bukoba boy
JF-Expert Member
- Jan 15, 2015
- 5,370
- 3,956
Saturn V (five) ni roketi iliyojengwa na NASA kwa ajili ya kupeleka watu mwezini.Hii roketi ilikua na nguvu za sana na ya pekee iliyoweza kurushwa kwa mafanikio.Saturn V ilotumika na progamu ya Apollo kwa miaka ya 60 na 70.
Ilikua na urefu wa meter 111 sawa na urefu wa jengo la ghorofa 36.Ikiwa imejazwa mafuta kwa kurushwa ilikua na uzito wa tani 280, uzito wa kama Tembo 40.Ilikua na uwezo wa kubeba mzigo wa tani 130 mpaka "orbit" ya dunia(eneo ambalo dunia hupita wakati wa kuzunguka jua) na tani 50 mpaka mwezini.
Saturn V ilikua na hatua 3 za ufanyaji kazi wake,kila hatua itawasha injini zake mpaka mafuta yaishe halafu itajitoe kutoka roketi,injini za hatua inayofuata zinawaka na roketi kuendelea na safari.
Hatua ya kwanza ndio ilikua na nguvu kuliko zote sababu ilikua na kazi nzito ya kuinyanyua roketi nzima kutoka ardhini.hatua hii iliruka mpaka urefu wa kwenda juu (altitude)wa 68km.Hatua mbili za kwanza zinaangukia baharini baada ya kujitenga hatua ya tatu inabaki angani au kuachwa mwezini.