Mpango wa kupeleka watu wakaishi Mars

Mpango wa kupeleka watu wakaishi Mars

lwambof07

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2016
Posts
4,643
Reaction score
5,348
Mjasiriamali Elon Musk ametangaza mpango wake wa kuunda makao ya binadamu katika sayari ya Mirihi (Mars kwa Kiingereza),ingawa wanaotaka kunufaika watahitajika kulipa pesa nyingi.

Tiketi ya kusafiri hadi kwenye sayari hiyo inakadiriwa kugharimu takriban $200,000.

Bw Musk, aliyeanzisha kampuni ya kibinafsi ya usafiri wa anga za juu kwa jina SpaceX, alitangaza mpango huo katika kongamano la kimataifa la wataalamu wa anga za juu (IAC) mjini Guadalajara, Mexico, Jumanne.

Mpango wake, unajumuisha mfumo wa usafiri ambao utaweza kusafirisha watu 100 hadi Mars, safari yote ikichukua siku 80.

Baadaye, safari hiyo inatarajiwa kuchukua siku 30 pekee.

Bw Musk amesema ili kufanikiwa na kuhakikisha gharama kwa kila mtu ni $200,000, basi lazima kuwe na njia ya kutumia tena mitambo ya uchukuzi itakayotumiwa.

Amezungumzia mpango wa kuunda koloni ya watu milioni moja hivi ambao wataweza kujitosheleza na kusema mpango huo utachukua miaka 10 hivi kutimizwa.

Ili kufikisha watu milioni moja, Bw Musk amsema: "Ninataka watu watazame kwamba ni jambo linalowezekana, jambo tunaloweza kutimiza katika uhai wetu ... na kwamba yeyote anaweza kwenda huko akitaka."

Chini ya mpango wa SpaceX, safari ya kwanza ya kupeleka watu sayari hiyo itafanyika 2022.

Chombo cha kwanza kupeleka watu Mars Bw Musk anataka kukiita The Heart of Gold, jina linalotokana na chombo kinachozungumziwa katika kitabu cha Douglas Adams The Hitchhiker's Guide to the Galaxy.

Kitarushwa kutoka Kituo cha Anga za Juu cha Nasa cha Keneddy, sehemu 39, ambayo ndiyo sehemu iliyotumiwa kurusha roketi na vyombo vya anga za juu chini ya mpango wa Apollo.

Chombo cha kwanza cha kusafirisha watu kitafanyiwa majaribio katika kipindi cha miaka minne ijayo.

Mwishoni mwa wiki, Bw Musk alitangaza kwamba majaribio ya kwanza ya roketi kwa jina Raptor ambayo itatumiwa kurusha chombo hicho pamoja na kifaa cha kuiweka kwenye mzunguko anga za juu (booster) yalifanyika.

Tangi la mafuta ya kifaa hicho limeundwa na kufanyiwa ajaribio na Bw Musk alionesha picha ya tangi hilo na wafanyakazi.

Mfumo wa kifaa hicho cha kuweka chombo cha anga za juu kwenye mzunguko wa sayari, pamoja na chombo chenyewe, kwa pamoja unafamika kama Mfumo wa Usafiri wa Sayari hadi Nyingine (ITC). Mitambo hiyo miwili kwa pamoja ina urefu wa mita 122, na inazidi mfumo wa Saturn V wa Apollo ambao ulitumiwa kwenda mwezini.

ITS kubwa zitaweza kubeba hadi abiria 200.
Mjasiriamali huyo anapanga kwamba wakati wa safari hiyo ya siku 80, watu wataishi kwa pamoja na kutazama filamu, kuhudhuria mihadhara na kucheza michezo isiyoathiriwa wa mvutano wa sayari.

Mpango wote utafadhiliwa na faida kutoka kwa SpaceX.

Bw Musk anatazama mpango huo wa kupeleka watu Mars kuwa "ushirikiano mkubwa wa umma na sekta ya kibinafsi" na anasema "hivi ndivyo Marekani ilivyoanzishwa".

Vyombo vya anga za juu vitatumwa kila baada ya miaka miwili Mars inapokuwa imekaribia sana dunia. Umbali kati ya sayari hizo mbili utakuwa kilomita 57.6 milioni mwaka 2018.

Sayari hizo zinapokuwa mbali sana, huwa umbali kati yake ni kilomita 400 milioni.

Miaka ya karibuni, umbali huo umepungua kufikia kilomita 100 milioni pekee.

Bw Musk anasema chini ya mpango wake, kunawezekana kuwa na vyombo 1,000 vikisafiri angani.

Gharama ya kusafiri baadaye inaweza kushuka hadi kati ya $100,000 na $140,000.

