Sarkozy speaks out against burka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sarkozy speaks out against burka

Discussion in 'International Forum' started by macho_mdiliko, Jun 22, 2009.

 1. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #1
  Jun 22, 2009
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,318
  Trophy Points: 280
  French President Nicolas Sarkozy has spoken out strongly against the wearing of the burka by Muslim women in France.
  In a major policy speech, he said the burka - a garment covering women from head to toe - reduced them to servitude and undermined their dignity.
  Mr Sarkozy also gave his backing to the establishment of a parliamentary commission to look at whether to ban the wearing of burkas in public.
  In 2004, France banned the Islamic headscarves in its state schools.........
  ...........
  full story go to: BBC NEWS | Europe | Sarkozy speaks out against burka
   
 2. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #2
  Jun 22, 2009
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,318
  Trophy Points: 280
  Safi sana Sarkozy.... hii kitu ya binadamu kutembea na "majumba" kama konokono ni udhalilishaji wa hali ya juu.....
   
 3. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #3
  Jun 22, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  He is stupid
   
 4. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #4
  Jun 22, 2009
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,318
  Trophy Points: 280
  Why do u think so?
   
 5. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #5
  Jun 22, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Suala la wanawake wa kiislamu kuvaa burka ni sehemu ya shuruti ya stara kwa mwanamke wa kiislam(hijab), na wanawake wa kiislamu waumini wa kweli hawajawahi kulalamika kuwa hiyo kwao ni adhabu,kero, mzigo au shida. Kujistiri maungo kwa mwanamke ni sehemu ya kuutukuza utu na heshima ya mwanamke n.k. Haya Sarkozhy hayajuwi, na anawasemea wanawake wa kiislamu wala hawajamtuma,nahisi nchi yake haipendi kuwaona wanawake wa kiislamu wakijistiri, anataka tujuwe kuwa Ufaransa haiheshimu uhuru wa kuuabudu wa raia zake na wageni.
  Wamarekani walipowafukuza wataliban Afghanistan walikurupuka kuwaambia wanawake kuwa sasa wapo huru kuvaa watakavyo, jibu walilolipata kuwa, masuala ya kivazi ni sehemu ya utamaduni wao wa kiislamu unaowapa stara na heshima.
  Kwa Sarkozy ambaye, anajuulikana historia yake ya kupenda mambo ya uchafu na uzinifu na wanawake waendao uchi, simshangai kukerwa na stara ya wanawake wa kiislamu, si ajabu anawaona heshima yao kubwa kwa stara yao kuliko hata ya mke kahaba aleyekuwa hawara yake zamani Carla Burni.
  Hajuwi nachokibwatukia.
   
 6. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #6
  Jun 22, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  hapa kuna swala zima la kuingiliwa kwa uhuru wa kuabudu na kujieleza.Kama mtu anapenda kuvaa burka kama kujieleza utamaduni wake tatizo liko wapi?

  Katika kutaka kupiga marufuku burka, Sarkozy anakuwa hana tofauti na wa Taliban wanaolazimisha burka na kupiga marufuku vichupi. Same game, different approaches.
   
 7. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #7
  Jun 22, 2009
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Junius, naomba nitofautiana na wewe kidogo. Wanawake wa kiislamu wanaovaa kininja tena nguo nyeusi wanataabika sana ila hawasemi tu. Wanatii tu kwa sababu wametishiwa kwenye quran kuwa watachomwa moto wasipokuwa watii. Hebu fikiria hilo joto la middle East na nguo hizo nyeusi ni mateso matupu ndugu yangu. Kufukuzwa kwa Wataliban huko Afghanistan na Wamarekani kulileta neema kwa wanawake kule maana walianza hata kwenda shule kwasababu ilikuwa mwiko wao wakae nyumbani tu wawastarehe wanaume ulikuwa ni uonevu wa hali ya juu sana. Wanaume nao tuliwaona kwenye TV wakijazana saluni kunyoa ndevu zao.
   
