Bifi baina ya Qatar na Saudia ni ya kimaslahi/influence na inaogopa sana ukoo wa kifalme kupinduliwa kwa kupitia mbinu za colour revolution, utawala wa Kifalme hawajiamini hata kidogo - katika mbinu zake za kutaka kujihami linataka ndiyo liwe Taifa linao wika Mashariki ya kati i.e a mimi Super Power - watumie uwezo wao kijeshi kuwatishia Waarabu wenzake na raia wa Saudia ili wasifurukute, vile vile Saudia inatumia vibaya utajiri wake kuendeleza siasa zake Mashariki ya kati zenye lengo la kutaka kuvuruga amani kwenye Nchi washindani wao notably IRAN na Syria kwa support ma rebels kwa kuwapatia silaha na fedha. Binafsi siamini kama Trump anahusika katika ku-influence mifarakano ya Saudia na Qatar we sema labda Saudia ilitumia ujio wa Trump nchini mwao kuikandia Qatar kwamba ina support Ugaidi wakati kila mtu mwenye akili timamu anajua Sadia ndiye kinara wa kuvurunga nchi za watu hasa Sysria na Iran.
Narudia kusisitiza kwamba Saudia ina wasi wasi na IRAN, Syria na sasa Qatar, kwa akili zao wanafikiri nchi hizo tatu zinaweza kuwapa mafunzo na ku-finance waasi wa kupidua utawala wa Kifalme, ndiyo maana kwa kupitia ushawishi wake wa kifedha inajaribu sana ku-influence mataifa mengine ya Kiarabu yamtenge Qatar na wao wanakubali bila ya kutafakari undani wa tatizo, mwishowe anaweza kuwashawishi waungane kuishambulia Qatar kijeshi kwa madai kwamba wanafunga ugaidi - Saudia hawataki kuchukua jukumu hilo peke yao baada ya enyeshwa na waasi wa Yemeni, huu sijui mwaka wangapi tangu wavamie Yemen pamoja na Saudia kuwa na silaha nyingi za kisasa bado wameshindwa kutimiza malengo yao huko Yemen, wanajua wakijiingiza Qatar mambo yanaweza kuwa mabaya zaidi ni afadhali wajaribu kuwashurutisha Waarabu wenzao ili washirikiane nao kijeshi/uvamizi just in case.