Sayari inayofanana na Dunia yagunduliwa

Sayari inayofanana na Dunia yagunduliwa

Ndio watu wajue kuwa uwepo waakili wamwanadamu bado nindogo sana Mungu ni Mungu akili zake azichunguziki Mwanadamu asijivune kwachochote kufika apo kwenye sayari aiwezekani mwadamu kufika tumpe Mungu maisha yetu ajeatufilishe mbinguni
 
Kuifikia sayari hiyo lazima kijengwe chombo kitakachokuwa na uwezo wa kusafiri kwa miaka yote hiyo na kiwe na jamii itakayoendelea kuzaliana mpaka kuifikia sayari hiyo
 
Siku si nyingi tutagundua makazi ya Sir. God. Time Will Tell.
Wameshagundua hukuiona ile thread inaonyesha jinsi mbingu ilivyo na kuna ile inasema wanasayansi wa kirusi wameiona jehanamu
 
Tuna safari ndefu kwani hata nyota tunazoziona kwa sasa si ajabu haziko tena , ila mwanga wake unaonekana kwa sababu ni mbali sana na inachukua maelfu ya miaka mpaka kutufikia.
 
Kuifikia sayari hiyo lazima kijengwe chombo kitakachokuwa na uwezo wa kusafiri kwa miaka yote hiyo na kiwe na jamii itakayoendelea kuzaliana mpaka kuifikia sayari hiyo
Hicho chombo kitakuwa sayari inayofuata sayari...!!
 
Tuna safari ndefu kwani hata nyota tunazoziona kwa sasa si ajabu haziko tena , ila mwanga wake unaonekana kwa sababu ni mbali sana na inachukua maelfu ya miaka mpaka kutufikia.
Ukiwa kwenye space sayari yetu nayo inan'gaa kama nyota zingine.
 
Kwani W anataka kutuhamisha humu au Wanataka kuhama wap? Maana kila Siku Wanataka pakuhamia
 
Ni kweli na ina rangi ya blue, ila kuhusu light years ni kwamba A light-year ni ( kwa kifupi ly) kipimo cha urefu kinachoelezea umbali katika anga za mbali. Nayo ni kilometa trillioni tisa au ( maili trillioni sita ). kama inavofafanuliwa na Umoja wa kimataifa wa anga za mbali ( International Astronomical Union) (IAU), umbali ambao mwanga unasafiri kwa mwaka mmoja yaani siku 365.25 .
 
For in him all things were created: things in heaven and on earth, visible and invisible, whether thrones or powers or rulers or authorities; all things have been created (Colossians 1:16)
 
View attachment 387393
Wanasayansi wamegundua sayari ambayo inakaribia sana Dunia kwa mazingira na ukubwa wake na ambayo inazunguka nyota ijulikanayo kama Proxima Centauri, iliyo na mfumo unaokaribia zaidi mfumo wetu wa jua.

Sayari hiyo, ambayo kwa sasa imepewa jina 'Proxima b' inazunguka nyota hiyo katika eneo ambalo kuna uwezekano mkubwa sana wa kupatikana kwa maji.

Proxima inapatikana umbali wa kilomita trilioni 40 na inaweza kumchukua mtu, akitumia teknolojia ya sasa ya vyombo vya usafiri wa anga za juu, maelfu ya miaka kufika huko.

View attachment 387394

Licha ya kwamba ni mbali sana, kugunduliwa kwa sayari hiyo huenda kukasisimua hisia na mawazo ya binadamu na wanasayansi kuhusu kuwepo kwa viumbe katika sayari nyingine au uwezekano wa wakati mmoja watu kuishi kwenye sayari nyingine.

"Kusema kweli, kufika huko kwa sasa hiyo ni kama hadithi ya kubuni kisayansi, lakini watu sasa wanalifikiria hilo na si jambo lisiloweza kufikirika kwamba wakati mmoja huenda watu wakatuma chombo huko," Guillem Anglada-Escudé, ambaye kundi lake la Pale Red Dot limechapisha matokeo ya ugunduzi wa sayari hiyo katika jarida la Nature amesema.

Mapema mwaka huu, bilionea Yuri Milner alisema atawekeza $100m katika utafiti wa kuunda chombo au kifaa kidogo kinachoweza kusafiri anga za juu kwa kutumia teknolojia ya laser.

