Hapo unafanya marudio tu! Maswali kama hayo yalishaulizwa na wanafalsafa wengi tu miaka nenda rudi! Nikuulize swali: Je, mtu akishindwa kujibu maswali yako ndiyo kusema Mungu hayupo na akijibu ndiyo kusema anakuwepo? I.e. Is knoweldge of a person about God what dtermines what God is and can do?
Indeed haya yote hakuna jipya na ukisoma classical arguments za theology kina Anselm na Augustine wame struggle kujibu haya unsatisfactory, ndiyo maana yapo mpaka leo.
Swala si kwamba swali ni jipya au la zamani, kuna mi Poincare's Conjecture watu wame struggle nayo kwa miaka mia, lakini hawakuacha kutafuta majibu kwa sababu maswali ni ya zamani.Kwa sababu hawakupata majibu, wakaendelea kutafuta mpaka hapa juzi tu in the 2000s.
Kwa hiyo maswali kuwa mapya au ya zamani si hoja, hoja ni, je yamejibiwa kikamilifu?
Kushindwa kujibu maswali rahisi tu ya kibinadamu kunaonyesha zaidi kwamba hii idea nzima ya mungu haiyumkiniki. Kama binadamu wenye akili zenye kifani wanaweza kukwaza idea nzima ya mungu asiye kifani kwa maswali madogo tu ya upeo wa kibinadamu, then swala zima la mungu mwenye uwezo wote na upendo wote linakosa msingi mzuri wa kuaminika.
Kutoweza kujibu hakuonyeshi kwamba mungu hayupo, lakini hakusaidii lolote kuonyesha watu zaidi kwamba mungu yupo. Kwa kweli kunaongeza shaka kama mungu yupo na kuongeza kusadikika kwa wazo la kwamba mungu hayupo.
Mimi naangalia hili swala la kuwapo kwa mungu kama kuangalia hesabu ya square root ya namba. Ingawa naweza kuwa sijui jibu kamili la square root ya 8, lakini kwa sababu najua square root ya 9 (3) na square root ya 4 (2) basi ukiniambia square root ya 8 ni kubwa kuliko 3 au ni ndogo kuliko 2 sitakubali, hata bila ya kuijua square root kamili ya 8, kwa sababu najua square root ya 8 iko kati ya 2 na tatu kama vile 8 ilivyo kati ya 4 na 9.
Kwa hiyo kuna maswali mengine unaweza kuona kwamba ingawa huna jibu kamili, lakini jibu hili nililopewa lina converge kwenda kwenye jibu kamili, au lina diverge kutoka kwenye jibu kamili.
Na hii habari ya watu kushindwa kutoa majibu kamili kwa haya maswali inaonyesha kwamba ukweli una diverge kutoka kwa jibu la kuwepo kwa mungu mwenye uwezo wote na upendo wote, bila hata mtu kuwa na uwezo wa kiungu kujua hilo.