 8. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #8
  Jun 22, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Unaposema jambo useme kwa uthibitisho...hizo ni speculations...ambzo hazina nafasi katika reasoning. Kama mtu jambo halitaki hachelewi kusema wala hangoji asemewe, nakupa challenge ww nitafutie mwanamke muumini wa kweli wa kiislamu, aliesema au kupiga kelele kuwa hijabu inamkera. Kwanza nikuweke sawa hijab si adhabu ni stara. Utamaduni wa kwenda, uchi haupo katika uislamu,utamaduni wa mwa'mke kupandishwa jukwaani na chupi, sidiria au kutembea mtupu kama alivyozaliwa haupo katika uislam, wala utamaduni wa mke, binti wa mtu kupita majiani akayaonyesha maungo yake kila mtu akamuona haupo katka uislamu. Uislamu umeanza kumtukuza mwanamke kwa kuyaheshimu maungo yake kuyafanya bora kwa kuwa si kila mtu anayaone isipokuwa wa halali yake tu. Hakuna na ni marufuku kwa mwanamke wa kiislamu kwenda uchi na kuonyesha maungo yake hadharan au kuvaa nguo zisizo na staha, na rejea tena, si utamaduni wa kiislamu. utamaduni huu wanaoushabikia kina Sarkozy ni wa kumdhalilisha mwanamke. Kuhusu Taliban mm sikutaja habari za shule, nilichosema kuwa wamarekani waliona kuwa Taliban iliwalazimisha wanawake kuvaa hijab, walipowataka sasa kutovaa hijab, jawabu waliloambulia ni kuwa hilo si vazi lililoshurutishwa na Taliban bali Mw'mungu kwa manufaa yao wanawake, na wamekuwa wakilivaa tokea enzi na enzi kabla ya hata hao taliban hawajaingia madarakani.Niambie ni wanawake wangapi wa Afghanistan walivua hijabu zao baada ya taliban kuondolewa? Habari za kunyoa ndevu si umeziona kupitia CNN na BBC! sina comment katka propaganda levya.
   
 9. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #9
  Jun 22, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Asiban nguo hizo moja kwa moja. Mimi naona kama watu tuna lilia uhuru wa dini tulilie na uhuru wa mtu binafsi. Iwekwe tu sheria kuwa mtu anayetaka na avae lakini siyo lazima. Mwanamke mwenyewe kama ni mshikadini yake sawa atavaa ila kama na yeye hataki basi isiwe lazima.
   
 10. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #10
  Jun 23, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Alafu kitu cha ajabu sasa, Madaktari na walimu wengi kule Afghanistan ni wanawake.
   
 11. B

  Bull JF-Expert Member

  #11
  Jun 23, 2009
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sindio hawa wanao preach democracy, freedom ya kuabudi, speech etc? sasa watawambia nini serikali kama za Afghan, Iran, Midleeast watakapo lazimisha wanawake kuvaa nguo ndefu? Zikowapi so called Human right organisation?

  Kama France watapitisha hii sheria, itabidi zilenchi zinazo preach freedom zikaekimya kwasasababu hazitokua na credibility kuwambia wengine what is freedom. Westeners wanaanza kukosa misimamo
   
 12. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #12
  Jun 23, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Poor Sarkozy, jamaa ameshakufa kisiasa sasa anajaribu kutafuta namna ya kujirudisha tena kwenye gemu bila kujua kuwa approaches anazotumia ndiyo zinamwangamiza kabisa..
   
 13. S

  Semjato JF-Expert Member

  #13
  Jun 23, 2009
  Joined: Jun 26, 2008
  Messages: 225
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  mjinga sana!sijui alikuwaje rais wa nchi kubwa kama France
   
 14. J

  JokaKuu Platinum Member

  #14
  Jun 23, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,781
  Likes Received: 5,022
  Trophy Points: 280
  ..kwani Wafaransa wana utamaduni wa kuvaa burka?

  ..hili ni tatizo ambalo limepelekwa Ufaransa na wakimbizi toka nchi za Kiarabu.

  ..ilitokea aibu kubwa jamaa hawa wakazomea wimbo wa taifa wa Ufaransa walipocheza na Algeria.

  ..halafu tatizo lingine wanazaana sana, hawataki kusoma, hawataki kujifunza Kifaransa,hawataki kazi, na siku zote wanasingizia ubaguzi.

  ..Sarkozy aache ku-dance around the bush. akusanye tu wakimbizi hao, akawabwage walikotokea.
   
 15. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #15
  Jun 23, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Kiongozi Jokakuu,
  kwani kuvaa Burka kunakuwaje tatizo?
  Je waarabu waliokuwa Ufaransa wote ni wakimbizi, ambao wanazaana sana na hawataki kufanya kazi? Na kama wanazaana sana, je kuna sheria ya Ufaransa inayowakataza kuzaana?
  Je wanaovaa Burka wote ni waarabu? Je wote wamelazimishwa?
  Alichokifanya Sarkozy ni kujaribu kuprovoke jamii za minority nchini Ufaransa. Kwa sababu hapa leo tunaona hili la Burka lakini Ufaransa minority wananyanyaswa sana, sio waarabu peke yao. Kuna jamaa orignally ni mtu wa West Indies nilikutana naye pamoja na mwingine toka Martinique, hawa ni raia wa Ufaran sa lakini hawana fursa sawa na mfaransa mweupe.
  Jokakuu ni vyema ukajiunga kukemea tabia hii ya kuwaamurua watu mambo binafsi.
  Ufaransa ndio nchi inayoongoza duniani kwa kuwa na nude beaches nyingi, kwa Sarkozy nude beach ni ustaarabu zaidi ya Burka!

  mara mojamoja sio mbaya kuingia hapa ili kuona side B ikoje Press TV
   
 16. J

  JokaKuu Platinum Member

  #16
  Jun 23, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,781
  Likes Received: 5,022
  Trophy Points: 280
  ZeMarcopolo,

  ..hao wanaonyanyaswa kwa kuvaa burka wakimbilie zile nchi zinazoruhusu mavazi ya burka.

