Kwamba hayo majengo yalikua imara kuliko mengine?!
Unajua haya mambo ya dini ni imani tu, ni sawa na wale wanaoamini ng'ombe, jua na maji kuwa ni miungu. Hindu karibu kila kitu kilicho muhimu maishani mwao ni mungu, sasa kwa waislamu na wakristu mmtataka kuwabishia na kung'ang'ania kuwa mungu ni mmoja na nini na nini!
Hata wale wenye siasa kali wa kiislamu kuamini kuwa kuua watu kutawapelekea sijui mbinguni na na nini hizo zoteni porojo, au wale wakristu kuamini dini zingine zote ni fake na ya kwao tu ndio yenyewe, yote ni hadithi tu za abunuwasi.
Uzuri wa dini kama mfuatiliaji sio "fanatic", basi humfanya kuwa na ustaarabu wa kujieshimu na kueshimu wengineo, kero ni pale wanapotaka kila mtu awe ka wawo!
Imani haina sayansi, huwezi kuipima wala kui prove, zadi ya kukubali hayo maandiko yalioletwa na waarabu na wakristu.
Sayansi ina majibu yake, na kama hamna basi binadamu anaendelea kutafuta, huwezi kuendelea ku force watu wawe wanasali sala tano kwa siku na kufunga, au watu kusoma agano jipya na kwenda kanisani mara kwa mara, haya ya kulazimishana yaliletwa na hao wenye dini wenyewe, sie ni wafuataji, sio dini yetu hiyo, tumeiga tu.
Uzuri wa sayansi ni kwa wewe mwenyewe kujiuliza, kama isingekuwepo je, tungeweza kusafiri na ndege? kwa magari? kutibu wetu? Kuacha kutegemea nguo za pamba? Kuacha kutegemea umeme wa maji? Au kutegemea maji ya kunywa ya kutoka vyanzo vichache?
Sasa hio ndio sayansi, inatutatulia matatizo yetu ya kila siku, dini kwa upande wangu naona imesaidia watu kufuata sheria za nchi, nchi ikiwa na sheria za nchi sio lazima iwe na dini, dini ilikuwepo ili watu at least wawe na sheria. Na ndio maana kila siku serikali inadai, nchi inafuata katiba, sio kuran au biblia la agani la kale au jipya.
Sasa wajuzi wa madini ya watu watakuja na verses na nini, lakini ukweli ndio huo