SAUT main campus, mambo haya yanakera acheni!

Man Mvua

JF-Expert Member
Apr 12, 2016
2,184
3,517
Wasalaam.

Hiki chuo ni miongoni mwa vyuo vyenye miundombinu mibovu haswa yaani nakifananisha na Pugu secondary shule niliyosoma A'level.

Najua wengi mtakasirika sana lakini ndo UKWELI, pia haya sio yalionifanya nianzishe hii thread.Yalionifanya nianzishe hii thread ni haya:

1. Hili la kwanza limeshazungumzwa na Rais nalo ni kuwahi kufungua chuo halafu kugoma kupokea wanafunzi bila kulipa ada. Hili jambo linatesa sana vijana hasa wale wa kaya maskini. Sitalizungumzia sana kwa kuwa kwa sasa lipo known kwa kila mtu. Mdogo wa rafiki yangu amefukuzwa chuo mpaka alipe nusu ya ada na yeye anategemea boom hana baba na ***** kajitahidi sana kumsomesha secondary na alipokuwa anaenda chuo alipewa laki mbili tuu, baada ya kuomba akaambiwa alipe laki nne kwanza so ikabidi nimkopee likiingia boom anirudishie. Naomba uongozi wa vyuo vyote nchini na wahusika wakuu mlifanyie kazi agizo la mh.Rais

2. Lakini ujinga level ya degree na sijui wameutoa wapi hawa jamaa wa SAUT main campus Mwanza la kulazimisha wanafunzi kukaa kwenye hostel zao. Kulisikia hili nilikasirika sana na chuo chenyewe kilivyo kibaya, utamlazimishaje mtu kukaa kwenye hostel zenu?

>Je ndo kusema mnawapenda sana au mnafanya biashara kwa lazima?

>Au mnalazimisha kwa kuwa hostel zenu mbovu mnahisi mtakosa watu ?

Embu acheni ujinga bana kama mnataka watu boresheni hostel zenu hizo ambazo zipo kama za secondary yenu ya Pugu.

Rais yupo sahihi hivi vyuo vingine bora vifutwe tuu.
 
Mkuu kweli unataka chuo cha mtakatifu Augustine kifutwe kisa tu umeorothesha hizo kero zako? Well nimewahi kufika Saut na nikweli chuo hakina miundombinu bora kulinganisha na vyuo mashuhuri Afrika mashariki lakini Saut wao wanayo library bora kabisa, kila aina ya kitabu unapata pale kujisomea kwaajili ya maendeleo yako kama mwanafunzi.

Kuhusu hostel kulazimisha wanafunzi hapo wanakosea haina mantiki kumlazimisha mwanafunzi. Lakini unapaswa kabla ya kujiunga ufahamu Saut wanasheria kali na hawafanyi negotiations kwanamna yoyote na wanafunzi. Mfumo wao wa utawala ni viongozi wa juu wanaamrisha chini lazima mfuate.
 
Pale Saut shida ni miundo mbinu tuu hakuna ubaya kabisa kuhusu vitu vingine mf. Library iko poa sana, barabara lami baadhi ya maeneo hakuna, zahanati ipo, majengo ya administration yapo yakisasa, lecture rooms zipo zakutosha, ila vitu vya kurekebishs SAUT ni vyoo, hostel ziboreshwe, cafeteria ziboreshwe, kule Darful hostel kuboresha pia hapo patakuwa pazullz
 
Uliwahi kufika vyuo vingine ukaona changamoto? Nenda UD au SUA ambako hawalazimishi hostel halafu njoo utupe mrejesho.
 
Tatizo lingine naliona hapa SAUT wanafunzi wasiokuwa na kipato unapoanza kujiunga ni vigumu kwani wana kitu kinaitwa Administrative costs kilichoanza 2006 na bado unatakiwa ulipe nusu ya tuition fees,sasa kwa wanafunzi walio wengi ambao wanatoka familia maskini hupatwa na tatizo kama hilo la ndugu yake na mleta uzi. Ingekuwa vema SAUT ibadilishe huo utaratibu wa kudai pesa kabla kwa kuwabana wanafunzi hata wasio kuwa na uwezo wakati wanasubiri mkopo kwani mkopo ukipata wangeweza lipa.
 
