwenda kulisha mbwa mwitu au simba huko porini.......mbwa kabisa huyo natamani nilione sura yake paka shume hilo halafu nilinase kofi moja.....
 
Sehemu zingine watu hujichukulia sheria mkononi kuwa poteza duniani wajinga kama huyo maana kumpeleka magereza ni sawa na kuendelea kumfuga!

wewe unataka Mh auawe..?ikiwa hivyo chadema na hakli za binadamu watamshitak Magufuri huko marekani na ulaya
 
Hawa wababe mbona hawaendi kule Ukuryani Ukonga? Wanapiga wanaume wa dar mitaa ya huku waambie waje ukonga aone moto wa wakurya
 
Sehemu zingine watu hujichukulia sheria mkononi kuwa poteza duniani wajinga kama huyo maana kumpeleka magereza ni sawa na kuendelea kumfuga!
Picha ya huo scopion iko wapi? Nashukuru polisi kwa kimkamata, ila naomba picha yake kama kweli ka kamatwa. Watu bado tunauoga!
Kuhusiana na tukio la Hekaheka ya jana kuhusu Mwanaume mmoja mkazi wa Ubungo Makuburi Saidi almaarufu baba D kujeruhiwa vibaya na kutolewa macho na Mbabe mmoja wa Buguruni anayejiita Scorpion tena mbele za watu na hakuna hata mmoja aliyejitokeza kumsaidia kwa madai ya kamba huyo Scorpion anaogopeka na watu wote maeneo hayo ya buguruni.

Idara ya Hekaheka ikishirikiana na website yako pendwa geahhabibu.co.tz imefika eneo la Buguruni kwa mnyamani ambapo ndipo tukio hilo lilifanyika nakuweza kuongea na baadhi ya wananchi wa waeneo hilo kutaka kujua zaidi kuhusiana na huyo jamaa anayejiita scorpion imekuaje mpaka mtu anapigwa hadi kutolewa macho mbele yao bila wao kutetea chochote.

Wengi wao hawakuwa tayari kumuongelea kutokana na hofu waliokuwa nayo juu ya mtu huyo na hata hao waliokubali walijikuta wakielezea kwa kujificha bila kutaka kujulikana.

Wakazi hao wa Buguruni walidai kuwa jamaa ni mtaalamu wa mambo ya ngumi na huwa haogopi mtu yoyote hata mkienda wengi yeye ndio anafurahi.Vilevile walieleza kuwa hilo ni tukio lake la tatu la kumjeruhi mtu na kumtoa macho alishawahi kumvunja kiuno na mkono mwanamke mmoja.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala Salum Hamdani amethibitisha kukamatwa kwa jamaa huyo ambapo anasema kwa sasa yupo ndani Magereza na kesi yake itasomwa tena tarehe 5 mwezi wa 10 2016.

Ni kweli hilo tukio limetokea na polisi tayari walishachukua hatua kwa maana ya huyo mtuhumiwa Scorpion jina lake halisi anaitwa Salum Mpepe alikamatwa siku ya tarehe 12 mwezi wa 9 akawa pale kituo cha polisi Buguruni wakati upelelezi ukiendelea tarehe 23 mwezi wa 9 alifikishwa mahakami na kusomewa jinai namba 276 unyanganyi kwa kutumia silaha, yupo magereza kesi yake itatajwa tena tarehe 5 mwezi wa 10 2016.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe.Paul Makonda zimemfika taarifa hizi ambapo yeye pamoja na Idara ya Hekaheka kupitia Leoetena ya Cloudsfm tutaungana kwa pamoja siku ya jumapili saa tisa jioni kwenda kuongea na wakazi wa Buguruni ili kuweka sawa mambo haya ya uhalifu yanayoendelea mtaani
 
Acheni kumuogopa na kumpamba huyu sijui SCORPION wenu huko Buguruni na kusema kuwa hakamatiki. Sidhani kama huyo SCORPION wenu anafikia ' UKATILI ' wa Mtu mmoja ' TISHIO ' na ' HATARI ' anaitwa MBUZI YAKE KAMBA aliyekuwa akitikisa Kawe nzima na vitongoji vyake na kuna wakati kwa Uwoga tu Watu walikuwa wakipishana nae barabarani wanamsalimu na kumwambia tafadhali MBUZI YAKE KAMBA leo nina Simu nzuri na HELA mfukoni chukua tu. Kwa wale waishio KAWE nadhani watakuwa wanaelewa ninachokisema kwani huyu Jamaa hata Police tu wa Kawe walikuwa wanamwogopa ila tunashukuru kwa ujio wa Kamanda mpya SIRO na Mkuu mpya wa Kituo cha Kawe kwa kushirikiana na Wananchi kadhaa waliojitoa mhanga walishirikiana hadi wakafanikiwa kumkamata huyo MBUZI YAKE KAMBA na sasa yupo SEGADANSI nadhani Ukonga au Keko.

