Sasa naanza kuwaelewa walioajiriwa

Sasa naanza kuwaelewa walioajiriwa

Baada ya kushauriwa na wana kwamba ukitaka kufanikiwa jiajiri.

Basi nikaacha kazi nikauza nyumba kuanza kuwekeza kwenye biashara.

Kilichofuata. Tusidanganyane ngoja niendelee kutumwa maisha yenyewe haya haya.

Nb sio kila binadamu kazaliwa kuwa tajiri wengine tumeubwa kutumwa using'ang'anize mambo
Utajipotezea muda.
Ndio Maana RC Paul Makonda anaajiriwa sio kwamba hajui kama Mwijaku amejiajiri.
 
Ni vizuri kuwa na ndoto ya biashara, lakini usiache kazi au kuuza mali kubwa bila mpango thabiti, ushauri wa kitaalamu, na mpango wa dharura. Anza kidogo, jifunze, kisha pandisha hatua kwa hatua.
 
Ingekua passion, consistency, and hard work makonda wa dala dala, mafundi ujenzi na mama ntilie wangekua wako na wealth maana ndiyo wanafanya kazi hivyo.
konda wa daladala ana miliki biashara ipi yenye uhakika?, maana na yeye ana tegemea neema za boss, dereva na uzima wa gari ili kupata kitu.

taking your game to another level ndio ina ku differentiate na wengine.

Utakuwa mama ntilie wa ofisi moja mpaka lini?, (expansion muhimu).

Kwenye ujenzi una wajua ma fomeni, hahaha hawa wana tafuta kazi, mafundi na hadi kuweka bei ya kupokea pesa na hesabu ya kumlipa fundi na vibarua.

Usipo jiongeza basi, huja wahi kumuona fundi ana vifaa vipya ana uza?, kesho akiwa na duka la ujenzi usi shangae.
 
Back
Top Bottom