Sarakasi za Matokeo zaendelea!

Sarakasi za Matokeo zaendelea!

wanajua kuwa shule zitakuwa hazina 'a' level mwaka huu.

watoe tu tangazo kuwa wamefaulu wote kwa kiwango cha a.

nchi yenyewe hii ya bora liende hivyo hivyo, tz imekuwa kama
haina mwenyewe.
 
Unao uhakika? Au unaropoka tu. Tena bora ungechangia na si kuanzisha mada ambayo hauna uhakika hata chembe. Acha kupotosha umma kwa mambo ya udaku na kufikirika. Hujui lolote kuhusu unachoongea

eleza sasa ukweli unaoufahamu baada kusoma na kuelewa uongo uko wapi kama hujui kitu ishia kusoma tu siyo dhambi mkuu
 
Huyu Prof.Mukandara kitambo sana tokea akiwa anaganga njaa na REDET kutoa data za uongo kumkampenia kikwete, haaminiki hata na ziara ya kwanza ya vasco walienda pamoja us baadaye akampa ukuu wa chuo UDSM, hana kitu, hana academic freedom mbele JK sababu ya njaa zake.........ndio maana maprof. critical pale udsm anawaboa wanasepa mfano baregu,mvungi, pia walizinguana mara kadhaa na marehemu prof.chachage...............hana maana huyo
 
Ukiona nchi imeingiliwa na viongozi wasio na credibility,integrity tayari ujue tatizo ni kubwa kuna nini sasa serikali haina uongozi thabiti serikali imekuwa serikali ya kudanganya wapi na wapi bwana wamechelewesha matokeo ya mitahani ya form six watoto nao wanakuwa affected psychologically hawajui hatima yao
 
Katika kile kinachoonekana kama kufanikisha mipango ya kuyaidhinisha kwa lazima Matokeo ‘mapya’ ya Kidato cha Nne,Serikali imedhamiria kutumia ipasavyo nafasi ya kutokuwepo kwa Prof .Rwekaza Mukandala kuyapitisha.

Prof.Mukandala ,ambaye ni Mwenyekiti wa NECTA na Makamu Mkuu wa UDSM, hayuko nchini kwasasa.Taarifa rasmi zinaoonesha kuwa Prof.Mukandala yuko nchini Marekani kuhudhuria Mahafali ya mtoto wake ambaye anahitimu katika chuo kimojawapo nchini humo.

Huku yeye akitarajiwa kurejea nchini mwishoni mwa juma lijalo,Serikali imeapa kuyapitisha na kuyaidhinisha matokeo hayo bila ya uwepo wa Mwenyekiti wa NECTA. Yuko kigogo mmoja wa NECTA ambaye amepangwa kukaimu Uenyekiti wa NECTA kwa ajili ya kupitisha matokeo hayo mapya tu.

Prof.Mukandala,akiungwa mkono na Katibu Mtendaji waNECTA,Dr.Joyce Ndalichako,tangu mwanzo wa mchakato wanapinga kusahihishwa au hata kupangwa upya kwa Matokeo ya Kidato IV-2012 kwa kile wanachosema kuwa Serikali ilishiriki kuyaidhinisha ya mara ya kwanza na hivyo haiwezi kuyabadili.

Katika siku za hivi karibuni,kumekuwa na mvutano mkali kati ya Maafisa Waandamizi wa NECTA na wale wa Serikali juu ya upangwaji upya wa matokeo hayo. Serikali inasisitiza kuwa matokeo hayo lazima yabadilishwe ili kukidhi haja ya Taifa kupata ‘elimu bora’.

Mengi yatajitokeza na mtayajua waungwana wote wa Tanzania!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam.
Sijakupata vizuri...Mkandala akatae kuyapitisha? Anajipenda? Itabidi ajiulize mara mbilimbili kama alistahili kuwa VC wa UD kabla hajaanza kuiletea zengwe serikali. Analijua hili vizuri na hawezi kujifanya hamnazo!
 
Yani mtoto wake anasoma marekani Tanzania ndio wanawaongezea credit watoto walio feli? kweli hii ndio tanzania. na chuo kikuu tunapeleka mambumbu? lakini wajue kuwa Mungu.
 
huruma kwa wadogo\watoto wetu walimaliza Form4 mwaka jana.
bado hakieleweki, muda unazidi kupotea, gharama znazidi ktk kutatua tatizo.
wkt vijana hao wapo njia panda ktk hali ya SINTOFAHAMU.
 
Tanzania ni kibajaji, kwa njia hii tuangalie sana abiria hatukawii kufunikwa
 
Kwani hawana utaratibu wa kiofisi wa kukaimu nafasi ikiwa mkuu hayupo? na kwani hawana utaratibu wa ukomo wa maamuzi kwa anayekaimu hiyo nafasi? story yako ina haijatoa majibu ya hayo maswali.
 
Jomo kenyatta-nyerere anaongoza maiti,,,,,sijui kama mpaka leo jk bado anaongoza maiti???
 
Nadhani kuna mengi yaliyosemwa ambayo bila shaka hukuyasikia au hutaki kuyatilia maanani. Maelezo yako ni kana kwamba kilichofanywa na NECTA ilikuwa ni maamuzi yao wenyewe.

Utaratibu waliotumia kupanga matokeo ilikuwa ni baada ya michakato iliyoendeshwa na serikali chini ya waziri wa elimu na katibu akiwa Mulugo, na hatimaye wakatoa maagizo rasmi kwa NECTA juu ya utaratibu wa kupanga matokeo.

Sasa cha ajabu watu wale wale waliotoa maagizo ya awali wanakuja na maagizo mapya yanayoashiria kupinga maagizo yao ya awali, kweli hapo utaendelea kutupa lawama kwa NECTA?

Cha ajabu kinachonishangaza, Tume iliyoundwa inaongozwa na mtu ambaye alikuwa mjumbe kwenye kikao kilichoamua kubadilisha utaratibu wa upangaji wa matokeo hayo, leo anakuja na fikra mpya ya kutengua wazo lao la awali. Nadhani haikuwa sahihi Tume kuwa chini ya aliyeshiriki kwenye kutengeneza huo utaratibu
Hujaifahamu hoja yangu! Hata kama serikali na NECTA walikaa na kukubaliana, hoja ya msingi ni kwamba haikuwa sahihi! Katika lugha ya "sikubali sikubali" ni kwamba walichofanya serikali ni kula matapishi yao lakini lugha ya kiungwana, walichofanya serikali ni kukubali udhaifu wao na kukiri kwamba walipotoka na hivyo hawana budi kurudi nyuma! Haingii akilini hata kidogo mnabadilisha GRADING kinyemela wakati watu washafanya mitihani huku hata walimu wenyewe hawafahamu kwamba grading imebadilishwa!Hili jambo linawagusa wanafunzi moja kwa moja na sio NECTA! Ukidai kwamba yaliyosemwa mengi ama sikuyasikia au sikutaka kuyatilia maanani niseme tu kwamba u're wrong; nilichoeleza kinaokana na yaliyosemwa na kuandikwa tangu sakata hili lianze....hii sio post yangu ya kwanza; nd am very sure haitakuwa ya mwisho!
 
Back
Top Bottom