Sasa nakunywa chai kwa biskuti!

Usedcountrynewpipo

JF-Expert Member
Aug 1, 2012
3,638
2,720
Jamani nyie haya mambo ya kijamii ni magumu acha.
Hapa jirani na kwangu kuna dada mmoja anapika vitafunwa na chapati zake ni tamuuu, yani nikizila wala hata sijilazimishi na ninazipiga mpaka nashiba kwa raha zangu.

Pia hapo kwenye kona mbele kidogo kuna 'mama mkwe' naye anapika chapati. Yani kumaliza chapati yake moja natumia nguvu nyingi na inabidi nijilazimishe sana. Sasa tatizo ninashindwa kununua hapa kwa huyu dada na kumkwepa mama mkwe maana kila saaa anatupia jicho huku...
Na juzi kati baada ya kukaza roho na kumpotezea mama mkwe, alitukuta baa tunapiga vinywaji, yani baada ya salam kauli aliyotoa ni ya kutusisitiza tuje kununua chapati kwake na pale mlengwa alikuwa mimi tu kwa sababu wengine wote pale wanakaa mbali na kitaa chetu...

Yani nimekuwa kwenye dilema sasa nimeona kuliko kumpotezea mama mkwe na kununua chapati hizi tamu, bora tu ninywe chai kwa biskuti...
Au waungwana mnanishaurije?
 
umetumia lugha ya picha? au halisia?
Halisia mkuu. Nazungumzia hivi vitafunwa kwa ajili ya tumbo. Sio yale mambo yetu. Huyu mama huwa ana kabinti kake kazuri sasa nikawaga namtania kuwa nitakuja kuoa kwake kabinti kakimaliza shule, ndio u mama mkwe ulipoanzia hapo...
 
Hapo ni kutafuta dogo wa jirani jirani mbali mbali unamtuma kwa huyo mdada..... labda kama unapenda kumuangalia usoni unapo nunua Hahahaaaaaaaa
 
Back
Top Bottom