Sasa mbona ananisumbua?

Sasa mbona ananisumbua?


Mi niko vizuri bwana, sija bahatisha
Everything happens for a reason ukute nayeye ndio ilikuwa breakthrough yake hiyo.

Lest say ningekuwa baba nikatumia hiyo point ningepata msamaha mapemaa.
Hahaha
Hiyo haiwezi fanya usamehewe kabisaa. Bibie hana shidaa alishamsamehe ila kurudiana naye ndo haitatokea, sawa baba mlezi eeeh
 
UKISIKIA MLIMA UMEHAHA AMINI KULIKO KUSIKIA HUYO MWANAUME AMEBADILIKA. HAUKUWA CHAGUO LAKE NDIO MAANA HATA NDOA ULIMLAZIMISHA.
HUYO MWANAO ASIKUPE PRESHA KWA SABABU HAJUI ULIVYOTESEKA NAE KWA SABABU YA HILO JINAMIZI, KAMA MALEZI YA BABA YAKE YANAMFAA ZAIDI AENDE TU LAKINI SIO KURUDIANA NAE.

NB: USHAURI WANGU UTAFANYA KAZI ENDAPO TU UTAKUWA UMESHAMFUTA MOYONI MWAKO😀
 
Dada zetu muwe na akili na muwe mnafanya maamuzi kama binadamu, yaani mtu kakufanyia ushenzi wote huo bado unauliza eti kama mrudiane au vipi?

Songa mbele achana na huyo fala.

Anataka akutumie na usipokuwa makini atakupora mali zako na kukuacha ukihangaika tena.

Mm Ni kijana mwenzenu, Nina utata kidogo ktk maisha yangu naomba mawazo yenu.

Nilipata kuwa na mahusiano na kijana mwenzangu wakat tukiwa chuo. Mapenz yetu yalikuwa matam tu tulipendana sana, mpk ilipofika hatua ya kumaliza chuo yule kijana akaenda kwao na mm nikawa nipo tu home.

Kwa vile kila mmoja alikua anakaa mbali na mwenzie na mm nilikuwa cwez kukaa mbali nae nikaamua kumshauri aje nyumbn kuniposa anioe. Yaani kumuambia suala la ndoa tu akawa km nimemfukuza.

Nikafanya jitihada nikamtafuta nikamuambia lazima anioe Mana alishakula tunda langu, ikawa ugomvi hataki mpk wakaingia wazee akalazimishwa akalazimishwa ndo akakubali kunioa.

Baada ya kunioa nilijuta Bora ningekaa nyumbani nikatafuta issue nikafanya , yn mume alikuwa ananipiga, ananisimbulia, ananisimanga kila baya ananifanyia. Huduma Hana ukimuambia anasema kachukue kwenu me sikutak.

Dah nikastahmili nikapata mimba, nilipopata tu mimba mume wangu alizid vituko harud kabisa cjui analala wap. Siku Moja akaniambia nenda kwenu me nataka kusafr, apo nilikuwa na mimba 6 months.

Kumbe yule bwana hakusafr Wala nn anaonekana mjini anadunda nikaja kusikia keshaoa mke mwengine kwangu hapiti kabisa. Nikimpgia cm hapokei Hana mawasiliano na mm iliniuma sana. Kwa uchungu na hacra nikazaa nikiwa na mimba miez Saba.

Baada ya kujifungua niliumwa sana na mtoto pia alikua mgonjwa, babaake alibadlisha namba na tulipokuwa tunakaa akahama.

Ndipo nilipoenda kwao kumuulizia lkn nashangaa ndugu zake walinidharau na kunicheka Kisha wakanipa waliosema mzigo Wangu ambayo ilikua Ni talaka.
Mume wangu aliniacha ktk Hali hii ngumu mm naumwa na mtt anaumwa kwa kweli nilikua namuhitaji nikaondoka nikashukuru mungu.

Kwa kwel nilipoteza muelekeo nikakosa dira nikijiangalia baba yangu alishakufa, mama nae mtu mzima Hana kitu. Nilisomeshwa kwa msaada wa jumuia fulan lkn nilishindwa kufanya vizur kutokana na mapenz nilijuta na kulia sana.

Sikua na msaada nikawa nauza maandazi kwa ajili ya kujikimu mm na mtoto na mama pia.

Siku Moja katika pita pita zangu nikakutana na rafiki yangu wa zamani alinishangaa kuona nilivyochoka akaniuliza yamenikuta yepi? Nikamuhadithia akanihurumia sana nilishaanza kukonga wakati nilikuwa na 23 years old.

Rafiki yangu akaniuliza unataka kufanya kaz za ndani Oman nikamuambia ndio, akanipeleka kwa mtu fulan hivi akaniambia yy atanifanyia Safari. Bac nikaondoka Tanzania nikaenda Oman mwanangu akiwa na miaka 3 na alikua anaendelea vizur japo alikua mwembamba sana.

