Sayari inayofanana na Dunia yagunduliwa

Sayari inayofanana na Dunia yagunduliwa

View attachment 387393
Wanasayansi wamegundua sayari ambayo inakaribia sana Dunia kwa mazingira na ukubwa wake na ambayo inazunguka nyota ijulikanayo kama Proxima Centauri, iliyo na mfumo unaokaribia zaidi mfumo wetu wa jua.

Sayari hiyo, ambayo kwa sasa imepewa jina 'Proxima b' inazunguka nyota hiyo katika eneo ambalo kuna uwezekano mkubwa sana wa kupatikana kwa maji.

Proxima inapatikana umbali wa kilomita trilioni 40 na inaweza kumchukua mtu, akitumia teknolojia ya sasa ya vyombo vya usafiri wa anga za juu, maelfu ya miaka kufika huko.

View attachment 387394

Licha ya kwamba ni mbali sana, kugunduliwa kwa sayari hiyo huenda kukasisimua hisia na mawazo ya binadamu na wanasayansi kuhusu kuwepo kwa viumbe katika sayari nyingine au uwezekano wa wakati mmoja watu kuishi kwenye sayari nyingine.

"Kusema kweli, kufika huko kwa sasa hiyo ni kama hadithi ya kubuni kisayansi, lakini watu sasa wanalifikiria hilo na si jambo lisiloweza kufikirika kwamba wakati mmoja huenda watu wakatuma chombo huko," Guillem Anglada-Escudé, ambaye kundi lake la Pale Red Dot limechapisha matokeo ya ugunduzi wa sayari hiyo katika jarida la Nature amesema.

Mapema mwaka huu, bilionea Yuri Milner alisema atawekeza $100m katika utafiti wa kuunda chombo au kifaa kidogo kinachoweza kusafiri anga za juu kwa kutumia teknolojia ya laser.

Chombo kama hicho kinaweza kusafiri kwa pengine asilimia 20 ya kasi ya mwanga na hivyo kufupisha safari ya kufika kwenye nyota kama vile Proxima Centauri kutoka maelfu ya miaka hadi miongo kadha.

Ugunduzi wa sayari hiyo ulifanikishwa kupitia darubini ya kisasa yenye kifaa kujulikanacho kama HARPS.

Darubini hiyo imewekwa nchini Chile.

Takwimu kutoka kwa darubini hiyo zinaonyesha uzito wa Proxima b huenda ukawa mara 1.3 zaidi ya uzito wa dunia na kwamba inazunguka nyota ya Proxima katika umbali wa kilomita milioni 7.5. Huchukua siku 11.2 kumaliza mzunguko mmoja.

Umbali kutoka kwa nyota hiyo na sayari hiyo ni mfupi ukilinganisha na umbali kutoka kwa Dunia hadi kwa Jua (kilomita 149 milioni). Lakini Proxima Centauri ni 'nyota nyekundu mbilikimo'. Si kubwa sana na nguvu zake si nyingi kama za Jua hivyo safari inaweza kuwa karibu na nyota hiyo lakini iwe na mazingira sawa na ya dunia.

Chanzo: BBC

Hawajagundua, wameiona. Maana iligunduliwa miaka 5300 iliopita pale misri na Mesopotamia. Ilikuwa inaitwa nibiru.

Kwa waerevu tunasema. U CANT SEE THE REALITY UNTIL OTHERWISE U HAVE ACCESSED THE MOTHER KNOWLEDGE.
 
ikitokea Tz ikahamia huko je watz mtapenda kwenda huko na jeshi gani la ulinzi?
 
Kwa majaribio nipo ladhi kwenda hata sasa hivi, ntafurah sana kama nikipata hiyo fulsa, Kuliko wamtume panya.
 
Hawajagundua, wameiona. Maana iligunduliwa miaka 5300 iliopita pale misri na Mesopotamia. Ilikuwa inaitwa nibiru.

Kwa waerevu tunasema. U CANT SEE THE REALITY UNTIL OTHERWISE U HAVE ACCESSED THE MOTHER KNOWLEDGE.
Mkuu hii nibiru si ndio tuliambiwa iko njiani kugongana na dunia yetu?
 
Wahame bac watuachie dunia yetu....waongo sana hawa!..Au wameona hatuwezi kufika huko....
 
Mkuu hii nibiru si ndio tuliambiwa iko njiani kugongana na dunia yetu?
Habari ya kugongana hapana. Isipokuwa huwa inaleta deflection kutokana na ukubwa wa gravity kwa zile sayar zinazokaribiana wakati inapospin kwenye mzunguko wake.

Hakuna Mzungu anaegundua kitu. Vyote wanavyojaribu kuvieleza wameaccess maarifa mama ambayo yapo na wanatufich wakati sie ndie wenye urithi.

