Sasa tumewaletea uwekezaji mpya unaolipa kihalali

"Ponzi scheme" ni utapeli wa kulipa wawekezaji wa zamani kwa mitaji ya wawekezaji wapya.

Miradi yetu hatufanyi hivyo kabisa. Napenda ufahamu kuwa kwa sasa kuna miradi mipya miwili ambayo tunakusanya pesa za kuianziasha, mmoja wapo ni huu wa excavator. Nimekataa kabisa kutumiwa pesa na wote wanaopenda kujiunga na hii miradi mipya mpaka zitimie pesa za kuanzisha miradi kwa ahadi (pledge). Yote ni ku avoid kuchukua pesa za watu kabla ya kuwa na uhakika wa kukamilika mtaji.

Pia tuna miradi ya zamani inayoendelea kwa sasa, tunakukaribisha kuja kujionea. Pesa zinazoingiza hiyo miradi ndizo zinazotumwa kwa wawekezaji wetu.

Hatuna sababu ya kufanya ponzi.
 
Umeshindwa kujibu hizi siku 365 zina affect vipi assumptions zote 4,
By the way rafiki yako (sijui ni wewe mwenyewe) ndio kajichanganya,
Kuna mahali anasema Mwaka Mmoja mmoja wa siku za kazi,
Kuna watu wako kazini siku 365 zote za mwaka, hawana mapumziko wala sikukuu,

Ninaomba nifafanue kwa ufupi kwa mwaka mmoja wa siku za kazi au siku 365 za kazi tunamaanisha nini...

Siku za kazi tunamaanisha ni siku kamili ambazo mwekezaji atalipwa, ni lazima zitimie siku 365. Tunagawa mtaji jumlisha faida gawa kwa 365 (siku za mwaka mmoja wa kazi), jawabu lake ni mapato kamili ya mtaji na faida kwa siku moja ya kazi.

Mfano tukifanya kazi vizuri tunaweza siku ya kulipwa tukakupa pesa za malipo ya wiki mbili mbele ili kumaliza hesabu za malipo ya siku kwa haraka (ndio matarajio yetu). Hapo kuna uwezekano mkubwa pesa za mwekezaji za siku 365 zikalipwa kabla ya mwaka kuisha. Na hapo ndipo utapoishia mkataba wetu wa malipo, hata ikiwa tumezikamilisha pesa za mwaka mzima baada ya miezi sita tu.

Na inaweza kutokea chochote ambacho kipo nje ya matarajio na muono wetu (force majeure) ikawa kuna siku hatujafanya kazi. Basi nazo pia hazitahesabiwa, zitazohesabiwa ki malipo ni siku 365 kamili (kuwahi ndio matarajio yetu ) au tuchelewe kidogo kwa sababu za msingi zinazoeleweka, na zisizo zuilika kama mvua, mafuriko, maandamano, mashine imeharibika na inafanyiwa matengenezo (kumbuka mradi huu ni wa excavator). Litapotokea lolote la namna hiyo lililo nje ya uwezo wetu likapelekea kazi kutokufanyika, haitokula kwako wala kwetu. Ni mpaka itimie siku 365.

Natumai kwa mwaka mmoja wa kazi au siku 365 za kazi nimeeleweka na ninakaribisha maswali ikiwa sijaeleweka.
 
Naona ni wazo zuri na nimejaribu kupiga hesabu kwa jinsi nilivyoelewa nikiwekeza 500,000 nitakua natumiwa 4110 kila siku ya kazi kwa siku 365, Ili iwe imekamilisha 1,500,000. Nimechukua namba za Mr Abdul niwasiliane naye zaidi. Nitafurahi ukinijibu kama nipo sahihi nilivyoelewa. Ahsante
Mi nimeona ni elfu 2000 kwa siku

ikanikatisha tamaa
 
Mradi huo una tofauti gani na miradi mingine iliyoko kwenye soko kama; Umoja,Wekeza,Nicol,Swala mfuko wa ukwasi,Jikimu,Deci na mingine mingi tu?, hapa nalenga zile saccos za akina mama mitaani?.
 
