Chakaza
Platinum Member
- Mar 10, 2007
- 41,027
- 74,714
Baada ya kuwasikiliza kwa kina watangaza nia wote wa CCM na hoja zao, watu wamejiongeza na kuwaangalia historia zao za utendaji huko nyuma, dhamira zao kulingana na historia zao na makundi yanayowasukuma na kuwaunga mkono katika mbio zao za kushika wadhifa wa juu zaidi nchi hii.
Mijadala iliyoshika kasi ndani ya jamii inaonyesha kuwa badala ya watu kujenga imani na hao waliojitokeza sasa Imani ndio imepotea zaidi na ni kuwa hata Wanachama wa kawaida wa CCM ambao huwa hawanufaiki moja kwa moja na ufisadi wa viongozi wa juu wa chama chao nao wamebadili mwelekeo na kuhitaji kufanya mabadiliko ya viongozi wa juu licha ya kuwa wao wataendelea kuwa Wanaccm.
Katika watangaza nia wote hakuna aliyeonyesha kuja na jambo jipya zaidi ya porojo, na kwa vile sasa Watanzania wameshachoka na porojo na ushabiki na mambo yote yaliyo wafanya wataabike kwa muda mrefu, waibiwe kile kidogo walichonacho huku ndugu zao wanashindwa kusoma na kufa kwa maradhi yanayotibika NI DHAHIRI HAKUNA ATAKAYE CHAGUA RAIS TOKA CCM.
Hayo yamedhibitika na mazungumzo yaliyo mitaani na huko vijijini (ambako ndio mtaji wa CCM) sasa wameshaonyesha wazi kuwa wamechoka kudanganyanywa.