Kumbuka DNA IS STORE HOUSE OF KNOWLEDGE
 
Hapo Ndipo dini inapodhihirisha udikteta wake uchwara!! Sasa nyie wenye huo urithi wa uelewa kutoka Mungu mumeutumiaje huo urithi kwa maendeleo yenu? Mbona asilimia. Kubwa ya nyie wenye utajiri mkubwa wa imani ndiyo maskini wakubwa wa kila kitu hadi fikra!! Au wewe uliamini ilipoandikwa Mtafuteni yeye TU!! Halafu mengine Yote mtapewa na Kuzidishiwa!! Nadhani hata wazazi wako hawaku practice hiyo dhana zubaishi! Maana Ungekufa kabla hata hujazaliwa!! Fanya kazi! Itafute Elimu!Ishi! Sijakuambia Usiamini MUNGU! Ila Changanya na zako.
 
Anayetaka kufikirisha akili zaidi akasome kitabu kinaitwa Thiaoouba Prophecy.
 
Kama chombo kitafikia asilmia 20 ya spidi ya mwanga ina maana miaka mitano kitakuwa kimesafiri mwaka mmoja wa mwanga. Hapo nimeona kama kuna miaka minne kwa hiyo mara tano ina maana miaka 20 au ni miongo miwili sina uhakina kama hesabu zangu zipo sahihi

maana hata tunachokiona kwenye hiyo sayari kwa kutumia darubini tayari kimeshapita miaka minne !!! kama huko kuna viumbe wangekuwa wanatuangalia kwa sasa wao wangeona hapa Tanzania Jk akiwa Rais na mambo mengine ya miaka minne iliyopita.
 
Point of correction hii sio sio complete exo-planet Bali ni candidate bado haijawa official
 
Tuna safari ndefu kwani hata nyota tunazoziona kwa sasa si ajabu haziko tena , ila mwanga wake unaonekana kwa sababu ni mbali sana na inachukua maelfu ya miaka mpaka kutufikia.
Great..... Uko nje ya box
 
sasa naamza kuamini kuwa maisha hayataisha ila mwisho ni pale mtu anapokufa.Mungu katupatia tujivinjari tuwezavyo yeye hata rudi tena ila ukifa ndio mwisho wa maisha yako yaani hakuna paradiso wala Jehanum utapotea tu kama upepo.
 
Hapo Ndipo dini inapodhihirisha udikteta wake uchwara!! Sasa nyie wenye huo urithi wa uelewa kutoka Mungu mumeutumiaje huo urithi kwa maendeleo yenu? Mbona asilimia. Kubwa ya nyie wenye utajiri mkubwa wa imani ndiyo maskini wakubwa wa kila kitu hadi fikra!! Au wewe uliamini ilipoandikwa Mtafuteni yeye TU!! Halafu mengine Yote mtapewa na Kuzidishiwa!! Nadhani hata wazazi wako hawaku practice hiyo dhana zubaishi! Maana Ungekufa kabla hata hujazaliwa!! Fanya kazi! Itafute Elimu!Ishi! Sijakuambia Usiamini MUNGU! Ila Changanya na zako.
Wewe ndio kilaza kweli. Hata hufahamu huu ni wakati gani na kwanin watu weusi wameanza kujitambua wao ni akina nani ktk ulimwengu huu. Hawajajifunza mashuleni kwa maana huku ndiko wapumbavu kama wewe mnadhani ndio sehemu ya kupata maarifa hali kwamba mifumo ya elimu uchwara na dini zenu uchwara ndizo zinazoendelea kuwapumbaza wenye urithi ili waovu waendelee kuishi na kuendelea kuwahadaa kwamba tumegundua so and so. WAPUMBAVU WAKUBWA.

KUAMSHWA KWA DNA ZETU NI PIGO KWAO NA WALE WANAWAABUDU KIUPUMBAVU KAMA WEWE. THIS IS THE END OF ACQUARIAN PERIOD AND THE COMING OF THE NEW ERA. THE ERA OF FINAL CALL FOR THE CHOSEN ONE.

UR MASTERS KNOW EAXCTLY THAT, THEIR TIME IS UP BECAUSE NO MORE LIES NO MORE MASQURADING. TRUTH IS PREVAILING. HIVYO KWA SISI WEREFU TUNAJUA WANAKOENDA NA WAVYOFIKIRIA KUWAYUMBISHENI. LAKINI HAWATAWEZA MAANA MUDA WAO WA KUWAHADAA WATEULE UMEKWISHA.

SISI TULIOAMSHWA NA TULUOACCESS MOTHER KNOWLEDGE Kazi yetu kuwaeleza na kuwafundisha ama kuwakumbusha ndugu wa jamaa zetu kuhusu ukweli.

HAKUNA JIPYA CHINI YA JUA. WAMESHINDWA KUJENGA MAPIRAMIDI YALIYOPO HAPA DUNIANI WANAKIMBILIA MAARIFA YA MBINGU. KICHEKESHO SANA. WATU WANGU WANAHARIBIWA KWA KUKOSA MAARIFA.
 
Back
Top Bottom