Naona ni wazo zuri na nimejaribu kupiga hesabu kwa jinsi nilivyoelewa nikiwekeza 500,000 nitakua natumiwa 4110 kila siku ya kazi kwa siku 365, Ili iwe imekamilisha 1,500,000. Nimechukua namba za Mr Abdul niwasiliane naye zaidi. Nitafurahi ukinijibu kama nipo sahihi nilivyoelewa. Ahsante

500,000 (mtaji) X 1.5 (150%) = 750,000 (faida)...

500,000 mtaji + 750,000 faida = 1,250,000...

1,250,000 / 365 (siku za kazi) = 3,425 kwa siku...

Utachagua zilipwe kila wiki 3,425 X 7 = 23,975 au kila mwezi 3425 X 30 = 102,750
 
Labda nizirudishe assumptions zote 4 tena hapa chini halafu uniambie kama zote zinahusiana na/au kuathirika na "muda" (siku 365),

Assumptions,
1) Biashara inangiza faida sawa kila mwezi (no peak no lower season)
2) 150% (Tshs 60,000,000) ni faida baada ya mtaji na gharama zingine kutolewa (net profit)
3) 40,000,000 ndio mtaji pekee (Neither excess nor deficit)
4) "Other things kept constant"

Biashara ya excavator kama tunaotafutia mtaji, yapo makubaliano ya aina nyingi. Nitajaribu kufafanua aina mbili tatu...

1) Aina moja ni kuikodisha kwa siku kwenye miradi na kunakuwa na malipo aina mbili kwa muda wote itakao kuwa kwao. Walioikodiaha wanalipa ikifanya kazi au isifanye, mradi ipo kwao wanailipia kima fulani cha pesa mlizokubaliana. Na siku itakayofanya kazi italipiwa kwa kila saa inapofanya kazi.

2) Aina nyingine ni kulipwa kwa siku inapofanya kazi tu lakini zisizidi siku tatu bila kufanya kazi itakapokuwa kwa walioikodi.

3) Aina nyingine ni kama hii yetu tunayoiongelea, excavator itafanya kazi ya kupakia mchanga kwenye magari yanaokuja kununua mchanga kwenye machimbo yetu. Na tutailipa excavator kwa siku, kila gari inalipia kutegemea na ukubwa wa gari.

Kwa uzoefu tulionao tunafahamu kabisa siku moja tutaingiza uwiano wa Shillingi ngapi.
 
Ninaomba nifafanue kwa ufupi kwa mwaka mmoja wa siku za kazi au siku 365 za kazi tunamaanisha nini...

Siku za kazi tunamaanisha ni siku kamili ambazo mwekezaji atalipwa, ni lazima zitimie siku 365. Tunagawa mtaji jumlisha faida gawa kwa 365 (siku za mwaka mmoja wa kazi), jawabu lake ni mapato kamili ya mtaji na faida kwa siku moja ya kazi.

Mfano tukifanya kazi vizuri tunaweza siku ya kulipwa tukakupa pesa za malipo ya wiki mbili mbele ili kumaliza hesabu za malipo ya siku kwa haraka (ndio matarajio yetu). Hapo kuna uwezekano mkubwa pesa za mwekezaji za siku 365 zikalipwa kabla ya mwaka kuisha. Na hapo ndipo utapoishia mkataba wetu wa malipo, hata ikiwa tumezikamilisha pesa za mwaka mzima baada ya miezi sita tu.

Na inaweza kutokea chochote ambacho kipo nje ya matarajio na muono wetu (force majeure) ikawa kuna siku hatujafanya kazi. Basi nazo pia hazitahesabiwa, zitazohesabiwa ki malipo ni siku 365 kamili (kuwahi ndio matarajio yetu ) au tuchelewe kidogo kwa sababu za msingi zinazoeleweka, na zisizo zuilika kama mvua, mafuriko, maandamano, mashine imeharibika na inafanyiwa matengenezo (kumbuka mradi huu ni wa excavator). Litapotokea lolote la namna hiyo lililo nje ya uwezo wetu likapelekea kazi kutokufanyika, haitokula kwako wala kwetu. Ni mpaka itimie siku 365.

Natumai kwa mwaka mmoja wa kazi au siku 365 za kazi nimeeleweka na ninakaribisha maswali ikiwa sijaeleweka.
Umefafanua vema lakini mdau alietoa pesa na ikatokea tatizo/dharula kazi haijafanyika huu mdau atathibitishaje kazi haijafanyika? Je hii haiwezi kuwa backdoor ya kuchelewesha siku za kutimiza mwaka wa siku za kazi? Wakati huo mashine ikiwa imetumika zaidi ndipo inapochoka na kufa au kuharibika mara kwa mara na kuongeza siku za matengenezo ambazo hazi hesabiwi ktk malipo?
 
Mradi huo una tofauti gani na miradi mingine iliyoko kwenye soko kama; Umoja,Wekeza,Nicol,Swala mfuko wa ukwasi,Jikimu,Deci na mingine mingi tu?, hapa nalenga zile saccos za akina mama mitaani?.

Hizo sifahamu zinajiendesha vipi, sitaweza kujifananisha au kujitafautisha nao.

Tunachokifanya sisi tunakielezea hapa kwa uwazi kabisa na unaweza kulinganisha na hao uliowataja kama unaelewa shughuli zao wanafanya vipi.
 
Umefafanua vema lakini mdau alietoa pesa nabikatokea tatizo/dharula kazi haijafanyika huyu mdau atathibitishaje kazi haijafanyika? Je hii haiwezi kuwa backdoor ya kuchelewesha siku za kutimiza mwaka wa siku za kazi? Wakati huo mashine ikiwa imetumika zaidi ndipo inapochoka na kufa au kuharibika mara kwa mara na kuongeza siku za matengenezo ambazo hazi hesabiwi ktk malipo?
Kwa kuangalia hoja hizo hapo juu haiwezi kutokea ujanja ujanja na kusababisha fedha yako na faida kulipwa baada ya mwaka na nusu au miaka miwili? Kwanini isiwe ktk mfumo kama ya kibenki ambayo wewe uliyechukua pesa ya watu ndio unawjibika kwa hizo siku ambazo tatizo limetokea? Ukikopa fedha benki kwa ahadi ya kuilipa baada ya mwaka ukanunua mashine ya kusaga nafaka kisha ikatokea tatizo isfanye kazi miezi 3 huwezi kuchelewesha kulipa pesa yao kwa miezi mitatu zaisi sababu dharula yako.
 
Uwekezaji wetu ni kwenye machimbo ya mchanga na kodi zote halali zinazohitajika kisheria tunalipia.

Huu mradi unahusika na machimbo ya mchanga lakini specifically tutawekeza kwenye excavator ya kuchimba mchanga na kupakilia kwenye magari tutapouuza.

Asante kwa swali zuri.
biashara ya mchanga inahitaji kulipia leseni na kusubili mteja aje anunue site. je pesa yote hiyo inafanya kazi gani?. au je utaratibu wa ufanyaji kazi wenu unakuwaje?. je site yenu iko wapi na soko lenu likoje?.
 
Ngoja nipige hesabu kidogo,

Data Given;
Mtaji 40,000,000
Hisa 1 = Tshs 500,000
Faida = 150% x 40,000,000 = 60,000,000/=

1) Idadi ya Hisa (Number of Shares)
= Tshs 40,000,000/Tshs 500,000 kwa hisa 1
= Hisa 80

2) Faida kwa kila Hisa (profit per share)
= Tshs 60,000,000/ Hisa 80
= Tshs 750,000/ Hisa 1

3) Uwiano wa Mapato na Mtaji (Return on Capital Invested - ROCE)
= Tshs 60,000,000/40,000,000 x 100%
= 150% (also given)

4) Muda wa kurudisha mtaji (Payback period)
= Mtaji / [Mapato kwa Mwezi]
= Tshs 500,000 / [ Tshs 750,000/12months]
= 500,000 / [Tshs 62,500/ 1month]
= 8 months

Assumptions,
1) Biashara inangiza faida sawa kila mwezi (no peak no lower season)
2) 150% (Tshs 60,000,000) ni faida baada ya mtaji na gharama zingine kutolewa (net profit)
3) 40,000,000 ndio mtaji pekee (Neither excess nor deficit)
4) "Other things kept constant"
but market vipi?. wanamkataba wa mnunuzi huyo?. je kama mwaka mzima wakiuza only 6 month itakuwaje?
 
Umefafanua vema lakini mdau alietoa pesa nabikatokea tatizo/dharula kazi haijafanyika huyu mdau atathibitishaje kazi haijafanyika? Je hii haiwezi kuwa backdoor ya kuchelewesha siku za kutimiza mwaka wa siku za kazi? Wakati huo mashine ikiwa imetumika zaidi ndipo inapochoka na kufa au kuharibika mara kwa mara na kuongeza siku za matengenezo ambazo hazi hesabiwi ktk malipo?

Kwanza kabisa kuwekeza ni amana na imani kwa pande mbili. Kama hakuna kuaminiana ni heri usiwekeze.

Pili, miradi yetu ipo wazi na unaweza kuitembelea wakati wowote na kujionea kinachoendelea.

Tatu. Hatuna sababu ya kutafuta "backdoor" kwa kuwa tuna measures tulizojiwekea ili tuhakikishe mwekezaji always analipwa zaidi in advance ili ikitokea chochote cha kuchelewesha kazi basi kisimsibu mwekezaji.

Kwa kusema siku za kazi hatumaanishi kuwa siku za matengenezo hazijatiliwa maanani ki malipo. Kwa kusema siku za kazi ni kurahisisha mahesabu ya kulipa, na matarajio yetu ni kulipa haraka iwezekanavyo kabla ya siku 365 za kazi haijafika labda kutokee yalio nje kabisa ya uwezo wetu.

Kwa uzoefu wetu, tatizo kubwa kabisa ni wakati wa msimu wa mvua kubwa (masika). Hapo barabara hazipitiki na kazi za mchanga kwa maeneo mengi husimama hadi miezi mitatu. Lengo letu ni tuwe tumelipa hadi miezi ya mbele kabla ya msimu wa mvua kubwa.
 
but market vipi?. wanamkataba wa mnunuzi huyo?. je kama mwaka mzima wakiuza only 6 month itakuwaje?

Market ni yetu wenyewe. Tuna eka za machimbo ya mchanga zisizopungua 15 chini ya usimamizi wetu. Kila eka ni average ya mwezi mmoja kuimaliza.
 
Kwanza kabisa kuwekeza ni amana na imani kwa pande mbili. Kama hakuna kuaminiana ni heri usiwekeze.

Pili, miradi yetu ipo wazi na unaweza kuitembelea wakati wowote na kujionea kinachoendelea.

Tatu. Hatuna sababu ya kutafuta "backdoor" kwa kuwa tuna measures tulizojiwekea ili tuhakikishe mwekezaji always analipwa zaidi in advance ili ikitokea chochote cha kuchelewesha kazi basi kisimsibu mwekezaji.

Kwa kusema siku za kazi hatumaanishi kuwa siku za matengenezo hazijatiliwa maanani ki malipo. Kwa kusema siku za kazi ni kurahisisha mahesabu ya kulipa, na matarajio yetu ni kulipa haraka iwezekanavyo kabla ya siku 365 za kazi haijafika labda kutokee yalio nje kabisa ya uwezo wetu.

Kwa uzoefu wetu, tatizo kubwa kabisa ni wakati wa msimu wa mvua kubwa (masika). Hapo barabara hazipitiki na kazi za mchanga kwa maeneo mengi husimama hadi miezi mitatu. Lengo letu ni tuwe tumelipa hadi miezi ya mbele kabla ya msimu wa mvua kubwa.
Nashukuru kwa ufafanuzi. Lakini napinga suala la kuwekeza (kwa sole proprietorship) kulifanya liwe la kiimani kama imani kama vile tunavyo amini ktk masuala ya kidini. Imani ktk kuwekeza kibiashara inajengwa na mifumo ya uwekezeji ya taratibu kama za kibenki au vikundi kama saccos n.k. ambako kuna vitu vinakupa uhakika wa usalama wa pesa zako. Na ndio maana tunasajiri hizo biashara au vikundi au mabenki. Kuna kuwa na vuwazi sana jinsi ya usimamizi na auditing ya uendeshaji wake.
NB: Mradi mzuri na faida kubwa, watu wawe jasiri wawekeze. Fortune favours the bold. Penye risk ndio penye faida kubwa.
 
Nashukuru kwa ufafanuzi. Lakini napinga suala la kuwekeza (kwa sole proprietorship) kulifanya liwe la kiimani kama imani kama vile tunavyo amini ktk masuala ya kidini. Imani ktk kuwekeza kibiashara inajengwa na mifumo ya uwekezeji ya taratibu kama za kibenki au vikundi kama saccos n.k. ambako kuna vitu vinakupa uhakika wa usalama wa pesa zako. Na ndio maana tunasajiri hizo biashara au vikundi au mabenki. Kuna kuwa navuwazi sana jinsi ya usimamizi na auditing ya uendeshaji wake.
NB: Mradi mzuri na faida kubwa, watu wawe jasirivwawekeze. Fortune favours the bold. Penye risk ndio penye faida kubwa.
Sijamaanisha imani ya kidini nimemaanisha imani kati ya mwekezaji na msimamizi.

Samahani kama umeelewa vingine.

Ahsante sana kwa kukumbushia kuhusu usajili, tumelifikiria hilo na tupo kwenye mchakato wa kusajili SACCOS mpya, pitia uzi huu Vitendo SACCOS - kukopeshana bila riba
 
Sijamaanisha imani ya kidini nimemaanisha imani kati ya mwekezaji na msimamizi.

Samahani kama umeelewa vingine.
Nimekuelewa Mzee wangu, ila namaanisha kwa hii biashara ilivyokaa kwa maelezo haya tu yaliyopo hapa JF kuamini na kuwekeza pesa yako ipo kama unatakiwa uamini kirahisi rahisi tu kama tunavyo amini masuala ya kidini. Kule huitaji insurance policy yeyote ili kuweza kuamini ukitenda uliyoambiwa basi utaingia mbinguni/peponi.
 
biashara ya mchanga inahitaji kulipia leseni na kusubili mteja aje anunue site. je pesa yote hiyo inafanya kazi gani?. au je utaratibu wa ufanyaji kazi wenu unakuwaje?. je site yenu iko wapi na soko lenu likoje?.
Sasa hivi machimbo yetu yanafanya kazi na magari yanapakiliwa kwa mkono.

Tunahitaji hiki kijiko ili tuongeze mapato.
 
Nimekuelewa Mzee wangu, ila namaanisha kwa hii biashara ilivyokaa kwa maelezo haya tu yaliyopo hapa JF kuamini na kuwekeza pesa yako ipo kama unatakiwa uamini kirahisi rahisi tu kama tunavyo amini masuala ya kidini. Kule huitaji insurance policy yeyote ili kuweza kuamini ukitenda uliyoambiwa basi utaingia mbinguni/peponi.

Huwa ninashauri wawekezaji waingie mkataba wa kisheria na sisi kupitia wanasheria wao ili wawe na amani. Sisi mikataba yetu ni local.
 
Back
Top Bottom