Hakuna MAASI ambayo huyu Jamaa MBUZI YAKE KAMBA wa Kawe hajayafanya na nakumbuka hata siku ile alipokamatwa tu sehemu mbalimbali za Kawe Wakazi walikuwa wakifanya Sherehe na kuna hata baadhi ya Police walisikika wakisema kuwa sasa WATAPUMUA. Nimeshamfuatilia huyo SCORPION wenu ila kwa aliyokuwa anawafanyia wana Buguruni miaka hii ya karibuni mwenzake MBUZI YAKE KAMBA wa huku Kawe aliyafanya miaka kumi ( 10 ) iliyopita.

Huyo SCORPION wala hashindikani kukamatika au kuchukuliwa hatua ila inaonyesha dhahiri kuwa nyie Wakazi wa Buguruni hamna Ushirikiano halafu yawezekana pia kuna Mtu au Mamlaka fulani inamlinda kwa minajili kuwa labda wanakula nae pale anapofanikisha ' tukio ' fulani lenye ' mtonyo ' wa maana. Nijuavyo Buguruni ndiko kumejaa ' Masela ' wa maana sasa inakuwaje mnlishindwa au mnashindwa kumdhibiti huyo SCORPION wenu?

sasa uyo SCORPION ange wekwa gereza moja na MBUZI YAKE KAMBA chumba kmoja mtu bee tu {2} af wakatumikia kifungo umo dan cjui ingekuwa 3RD world war
 
Hawa wababe mbona hawaendi kule Ukuryani Ukonga? Wanapiga wanaume wa dar mitaa ya huku waambie waje ukonga aone moto wa wakurya

Kule kuna ma ANACONDA kabla hajapelekwa polsi angekuqa kisha tendewa alcho kitenda x100
 
Kamanda wa polisi kanda maalum ya mkoa wa Dar es Salaam, Simon Sirro amesema jeshi lake limemkamata mtuhumiwa ‘Scorpion’ anayetuhumiwa kuhusika katika tukio la kumtoa macho, kumchoma visu na kumpora mfanyabiashara Said Ally katika maeneo ya Buguruni Sheli.
Kamanda Sirro ametoa kauli hiyo Jumapili hii Buguruni kwa Mnyamani, jijini Dar es Salaam, wakati wa mkutano wa kujadili usalama katika eneo hilo ulioandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Video ya mtuhumiwa akielezea kisa chake

Alisema mtuhumiwa huyo anayejulikana kwa jina maarufu kama ‘Scorpion’ alikamatwa baada ya polisi kupewa taarifa za matukio ambayo ameyafanya ikiwemo la kumchoma kisu, kumtoa macho na kumsababishia upofu, Said Ally.

“Nimesikia wananchi wanalalamika hapa kuwa tumeshindwa kumkamata Scorpion, ni nani kwa Jeshi la Polisi asikamatwe? Tayari tumemkamata na sheria itachukua mkondo wake, hakuna mtu anayeweza kushindana na jeshi,” alisema Kamanda Sirro.

Aidha Sirro alisema baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo na kuhojiwa aliutaja mtandao wake wote na tayari wameukamata. Awataka wakazi wa eneo hilo kutokuwa na hofu kwani mtuhumiwa huyo hayupo tena katika eneo hilo.

“Najua suala hili bado lipo mahakamani hatuwezi kulizungumzia sana, bahati nzuri alipokamatwa alieleza aliyoeleza na tukafanikiwa kuukamata mtandao wote, hivyo hakuna haja ya kuwa na uwoga eneo hili lipo salama,” aliongeza.

Shit!shit! Mbona kama nimemuona Buguruni Marapa leo jioni? Au ni pacha wake yule?😳😱
 
Anastahili adhabu kali ili iwe fundisho na kwa wengne pia wenye tabia Kama hizo katka jamii
 
Ila nashangaa sana hao raia na wafanyabiashara wahio sehemu inamaana wanashindwa mdihibiti huyo psycho kisa mpiga ngumii that a damn shame
 
Back
Top Bottom