Wote mnaongea hapa haijui SAUT zaidi mmfika na kuona chuo nakuondoka SAUT ya leo hii 2016 si SAUT ya miaka mitano nyuma ukisema leo saut miundo mbinu yake mibaya leo hii kwa mtu aliyesoma soma hapo zamani kidogo hawezi kukuelewa atakuona wewe ni mnafiki

Ukisema SAUT leo wana garama za ajabu ajabu atakuona wewe ni mnafiki

Kwanini nasema hivi matatizo ambayo unayasema na ambayo wadau wameongezea hapo yalikuwepo miaka mitano iliyopita na si leo

SAUT ya leo miundombinu mbinu mizuri vyoo vipo vingi, maeneo ya kujisomea nje ya mktaba yapo mengi, lecture room zipo za kutosha tena mmefungiwa na viti vya kisasa zamani wenzenu tulisomea kwenye viti vya mbao vya kuhamisha, lecture room chache,

SAUT leo huduma za kibenki zipo mlangoni unalipa ada mlango huu unachukua risiti mlango huu, saut leo si mpaka upande gari uende utawala leo hapo hapo unatoka darasani unaenda utawala

SAUT leo wanafunzi mnalazimishwa kukaa hostel za chuo jamani zamani kupata hostel ya chuo mtu ana honga maana zilikuwa chache alafu mtaani uko hostel hazishikiki bei kuanzia laki 6 mpaka milioni moja na mwenye nyumba anataka cash siyo nusu nusu

Suala la chuo kufunguliwa mapema kwa saut ni kawaida si jambo geni

Kuna kitu mdau kaongelea kuhusu Sijui garama za kila mwaka kujiandikishia hilo suala Siku hizi alipo hizo garama zipo kwenye ada walishaga ziondoa

Kitu kingine mwanafunzi anaendelea na masomo hawezi kuambiwa arudi nyumbani kisa hana ads au boom bado yeye aingie vipindi kama kawaida Siku akipata pesa akajisajili

Mwanafunzi aliyepewa admission saut na hana pesa aende kuongea na uongozi

''WE BUILD THE CITY OF GOD'''
 
Hii dunia bhana,UDSM kupata room ni dream ya kila mwanafunzi,UDOM naona kila mwanafunzi ni lazima apate room, SAUT wadau wanalazimishwa kukaa hostel na ninasikia kuna chuo hawana hata room moja kwa ajili ya mwanafunzi
Kama nit mabibo
 
Haha wataka ukae hostel Za nje ya chuo wakati umeenda SAUT na laki 2. Mkisikia chuo cha kanisa mwajua elimu bure. Nenda UD na hiyo mahela.
 
Mleta Uzi umeonyesha hadharani ulivyo mtupu kichwani na usivyofahamu gharama za kuendesha elimu ya juu. Hivyo una akili kutuletea mfano wa mwanafunzi kwenda Chuo na ada ya laki mbili halafu utarajie adahiliwe! Hiyo ni chekechea au Chuo kikuu? Tafadhali jiongeze kabla ya kuandika uzi.
 
Udom yenyewe ni chuo cha serikali lazima ulipe hvo vitu ulivosema ndio wakupokee sembuse chuo binafsi?!!hapo usiwalaumu chuo walaumu bodi wanaochelewesha pesa, kesi za hvo ni nyingi sana wenyewe wanategemea hzo pesa kujiendesha..mwambie achangishe kwa ndugu na majirani atapata tu ya kuanzia
 
Saut pako poa. Miundo mbinu iko normal tu, wala si mibovu uki compare na uhalisia, yaani the way chuo kinavyokua. Kielimu wanajitahidi sana, na ndio maana wengine nikiwemo mimi, nimefanikiwa sana kupitia hapo, within 2yrs i have acquired CPA na niko kwenye parastatal kubwa tu. Ila suala la pesa during registration hawana mzaha na hawashauriki, kabisa. Lazima ujipange hata mimi ilinikuta. Kipindi hicho. Pole sana but kumbuka ni mission hiyo
 
Ni chuo gani ambacho unaweza fanya usajili bila kulipa ada? Hizo ada ndio wanapata pesa ya uendeshaji ikiwemo kulipa mishahara wahadhiri na supporting staff. Bila kuwabana walipe gharama, hicho chuo kitajiendeshaje!!
 
