Sasa tumewaletea uwekezaji mpya unaolipa kihalali

Karibu sana kwenye mkutano wetu wa kuchagua viongozi. Vitendo SACCOS Inawaalika Wapenda Maendeleo Wote


Update...

Wadau,

Kwanza tunashukuru AlhamduliLlah mkutano umeenda vizuri na umeisha salama.
Tunafuraha kuwafahamisha wadau wote kuwa mkutano umeenda vizuri kabisa na umefana sana.

Tulianza kwa kukaribishwa na Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Vitendo...

Kisha nikaongea kidogo mimi kuwakaribisha wajumbe wote...

Baada ya hapo ikaanza semina ya ushirika iliotolewa na Afisa Ushirika wa wilaya ya Kibaha, Bwana Msangi. Semina ilikuwa ndefu kidogo lakini ilitoa mwangaza mpana wa nini SACCOS, vipi iongozwe, nini haki za Wana SACCOS na vipi haki zao zinalindwa na kusimamiwa na sheria rasmi za vyama vya ushirika na vipi serikali inasimamia vyama vya ushirika.

Yalizuka maswali mengi kiasi na hususan lilipoongelewa suala la kuendesha saccos kwa riba.

Hatimae kila mtu akaelewa kuwa hakuna tatizo kubwa isipokuwa ni namna tu ya mfumo wa uendeshaji SACCOS bila riba utavyofanyika.

Hilo na mengine yaliojiri mtajionea mkanda wa video.

Baada ya semina ukaanza mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa muda. Ulioendeshwa na kusimamiwa na Afisa Ushirika kama sheria zinavyotaka.

Hatimae tukapata kamati ya uongozi wa muda ya uanzilishi wa Vitendo SACCOS Ltd., kwa mujibu wa Sheria na chini ya usimamizi wa Afisa Ushirika wilaya ya Kibaha.

Kamati hio ya muda ikamteua Katibu wa kwanza wa muda wa Vitendo SACCOS Ltd., chini ya usimamizia wa Afisa Ushirika wilaya ya Kiabaha.


Mambo yote hayo yapo kwenye video na picha. Zitakapokuwa tayari, tutapandisha video YouTube na kwenye tovuti yetu (inayoanadaliwa kwa sasa) tutapandisha video na picha.

Tunakaribisha maswali.

Asanteni na karibuni kujiunga na Vitendo SACCOS Ltd. kwa faida ya wengi.

Abdul Ghafur
Mwenyekiti
Mobile / Whatsapp 0625249605
 
Wadau...

Tumeanza kupokea wanachama kiukamilifu. Kiingilio, hisa na akiba. Na uwekezaji kwenye miradi mbali mbali.

Kwa maelezo zaidi whatsapp au piga 0625249605
 
Wanachama na Wana hisa wa Vitendo SACCOS wanategemea kuzindua na kuanza kazi miradi yao mitatu mipya hivi karibuni.

Miradi hiyo mitatu yote iliyo nje ya Vitendo SACCOS lakini imebuniwa na Wana VTS na itaendeshwa kwa njia ya kuchangiana mitaji na kugawana faida kwa muda maalum.

Miradi inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni ni, mradi wa ukumbi wa sinema na mikutano, unaoweza kukaa watu 100, unatambulika kama mradi wa Vitendo Cinema Hall. Huu ni mradi wa muda mfupi kwa waliowekeza. Inatarajiwa kuwa mara tu utakapoanza hivi karibuni, wote waliowekeza kwenye mradi huu kuanza kupata mafao yao na faida ndani ya miezi sita.

Mradi mwingi unaotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni unaojulikana kwa jina la Vitendo Bricks, mradi huu ni wa muda wa kati. Mradi huu utajumuisha utengenezaji wa matofali ya aina tofauti tofauti na pia kwa siku za mwanzoni unatarajiwa kuwa na bidhaa tofauti zinazotokana na mchanga, kokoto na simenti.

Mradi huo pia unatarajiwa kuwa na uwezo wa kutengeneza bidhaa zote za ujenzi zinazotokana na simenti, kokoto na michanga.

Mradi mwengine kuanza hivi karibuni ni mradi wa kijiko (excavator) ya kuchimba na kupakilia mchanga. Mradi huu upo kwenye matayarisho ya mwisho na unategemewa kuanza hivi karibuni. Huu ni mradi unaotarajiwa kuanza kulipa mafao ya wawekezaji na kukamilika ndani ya siku 365 za kazi.

Tunawakaribisha nyote kujiunga na Vitendo SACCOS Ltd. Kwa faida ya wengi.

Vitendo SACCOS imedhamiria kufanya mabadiliko ya uwekezaji Tanzania. Na sasa unaweza kuanza kuwekeza na VTS kwa kuanzia Shillingi 10,000 tu.

Kwa maelezo zaidi, wasiliana nasi kwa simu au whatsapp namba 0625249605.

Ahsanteni sana.
 
Wadau...

Tunafuraha kubwa kuwafahamisha kuwa mradi wetu tulioutangaza humu JF tuliouita mradi wa excavator sasa umeanza kulipa mafao kama tulivyoahidi.

Tunawashukuru sana wote waliowekeza na tunaomba Mwenyeezi Mungu atujaalie tuendelee kulipana kama tulivyotarajia.

Ahsanteni.
 
Wadau...

Tunafuraha kubwa kuwafahamisha kuwa mradi wetu tulioutangaza humu JF tuliouita mradi wa excavator sasa umeanza kulipa mafao kama tulivyoahidi.

Tunawashukuru sana wote waliowekeza na tunaomba Mwenyeezi Mungu atujaalie tuendelee kulipana kama tulivyotarajia.

Ahsanteni.
Natoa shukran zangu nyingi sana tena, kwanza kwako "babu" Abdul, halafu kwa Bi Zainab. Kweli kabisa "mafao" twala.

Binafsi nasema nimewekeza miradi yenu yote, kuanzia wa boda boda wa kwanza , wa pili, mchanga, excavator, na VIP na hivi karibuni In shaaaa Allah ntanunua hisa za Vitendo Bricks.

Kwa ufupi, nlikuwa sipo sasa nimerudi. Ahsanteni benki imetuna kwa mafao na sasa nawajulisha kuwa nahamisha zote na kuzileta kwenye akaunti zenu zote. Kama mlituambia tukae "mkao wa kula", sasa nawaambieni "kaeni mkao wa kupika".

Nimeipenda "vunja kibubu".
 
Natoa shukran zangu nyingi sana tena, kwanza kwako "babu" Abdul, halafu kwa Bi Zainab. Kweli kabisa "mafao" twala.

Binafsi nasema nimewekeza miradi yenu yote, kuanzia wa boda boda wa kwanza , wa pili, mchanga, excavator, na VIP na hivi karibuni In shaaaa Allah ntanunua hisa za Vitendo Bricks.

Kwa ufupi, nlikuwa sipo sasa nimerudi. Ahsanteni benki imetuna kwa mafao na sasa nawajulisha kuwa nahamisha zote na kuzileta kwenye akaunti zenu zote. Kama mlituambia tukae "mkao wa kula", sasa nawaambieni "kaeni mkao wa kupika".

Nimeipenda "vunja kibubu".
FaizaFoxy ni kipindi kirefu sikuona huu mwandiko.
Karibu tena mkuu
 
Milion 40 kwenye heavy equipment? Nan analinda pesa yangu incase mradi ukifeli? Au ndo kama ya zile benk zilizofungiwa? Kurudishiwa mil moja na nusu tu? Hebu jaribu kunishawishi
 
Milion 40 kwenye heavy equipment? Nan analinda pesa yangu incase mradi ukifeli? Au ndo kama ya zile benk zilizofungiwa? Kurudishiwa mil moja na nusu tu? Hebu jaribu kunishawishi
Uwekezaji una risks zake. Nasi hatuna guarantee ya faida, tukifanya hivyo tutakkuwa tunaingia kwenye riba. Na hilo hatutaki.

Ni mahesabu. Heavy equipment ipo na inafanya kazi kwa sasa, by the way thamani yake ni way above the 40m. Be wise.

Pia kwa kukujulisha tu, tumekusanya zaidi ya million 65, million 15 juu ya tulivyotarajia awali. Tunashukuru mradi umeanza kuzalisha na excavator ipo kazini...
upload_2018-1-21_11-21-21.jpeg

upload_2018-1-21_11-22-55.jpeg
 
Tunataraji kuanza mradi wa Excavator II hivi karibuni, kaeni mkao wa kuwekeza.

Msione tunashughulika sana na excavator, hizi excavator tunazifanyia kazi sisi wenyewe, tuna eka za mchanga tunaouza na hizi zinatumika kupakilia kwenye trucks kama muonavyo picha juu hapo.
 
Back
Top Bottom