Scientific fact na knowledge Thread

Ukiwa umesinzia hasa wakati wa REM(Rapid eye movement) muda wa kuota ndoto kuna baadhi ya sehemu za ubongo huwa Zina chapa kazi(firing) kama vile hippocumpus( huchakata kumbukumbu), amygdala na limbic system(emotions), visual cortex( for visual dreams) lakini prefrontal context(logic) huwa inashutdown usije kuanza ubishi ndotoni ooh haiwezekani kupaa haha.
 
Una point ila namna ulivyo iwasilisha hata mimi sijaelewa
 
Ni galaxy kubwa iliyo karibu nasi, ikiwa umbali wa takribani miaka milioni 2.5 ya mwanga, ikumbukwe mwanga ndio kitu kinachosafiri kwa kasi zaidi, kikisafiri kwa umbali wa kilomita 300,000 km ( Laki tatu kwa sekunde) sawa na kilomita trilioni 9.46 kwa mwaka

Galaxy ni nini?
Galaxy kwa kiswahili majarra ni mkusanyiko mkubwa wa mabilioni ya nyota, gesi, vumbi la anga na dark matter (mada ya giza) vinavyoshikamana angani kwa nguvu ya uvutano.

Je? Andromeda Galaxy ina nyota ngapi?
Galaxy hii ina nyota zaidi ya trilioni moja, mara zaidi ya nne ya idadi ya nyota zilizopo katika galaxy yetu ya njia ya maziwa (Milky way)

Uonekanaji wake angani

Galaxy hii huonekana vizuri zaidi kipindi cha Oktoba hadi Desemba katika nchi zetu za kizio cha Kusini (Southern hemisphere), kuanzia saa mbili usiku na huonekana vizuri zaidi kipindi ambacho mbalamwezi haipo

Katika umbali wake wa miaka zaidi ya milioni 2.5 ya mwanga tunaiona kadiri ilivyokuwa miaka milioni 2.5 iliyopita kabla zinjanthropus hawajaanza kutembea duniani

Na pia ndiyo kitu cha masafa ya mbali au kitu cha mbali zaidi kinachoweza kuonekana kwa macho angani

Pia inakadiriwa kuwa ndani ya miaka bilioni 5 ijayo itagongana (collided) na galaxy yetu Milky way kwani kwa mujibu wa wanasayansi wa NASA ni kuwa galaxy hii ya Andromeda inasogea karibu na galaxy yetu ya Milky way kwa spidi ya takribani kilomita 124 kwa sekunde na ndani ya miaka bilioni 5 ijayo itagongana (collided) na galaxy ya mfumo wetu wa jua yaani Milky way
 
Na ndo maana ndoto hazimake sense, kama vile kutokujua ilipoanzia
 
Ndiyo, chukuliwa pangaboi la ndege ikiwa imetulia linaoneka kiwa yabisi (solid) lilianza kuzunguka kwa kasi unaanza kuona kilicho nyuma yake!
Yes, yes...
Why is that? Unakuwa umefanya particle za lile panga zitransform ama? Ile speed ya mwanga utokao kwenye surface ya panga inakuwa imezidiwa na kilichopo nyuma yake?
 
Katika habati za cosmos.

Inasemekana astronomers wakitumia hizo telescope zao wakifocus pale ambako kuna nafasi kati ya nyota( usiku ukiangalia angani utaona kuna vijinafasi kati ya nyota) basi hapo wanaona zaidi ya galaxy laki moja.

Inasemekana supernova huwa inatokea mara moja kwenye galaxy husika kila baada ya miaka Mia moja so astronomer akiwa na telescope yake usiku kucha anaweza kushuhudia nyota kuanzia moja hadi Tatu ziki explode(supernova).
 
Kwa hiyo kunauwezekano kuwa vitu tunavyoviona vikawa ni tofauti na uhalisia wake?
 
Hapana, unaweza kuuona uwepo wako bila ego na bado usitambue the absurdity or the impeenance of it all...that you're basically nothing. Emptiness
Ukisema “I am nothing,” umebadilisha ego tu umeipa jina la emptiness.

Awareness haiwezi kuwa nothing , Inaweza tu kuwa bila upofu wa ego, lakini bado ni uwepo unaojitambua.
 
Ukishajua tu kuwa ulimwengu una mwanzo utajidogosha. Na hicho ndo kinasukumwa
Hahaha hapana na ndio maana pia kuna theory ya big crunch ambapo ulimwengu unacolapse na kurudi kwenye point kama ilivyokuwa Kabla ya big bang. Yaani nothing is created nor destroyed its just manifest and unmanifest and the circle continues until forever.
 
Ukisema “I am nothing,” umebadilisha ego tu umeipa jina la emptiness.

Awareness haiwezi kuwa nothing , Inaweza tu kuwa bila upofu wa ego, lakini bado ni uwepo unaojitambua.
In Buddhism hatumaanishi emptiness ya kufikirika au ku conceptualize?

Ni dhana ya kujua kuwa even being aware of the self is an illusion to keep you hooked at ego

Najua utasema awareness ni being aware of awareness.

Je ni kuulize hiyo awareness ni nini?

Nothingness sio concept wala haiko atttached to anything. Ni kudrop kila kitu hata wazo lakujua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…