...mdogo wangu wangu anahaha kupata hosteli UD COET, tunahangaika Sa hv kumtafutia chumba off campus, Halafu mtu anakuja kuongea upupu humu

Uliwahi kufika vyuo vingine ukaona changamoto? Nenda UD au SUA ambako hawalazimishi hostel halafu njoo utupe mrejesho.
 
....hata chekechea laki 2 wanazingua, huyu hajui nini maana ya Elimu, Halafu SAUT Ni Chuo cheap Sana, Ada Yao ilikuwa 950k
Mleta Uzi umeonyesha hadharani ulivyo mtupu kichwani na usivyofahamu gharama za kuendesha elimu ya juu. Hivyo una akili kutuletea mfano wa mwanafunzi kwenda Chuo na ada ya laki mbili halafu utarajie adahiliwe! Hiyo ni chekechea au Chuo kikuu? Tafadhali jiongeze kabla ya kuandika uzi.
 
Tatizo lingine naliona hapa SAUT wanafunzi wasiokuwa na kipato unapoanza kujiunga ni vigumu kwani wana kitu kinaitwa Administrative costs kilichoanza 2006 na bado unatakiwa ulipe nusu ya tuition fees,sasa kwa wanafunzi walio wengi ambao wanatoka familia maskini hupatwa na tatizo kama hilo la ndugu yake na mleta uzi. Ingekuwa vema SAUT ibadilishe huo utaratibu wa kudai pesa kabla kwa kuwabana wanafunzi hata wasio kuwa na uwezo wakati wanasubiri mkopo kwani mkopo ukipata wangeweza lipa.
SAUT wanaconsider administrative fees Tu during registration, Na SAUT ndo Chu kilicho cheap ukicompare Na vyuo vingine Na vya serikali, sasa sijui tatizo lipo wapi
 
Wote mnaongea hapa haijui SAUT zaidi mmfika na kuona chuo nakuondoka SAUT ya leo hii 2016 si SAUT ya miaka mitano nyuma ukisema leo saut miundo mbinu yake mibaya leo hii kwa mtu aliyesoma soma hapo zamani kidogo hawezi kukuelewa atakuona wewe ni mnafiki

Ukisema SAUT leo wana garama za ajabu ajabu atakuona wewe ni mnafiki

Kwanini nasema hivi matatizo ambayo unayasema na ambayo wadau wameongezea hapo yalikuwepo miaka mitano iliyopita na si leo

SAUT ya leo miundombinu mbinu mizuri vyoo vipo vingi, maeneo ya kujisomea nje ya mktaba yapo mengi, lecture room zipo za kutosha tena mmefungiwa na viti vya kisasa zamani wenzenu tulisomea kwenye viti vya mbao vya kuhamisha, lecture room chache,

SAUT leo huduma za kibenki zipo mlangoni unalipa ada mlango huu unachukua risiti mlango huu, saut leo si mpaka upande gari uende utawala leo hapo hapo unatoka darasani unaenda utawala

SAUT leo wanafunzi mnalazimishwa kukaa hostel za chuo jamani zamani kupata hostel ya chuo mtu ana honga maana zilikuwa chache alafu mtaani uko hostel hazishikiki bei kuanzia laki 6 mpaka milioni moja na mwenye nyumba anataka cash siyo nusu nusu

Suala la chuo kufunguliwa mapema kwa saut ni kawaida si jambo geni

Kuna kitu mdau kaongelea kuhusu Sijui garama za kila mwaka kujiandikishia hilo suala Siku hizi alipo hizo garama zipo kwenye ada walishaga ziondoa

Kitu kingine mwanafunzi anaendelea na masomo hawezi kuambiwa arudi nyumbani kisa hana ads au boom bado yeye aingie vipindi kama kawaida Siku akipata pesa akajisajili

Mwanafunzi aliyepewa admission saut na hana pesa aende kuongea na uongozi

''WE BUILD THE CITY OF GOD'''
Wakala wao wewe
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom