Sasa ni Rasmi Magufuli amegoma kufa!

Kifo chema Cha kufia mbele ya viongozi wa dini? Acha vichekesho bana.
Soma hapa itakusaidia
Yakobo 5:14-15
Neno: Bibilia Takatifu
14 Je, kuna mtu miongoni mwenu aliye mgonjwa? Basi awaite wazee wa kanisa wamwombee na kumpaka mafuta katika jina la Bwana. 15 Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa huyo na Bwana atamwinua. Kama ametenda dhambi, atasamehewa.
 
Wamekufa viongozi wengi wa nchi hii, lakini wakati wote Magufuli anaonekana kuongelewa kila mara na kila sehemu.

Wengine wanasema angekuwepo tungekuwa nchi ya ahadi kwa sasa, wengine wanasema bwana ya Nyerere lingekuwa limeshaisha na hivyo mgawo wa umeme tungekuwa tunausikia tu.

Treni Dar Dodoma ingekuwa tayari. Upigaji wa hela za umma ungekuwa mdogo sana.

Hadi 2030 tutasikia mengi.

Jana watu walilia, mkuu wa majeshi mstaafu alilia.
Msalimie!
 
Hicho kitabu chako kinaaminika na Kila mtu humu duniani ama? Naona unaniwekea mistari kama na Mimi ni muumini wa hicho kitabu chako.
 
Hicho kitabu chako kinaaminika na Kila mtu humu duniani ama? Naona unaniwekea mistari kama na Mimi ni muumini wa hicho kitabu chako.
Sawa shekhe ila kwa imani yetu ni ufalme kufa katika kristo

Ni kama nyie mnapokaribia kufa si huwa mnatamka shahada
Ili kuthibitisha imani ya Muislamu kwa kusema:

"La ilaha illallah, Muhammadur rasulullah"
 
Utakuwa na ujinga wa kipaji, unadhani mtu asipokuwa mkristo basi automatically ni muisilamu! Tafuta takwimu ya kidunia uone wakristo ni wangapi, na waisilamu, kisha uje tuendelee na mjadala. Sio Kila mtu Yuko kifungoni kwenye hizo dini zenu.
 
Wamekufa viongozi wengi wa nchi hii, lakini wakati wote Magufuli anaonekana kuongelewa kila mara na kila sehemu.

Wengine wanasema angekuwepo tungekuwa nchi ya ahadi kwa sasa, wengine wanasema bwana ya Nyerere lingekuwa limeshaisha na hivyo mgawo wa umeme tungekuwa tunausikia tu.

Treni Dar Dodoma ingekuwa tayari. Upigaji wa hela za umma ungekuwa mdogo sana.

Hadi 2030 tutasikia mengi.

Jana watu walilia, mkuu wa majeshi mstaafu alilia.
Watu walilia,mkuu wa majeshi mstaafu alilia.

"Huyu mkuu wa majeshi siyo mtu?
 
Nikawa nawaza kwa mbaali,

Ni kama kifo cha Ruksa watu walitaka kiwe big issue kuliko mwamba Jiwe.

Imagine juzi Konda Boy anasema rais atapokea changamoto za mwananchi kama kuenzi upokeaji wa changamoto alivyofanya mzee Ruksa, nikawaza

Hivi kati ya Ruksa na Jiwe nani alikuwa mwaasisi wa dhati kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi papo kwa papo.

Jibu likaja kwamba maumivu niliyo nayo juu ya JPM sio ilivyo kwa hao tunaotegemea kutuongza kumuenzi,

Ila ukweli utabakia pale pale Mwamba ni kipenzi cha mamilion ya watanzania, hata mmunyamazie kaburi lake litafukuta na kunena jambo.
Mwamba anawatesa sana.
 
Wamekufa viongozi wengi wa nchi hii, lakini wakati wote Magufuli anaonekana kuongelewa kila mara na kila sehemu.

Wengine wanasema angekuwepo tungekuwa nchi ya ahadi kwa sasa, wengine wanasema bwana ya Nyerere lingekuwa limeshaisha na hivyo mgawo wa umeme tungekuwa tunausikia tu.

Treni Dar Dodoma ingekuwa tayari. Upigaji wa hela za umma ungekuwa mdogo sana.

Hadi 2030 tutasikia mengi.

Jana watu walilia, mkuu wa majeshi mstaafu alilia.
Ukigusa mioyo ya watu...hakika ujapokufa utakuwa bado unaishi...Ref.Bob Marley
 
Mkuu Kipindi Vita Inaanza nilikuwa sina umri mkubwa sana japo nilikuwa Mtoto ila baadae nilijitafutia Ukweli kwa sababu Vita ilifanikiwa kumuua kaka Yangu pia!

Kipindi vita inaanza nilikuwa Nina umri wa miaka 6 mwaka 1978 na iliisha mwaka 1979 nikiwa na miaka 7..

Ukitaka kubalance story yote ya Bita vya Idd amini..
USitafute story kwa upande mmoja Nenda kagera Soma historia ya pale uliza wazee wa pale ukitoka hapo nenda Uganda uliza watu wa uganda..

Kiufupi ni kuwa Nyerere alitaka Rafikiye Obote ndo awe Rais..
Na alifanikiwa kufanya hivyo..
 
Mtaongea mengi ila rohoni mwenu mnamkumbuka. Binafsi hata juzi nililia tena. Endelea kupumzika baba yetu kipenzi cha watanzania
Pole sana.

Mungu akufariji. Mimi siku natangaziwa na umri wangu huu eti sikuamini kama kweli kafa.
 
Mimi mmoja wa wakubwa wa jeshi alikuwa mzazi wangu kabisa hadi mkuu wa majeshi msuguri watoto wake tunajuana maana tulikuwa marafiki ...siku moja msuguri alikuwa anaojiwa kwenye tv akamtaja mzee wangu...jina la mzee wangu lipo hadi kwenye kitabu kile cha kingereza cha vita vya uganda na vitabu vyote yupo ...nimeishi sana kwenye makambi ya jeshi musoma kuna sehemu inaitwa fotikoma kuna kambi sijui chuo cha jeshi kulikuwa na swimming pool ... hivyo uwezi kunidanganya nyumbani kulikuwa hadi na msanduku ya radio call mikubwa ya kivita na sisi kipindi hicho tulikuwa na tv ya mbao huo.mwaka 79 tayari tulikuwa tunamiliki tv
Mkuu naelewa unachokisema lakini kaa ukijua kuna Sheria za privacy za kijeshi...Baba yako hawezi kukwambia kwamba Eti ukweli ulikuwa huu..
Hiyo ni sawa na kesi ya uhaini mkuu
 
Wivu kwa kuwa walienda kumuombea dakika za mwisho na hicho kitu ndio kinawatesa sana hadi mnawachukia maaskofu walioenda kumuombea
Omba na wewe Mungu akujalie kifo chema kama Magufuli
Hakuna tatizo la kuombewa maana ndiyo kazi ya makuhani kuombea watu.
 
Ngoja niwa-tag wazazi wa Erick Kabendera, Ben Saanane, Aquiline Aqulina, Azory Gwanda, James Rugemalira, Bollen Ngetti, Yusuf Manji, Mo Dewji, Antony Dialo na wengineo nao wasome.
 
Mkuu wa makeshi kwa kawaida anatakiwa kulilia tumboni. Akimwanga machozi nje ni kiwango Cha juu Cha huzuni, kimevuka mipaka
Umesema hivi.
"Watu wamelia na mkuu wa majeshi amelia"
Hii ina maanisha kuwa kuna watu wamelia,lkn kiumbe mwingine ambaye siyo mtu (mkuu wa majeshi mstaafu naye amelia).
 
Back
Top Bottom