Mtu akitaka kurejea duniani, ataweza kufanya hivyo "bila malipo".
IMG_20220115_131121.jpg
IMG_20220115_131107.jpg
IMG_20220115_131054.jpg
IMG_20220115_131042.jpg
IMG_20220115_131028.jpg
IMG_20220115_131012.jpg
 
Brilliant! As long as huku kwetu nchi inaelekea kupigwa mnada, kuna space ya kukimbilia.
 
Mtu akitaka kurejea duniani, ataweza kufanya hivyo "bila malipo".View attachment 2082157View attachment 2082158View attachment 2082159View attachment 2082160View attachment 2082161View attachment 2082162
Kuna nini huko Mars cha ajabu?? Nasikia ata Oxygen hakuna.Si bora niende Moshi nikale mbege na watu wangu tu
 
Hata Kama napenda sayansi ya anga ndio ila kwenda huko never! Kwa jinsi nilivyofatilia hatari zilizopo can't keep my body inside space ships to mars!.

Ni hatua nzuri waliyofikia lakini kwanini waanze na watu wengi badala ya wachache Kwanza..? Heri ingeanza Kwanza crew ya watu hata kumi baadae ndo waje 100. It's too risk aisee heri uniambie kwenda mwezini hapo chap kidogo..
Wengine sie tubakieni hapahapa tuonyeshane ubabe wa kurogana..😂
 
Bora uende Dubai ukapumzike.Kuna hatari nyingi za kiafya kwenda Mars

(1) Mionzi ya hungani inaweza kukuleta saratani , magonjwa ya moyo na akili.

(2) Safari ya kuelekea Mars inaweza kukuletea upofu (Spaceflight-Associated Neuro-ocular Syndrome )

(3) Unaweza kupata msongo wa mawazo (behavioral health and performance decrements)

(4) Kule hakuna chakula
 
Wengine sie tubakieni hapahapa tuonyeshane ubabe wa kurogana..[emoji23]
[emoji1787][emoji1787]acha uoga yan dunia unaiona ile pale
 
Bora uende Dubai ukapumzike.Kuna hatari nyingi za kiafya kwenda Mars

(1) Mionzi ya hungani inaweza kukuleta saratani , magonjwa ya moyo na akili.

(2) Safari ya kuelekea Mars inaweza kukuletea upofu (Spaceflight-Associated Neuro-ocular Syndrome )

(3) Unaweza kupata msongo wa mawazo (behavioral health and performance decrements)

(4) Kule hakuna chakula
Musk mjanja si ndiyo maana anatuma watangulizi kwanza chambo ukimuona yeye kaenda aisee na wewe hapo ndo unaweza kwenda yaan vitu vinatoka huku vinapelekwa kule msoc kila kitu
 
Bora uende Dubai ukapumzike.Kuna hatari nyingi za kiafya kwenda Mars

(1) Mionzi ya hungani inaweza kukuleta saratani , magonjwa ya moyo na akili.

(2) Safari ya kuelekea Mars inaweza kukuletea upofu (Spaceflight-Associated Neuro-ocular Syndrome )

(3) Unaweza kupata msongo wa mawazo (behavioral health and performance decrements)

(4) Kule hakuna chakula
Nayajua yote haya mkuu na kunakugongwa na magimba makubwa na haya ndo kiboko yanawapoteza kabisa Mambo yanakuwa movie sasa..😂
 
yaan mzungu kamuona Mungu fala alivyochagua dunia kwa ajili ya uhai anataka kumkosoa dah
 
[emoji1787][emoji1787]acha uoga yan dunia unaiona ile pale
Dunia yetu inaulinzi mzuri sana heri nijitulize hapa tu mkuu huko sikia tu Kuna midude ishavurugwa spidi inayotembea ikiwafuma mbona hizo dollar mtaona mmejifanyia maziko..😂
Mi kwenye moon natimba tu risk zake si nyingi Kama mars,kule ndio maana mpk sasa hajatimbako mtu coz sio mchezo ni zaidi ya kuwa jangwani.
 
Dunia yetu inaulinzi mzuri sana heri nijitulize hapa tu mkuu huko sikia tu Kuna midude ishavurugwa spidi inayotembea ikiwafuma mbona hizo dollar mtaona mmejifanyia maziko..[emoji23]
Mi kwenye moon natimba tu risk zake si nyingi Kama mars,kule ndio maana mpk sasa hajatimbako mtu coz sio mchezo ni zaidi ya kuwa jangwani.
na wanapambana leo kesho kufanikisha ili kuwaprove wrong watu wengi wanaobeza unajua wajamaa wanawashwa maana almost kila kitu kipo sasa wanatafuta chenye challenge
 
Bora twende TU uko, maana nchi yetu MDA wowote inapigwa mnada[emoji4]
 
Back
Top Bottom