Nashkuru mungu kumbe hii ilikua ndio njia yangu ya kunifungulia milango ya kheri na barka, nikawa napata pesa Sasa natuma nyumbani. Niliporud nikakuta nyumba yetu ishajengwa vizur na milango ya maduka miwili. Sikutosheka nikarud Tena Oman tukafungua biashara pale home duka Moja la vyakula na Moja stationaries Kuna ndugu zangu wanauza pamoja na mama. Niliporud Tena nikajenga nyumba yangu na biashara ikakua nimekod mlango mjini nikaweka nguo za kike. Huu mwaka wa tano nipo Oman nataka nikirud next year iwe ndo mwisho sirud ntakuwa na kila kitu nilichokuwa nahitaji.

Tatizo Sasa yule kijana aliyeniacha kwa dharau akanifanya nichukie wanaume wote amepata habari zangu na mtoto kampa namba yangu ananipigia kila sekunde ananiambia mke wangu turudiane tulee mtoto wetu. Jaman na mtoto nae anasema nirud kwa babaake km sitak nikiolewa na mtu mwengine atamuua.

Nipo njia panda nampenda sana mwanangu Ila siko tayar kurudiana na yule babaake nifanyeje jamani!!
 
Dada zetu muwe na akili na muwe mnafanya maamuzi kama binadamu, yaani mtu kakufanyia ushenzi wote huo bado unauliza eti kama mrudiane au vipi?

Songa mbele achana na huyo fala.

Anataka akutumie na usipokuwa makini atakupora mali zako na kukuacha ukihangaika tena.
Ahsante sana
 
Rudisha moyo nyuma wewe! Kwani wagombanao ndio wanaopatana, inawezekana amekua kiakili kwa sasa, mpe nafasi nyingine mkaijenge familia
 
Hivi hii busara umeitoa wap shunie Jaman khaa mbna sio wa hvyo wewe.
Back to the topic kama unaomba ushaur means bado unampenda other wise usingejisumbua nae.
So kama unamtaka mrudie otherwise usje ukaanzisha thread nyengne
Mi bado nafuatilia kwa karibu uhusiano wa Shunie ma thatsit

Lazima waraka wetu uboreshwe...
 
Kuna wanaume wana roho mbaya,nadhani hata shetani huwa anawashangaa.
 
Mwanao ana akili mbovu kama za baba yake huenda amemrithi akili kwa kiwango kikubwa ndiyo maana anatishia kuja kumuua mme atakayekuoa, sasa usiendelee kufikiria kurudi kwa huyo jamaa dada, huenda atakutesa tena, mwambie mwanao wewe ndiye mama yake uliyemzaa lazima akuheshimu kama hataki bhasi aondoke akafanye akapige kambi na babaye.(mikwara inasaidia).
 
Maneno mawili tu
KA - TA
Kata mawasiliano nae sio mtu huyo anataka kukutumia, sio yeye wala ndugu zake Leo hii anajua kama ana mtoto eeh!!
Ukitaka M/Mungu akupige kofi la pili La maisha baada ya lile la kufeli kutokana na mapenzi basi rudiana na Huyo Filauni
 
Mie nakulaumu Sana Sana. Sio tu kurudi kwa huyo bwana, Hata huo muda wa kumfikiria unautoa wapi? Kwa nini huo muda wa kumfikiria huyo "mzazi mwenzio" usiutumie kwa kucheka.
 
Mie nakulaumu Sana Sana. Sio tu kurudi kwa huyo bwana, Hata huo muda wa kumfikiria unautoa wapi? Kwa nini huo muda wa kumfikiria huyo "mzazi mwenzio" usiutumie kwa kucheka.
Nacheka sana sa iv I'm not dealing with him nmore mpk naacha kupokea cm ngeni mana najua ni yy tu hamna mwengne, angalau sasa nina furaha ya linah sanga ndo ringtone yangu and is my favourite song.
 
Kama amefikia hatua ya kusema ucporudi atamuua Mtoto, tambua huyo co mtu sahihi kwako
Kwa yote aliyokufanyia Bado unapokea hata cmu yake
Kata mawasiliano nae na huyo mtt mkanye aache upumbavu
Tafuta Mwanaume wa kuishi nae ambae unaona kwako ni sahihi,hiyo itasaidia kuondokana na stress za huyo mpuuzi
 
Huyo mtoto wako naye ana akili za kibashite?

Haiwezekani uhangaike hivyo alafu aje alete madoido eti atamuua mtu. Muache aende kwa baba yake siku akijisikia aje kwako. Si lazima uishi naye.
hhahahaahaha
 
kwanza ulikosea sana kumlazimisha akuoe, hilo ni kosa ambalo akina dada wengi wanakosea, lakini ndio kujifunza maisha pia! siku zote wanasema majuto ni mjukuu, pili huyo mtoto wako atakuwa amechukua roho ya baba ake (roho ngumu) kama ameshajitambua na kumjua babaake mwache aende akaishi nae, ila wewe usijaribu kurudi kwake hata bure
 
Back
Top Bottom