Sasa ni dhahiri, Rais hatatoka ndani ya CCM

Sasa ni dhahiri, Rais hatatoka ndani ya CCM

Mkuu nimecheka sana nilosikia kuwa Jangala naye eti kasema atatia nia wasimdharau. Una jua maana yake ni nini! Yaani yeye ndio kawadharau wote hao na kuwaona wanafanya maigizo kama yale yake.
nakuhakikishia kwamba jangala ndio mgombea tishio , kuna tetesi kwamba itv itarusha live nia yake .
 
Kufikiria CCM imechokwa na kuridhishwa na hizo fikra zenu ni wazi kuwa mmekata tamaa. Tusubiri octoba, muda huwa haudanganyi wala hauna porojo.

Je wewe bado uko na yule jamaa wa Monduli nimesikia hamfiki hata hatua ya mtoano, je akipigwa chini bado utamwuunga mkono mwingine, Karibu Ukawa maana huku safari ni ya uhakika siyo ya matumaini!!!!!!!!!!!!
 
Kama wagombea wanaitana vibaka unategemea nini kutoka katika mnyukano huo? Ondoka kwenye keyboard na nenda field ndio utakapo jua uhai wa CCM ulivyo mashakani

Kuna kamanda moja juzi aliposti kuwa kumtafuta mgombea anayefaa ndani ya ccm ni sawa na kumtafuta bikira wodi ya wazazi!!!!!!!!!!!!!
 
Tena kasema kibaka ni kibaka tu ata atembelee STK na gari ipeperushe bendera ya taifa mbele...bado atakua kibaka tu
 
mgombea toka chama chochote asiye unga mkono rasimu ya katiba ya warioba asahau kwenda magogoni,
maccm yaoga sana yanaliogopa hili, na kwenye ilani yao hili halimo. UKAwA hapo ndo watakapopigia bao, kuiunga mkono rasimu ya pili ya warioba, na kufufua upya mchakato wa katiba yenye maridhiano ya watu wote na makundi yote,
viva ukawa!! mwaka huu wenu!!
 
Ndo maana nilikwambia una PHD (Pure Head Damage). HUJIELEWI!!!
Bahati mbaya wewe ni timu ubwabwa..........so ni km tunapoteza muda kujibizana na ww.

Hiyo shahada humu JF naona wapo wengi wanayo. Tuwasaidie tiba.
 
Baada ya kuwasikiliza kwa kina watangaza nia wote wa CCM na hoja zao, watu wamejiongeza na kuwaangalia historia zao za utendaji huko nyuma, dhamira zao kulingana na historia zao na makundi yanayowasukuma na kuwaunga mkono katika mbio zao za kushika wadhifa wa juu zaidi nchi hii.

Mijadala iliyoshika kasi ndani ya jamii inaonyesha kuwa badala ya watu kujenga imani na hao waliojitokeza sasa Imani ndio imepotea zaidi na ni kuwa hata Wanachama wa kawaida wa CCM ambao huwa hawanufaiki moja kwa moja na ufisadi wa viongozi wa juu wa chama chao nao wamebadili mwelekeo na kuhitaji kufanya mabadiliko ya viongozi wa juu licha ya kuwa wao wataendelea kuwa Wanaccm.

Katika watangaza nia wote hakuna aliyeonyesha kuja na jambo jipya zaidi ya porojo, na kwa vile sasa Watanzania wameshachoka na porojo na ushabiki na mambo yote yaliyo wafanya wataabike kwa muda mrefu, waibiwe kile kidogo walichonacho huku ndugu zao wanashindwa kusoma na kufa kwa maradhi yanayotibika NI DHAHIRI HAKUNA ATAKAYE CHAGUA RAIS TOKA CCM.

Hayo yamedhibitika na mazungumzo yaliyo mitaani na huko vijijini (ambako ndio mtaji wa CCM) sasa wameshaonyesha wazi kuwa wamechoka kudanganyanywa.
Kamanda naona umeamua kujifari na kujiliwaza siyo mbaya unapungaza msongo wa mawazo.
 
Storyza chinua achebw ukisikia matokeo unaazima nguo ya kija. Hata kama jezi ya yanga
 
Storyza chinua achebw ukisikia matokeo unaazima nguo ya kija. Hata kama jezi ya yanga

Goli la mkono halitakuwepo maana hakuna kuchezea mpira eneo la hatari.
 
Kamanda naona umeamua kujifari na kujiliwaza siyo mbaya unapungaza msongo wa mawazo.

Kujifariji na kujiliwaza sasa ndio kumetimia rasmi pale Mlimani city baada ya kuita burudani ya wanaoitwa wasanii ili kupunguza msongo wa mawazo walao kwa kuwaona akina Wema wakinengua. Nadhani ule utakuwa ushauri wa Madaktari.
 
Back
Top Bottom