Chombo kama hicho kinaweza kusafiri kwa pengine asilimia 20 ya kasi ya mwanga na hivyo kufupisha safari ya kufika kwenye nyota kama vile Proxima Centauri kutoka maelfu ya miaka hadi miongo kadha.

Ugunduzi wa sayari hiyo ulifanikishwa kupitia darubini ya kisasa yenye kifaa kujulikanacho kama HARPS.

Darubini hiyo imewekwa nchini Chile.

Takwimu kutoka kwa darubini hiyo zinaonyesha uzito wa Proxima b huenda ukawa mara 1.3 zaidi ya uzito wa dunia na kwamba inazunguka nyota ya Proxima katika umbali wa kilomita milioni 7.5. Huchukua siku 11.2 kumaliza mzunguko mmoja.

Umbali kutoka kwa nyota hiyo na sayari hiyo ni mfupi ukilinganisha na umbali kutoka kwa Dunia hadi kwa Jua (kilomita 149 milioni). Lakini Proxima Centauri ni 'nyota nyekundu mbilikimo'. Si kubwa sana na nguvu zake si nyingi kama za Jua hivyo safari inaweza kuwa karibu na nyota hiyo lakini iwe na mazingira sawa na ya dunia.

Chanzo: BBC


Kuna kitu sijakielewa barabara.Hivi kwa nini ile Darubini iwepo kule Chile? Inamilikiwa na nchi ya Chile au ni kwa sababu ya Kijiografia?
 
Wataalam wanase ubongo wabinadam mbaka sasa unaasilimia arobaini yakufanya kazi ikifika mia ndo mwisho wadunia maana tutamuona mungu nasema sisi Tanzania bado manyani at a katiba yetu tunaivunja wenyewe send
 
Kuifikia sayari hiyo lazima kijengwe chombo kitakachokuwa na uwezo wa kusafiri kwa miaka yote hiyo na kiwe na jamii itakayoendelea kuzaliana mpaka kuifikia sayari hiyo
Kama chombo kitafikia asilmia 20 ya spidi ya mwanga ina maana miaka mitano kitakuwa kimesafiri mwaka mmoja wa mwanga. Hapo nimeona kama kuna miaka minne kwa hiyo mara tano ina maana miaka 20 au ni miongo miwili sina uhakina kama hesabu zangu zipo sahihi
 
Wataalam wanase ubongo wabinadam mbaka sasa unaasilimia arobaini yakufanya kazi ikifika mia ndo mwisho wadunia maana tutamuona mungu nasema sisi Tanzania bado manyani at a katiba yetu tunaivunja wenyewe send

Jamii yeyote ambayo bado fikra zake ziko katika stage ya kusaka chakula unategemea ifanye nini cha ziada?Kama wewe ni Mkiristu naomba nikukumbushe kile kisa cha wale watu waliolishwa na Yesu kwa mikate na samaki hata kingine chakula wakamwaga na kupiga mateke.Wale jamaa walipoamka tena kesho yake mawazo yao ilikuwa ni kwenda tena kwa Yesu kupiga msosi. Hawakuwa na wazo la kwenda kujifunza falsafa ya maisha zaidi ya chakula.Hawakujua Yesu alikuwa na kitu ambacho kwake ndo vitu vingine kama chakula vilikuwa vinawezekana.

Nchi yetu na Afrika kwa ujumla tumepata uhuru toka kwa wakoloni(sawa na tulilishwa chakula na Yesu) lakini hata sasa akili zetu zinawaza kutawala wenzetu ili tupate kula tu.Hakuna kitu tunafikiria nje ya madaraka ya kula.CCM na watu wake wanafikiria kuonyesha jinsi askari wake wanavyoweza kupandana juu ili kumkabili mwana UKUTA.Wenzetu wanaonyesha ambako darubini zao zinakoona mbali.Sisi macho yetu yanaona wana UKUTA kwenye mikutano ya ndani.
 
Kama chombo kitafikia asilmia 20 ya spidi ya mwanga ina maana miaka mitano kitakuwa kimesafiri mwaka mmoja wa mwanga. Hapo nimeona kama kuna miaka minne kwa hiyo mara tano ina maana miaka 20 au ni miongo miwili sina uhakina kama hesabu zangu zipo sahihi


Leo tunafikiria tu Mwanga kama ndio kitu kinachosafiri kwa kasi kuliko vitu vingine.Hatuwezi kujua vizazi vijavyo vitakuwa na uelewa gani.
 
Back
Top Bottom