Wote mnaongea hapa haijui SAUT zaidi mmfika na kuona chuo nakuondoka SAUT ya leo hii 2016 si SAUT ya miaka mitano nyuma ukisema leo saut miundo mbinu yake mibaya leo hii kwa mtu aliyesoma soma hapo zamani kidogo hawezi kukuelewa atakuona wewe ni mnafiki
Ukisema SAUT leo wana garama za ajabu ajabu atakuona wewe ni mnafiki
Kwanini nasema hivi matatizo ambayo unayasema na ambayo wadau wameongezea hapo yalikuwepo miaka mitano iliyopita na si leo
SAUT ya leo miundombinu mbinu mizuri vyoo vipo vingi, maeneo ya kujisomea nje ya mktaba yapo mengi, lecture room zipo za kutosha tena mmefungiwa na viti vya kisasa zamani wenzenu tulisomea kwenye viti vya mbao vya kuhamisha, lecture room chache,
SAUT leo huduma za kibenki zipo mlangoni unalipa ada mlango huu unachukua risiti mlango huu, saut leo si mpaka upande gari uende utawala leo hapo hapo unatoka darasani unaenda utawala
SAUT leo wanafunzi mnalazimishwa kukaa hostel za chuo jamani zamani kupata hostel ya chuo mtu ana honga maana zilikuwa chache alafu mtaani uko hostel hazishikiki bei kuanzia laki 6 mpaka milioni moja na mwenye nyumba anataka cash siyo nusu nusu
Suala la chuo kufunguliwa mapema kwa saut ni kawaida si jambo geni
Kuna kitu mdau kaongelea kuhusu Sijui garama za kila mwaka kujiandikishia hilo suala Siku hizi alipo hizo garama zipo kwenye ada walishaga ziondoa
Kitu kingine mwanafunzi anaendelea na masomo hawezi kuambiwa arudi nyumbani kisa hana ads au boom bado yeye aingie vipindi kama kawaida Siku akipata pesa akajisajili
Mwanafunzi aliyepewa admission saut na hana pesa aende kuongea na uongozi
''WE BUILD THE CITY OF GOD'''