  ..nimekueleza kwamba burka haina asili Ufaransa. inaeleweka kabisa vazi hilo asili yake ni wapi.

  ..nadhani tatizo ni hao wakimbizi wanakaribishwa nchi za watu, wanakuwa comfortable, na kuanza kulazimisha mila na tamaduni zao kwa wenyeji wao.

  Mazingira,

  ..nchi za Ulaya na Marekani wanaponzwa na wema wao wa kupokea wakimbizi.

  ..kuna nchi kibao zinaruhusu burka. "Wafaransa" wanaotaka kuvaa burka wanaweza kuomba asylum huko.

  NB:

  ..hebu nenda Teheran au Riyadh ujaribu kufungua bucha la nguruwe au strip club uone kitakachokutokea.
   
 17. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #17
  Jun 23, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Hivi kweli mtanzania anaweza kumuelezea msomali kama mtu asiyependa kufanya kazi?
  Wasomali waliokuja Tanzania ndio wanafungua mahoteli na kuajiri watanzania. Mpakani Namanga ni wasomali wanafanya biashara zote pale.
  Jamani hizi stereotypes agains minorities siyo nzuri.
  Just because its not the black guys being victims of stereotype doesnt mean its ok to dance the music.
   
 18. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #18
  Jun 23, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Hata hizo nchi watakazoruhusiwa kuvaa Burka haimaanishi kila kitu kitafanana na tamaduni za kwao walikotoka, kwa hiyo tukiruhudu hii wakakimbilia Uturuki. Uturuki nao wanaweza kuwaambia hawaruhusiwi kuongea kiarabu, wakitaka waende kwenye nchi inayoongea kiarabu. Wakienda huko nako wakatafuta kigezo kingine cha kuwabagua etc. Ila cha msingi Jokakuu ni kuelewa kuwa wanaovaa Burka sio wote wakimbizi, na kwa Ufaransa wakimbizi wala sio majority.

  Kwani nani amelazimisha mila yake? Kuna mtu amelazimishwa kuvaa Burka?

  Halafu unaposema utamaduni wa sehemu nyingine usipelekwe sehemu nyingine unakuwa unakosea, kwani utamaduni wa ufaransa uko static? tamaduni zote ni dynamic. Sarkozy pia nyumbani kwake na ndugu zake bado watakuwa na tamaduni fulani za ki Bulgaria wanazo.

  Jokakuu, ubaguzi wa namna hii haupaswi kuachwa bila kukemewa. Kesho watakwambia wewe ukipika ugali unatoa harufu mbaya kwa hiyo lazima upike vyakula wanavyopika wafaransa wengine.
   
 19. J

  JokaKuu Platinum Member

  #19
  Jun 23, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,781
  Likes Received: 5,022
  Trophy Points: 280
  Zermacopolo,

  ..nadhani mtu anayetaka kuvaa burka akienda kuishi Ufaransa,Holland, au nchi nyingine zinazofanana na hizo, anakuwa amepotea njia huyo.

  ..unapoamua kuondoka kwenu, kuhamia, na kuwa raia wa nchi za watu, unapaswa KU-ASSIMILATE. hawa wenzetu kitu hicho hawakielewi kabisa.

  NB:

  ..matatizo hayo hayako wa wanaopenda kuvaa burka tu.

  ..wengine wanaonitibua zaidi ni gays. hawa wanajua kabisa jeshi,kanisa,..haliruhusu tabia zao. lakini unakuta wanajiunga humo, wanakaa kimya mpaka wamekubalika na kupewa madaraka, halafu ndiyo wanajilipua kwamba wao ni gays.
   
 20. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #20
  Jun 23, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  kwa hiyo waziri Batilda Buriani,Hawa Ghasia na wengine wakienda ufaransa inaabidi wafunue vichwa? Kumbuka sheria haihusu wanaohamia tu!!!
  Nadhani tatizo ni kutokuelewa essence ya burka na kutokuwa tayari angalau kujaribu kuelewa.
  Kuna wavaa burka wako Ufaransa generation nyingi kabla hata Sarkozy na familia yake hawajahamia Ufaransa.Sasa anataka kusema yeye ni mfaransa zaidi kuliko hao?
   
Loading...