Hoja za Warioba zijibiwe, zisipigwe Rungu!

Dr Adam Francis

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
786
Reaction score
1,315
Kwa waliopata nafasi ya kuyasikiliza mahojiano ya Jaji Joseph Sinde Warioba na mwandishi wa habari nguli, mzee wetu Jenerali Ulimwengu, watakubaliana na mm kuwa hayakuwa mahojiano ya kawaida.

Kwaajili ya kuweka kumbukumbu sawa ni vyema tukakumbuka Joseph Sinde Warioba ni mwanasheria aliyepata kuwa Jaji wa mahakama kuu, mwanasheria mkuu wa serikali, waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na mwenyekiti ya tume ya mabadiliko ya katiba.

Kwa muktadha huo sio mtu ambaye tunaweza kumpuuza na mambo yakaendelea kama yalivyo. Zaidi sana ni uzito wa madai aliyoyatoa katika mahojiano yake hayo. Ni ukweli kuwa mambo aliyoyasema, yasipojibiwa yataacha doa kubwa kwa nchi yetu.

Kwa mfano, Jaji Warioba ana hoji vyombo vya ulinzi na usalama vilikuwa wapi kwa kipindi chote cha miezi sita wakati vikundi vilivyopanga, vilivyoratibu na vilivyofadhili machafuko ya October 29 vikiingia nchini, vikitoa mafunzo na vikigawa hela kuchochea machafuko?

Hoja nyingine ni wasiwasi wake juu ya njia gani zitakazotumiwa na tume ya uchunguzi iliyopendekezwa kuwezesha kubaini muhusika mmoja mmoja wa mauaji ya October 29 ili awajibike kibinafsi? Kwa utaratibu huu, Jaji Warioba anasema mwisho tutarajie kuambiwa waliotekeleza mauaji ya wananchi ni watu wasiojulikana.

Jaji ameenda mbali zaidi kwa kuhoji uhalisia wa idadi ya vifo 518 vilivyoripotiwa na tume akidai watu wengi zaidi waliuawa. Hili si dai dogo, linahitaji kupata ufafanuzi kutoka kwa Jaji Chande na Tume yake.

Kubwa kuliko yote, Jaji anasema matokeo ya uchaguzi wa 2025 ni matokeo bandia yaliyotengenezwa na Tume. Hii ni tuhuma nzito sana, n vyema Tume ya uchaguzi ikafafanua takwimu za matokeo ya uchaguzi ili kukata mzizi wa fitna.

Mwisho ni madai ya ukiukwaji wa haki zake za kiraia ikiwemo kuzuiwa kutumia simu yake, kuzuiwa kushiriki mikutano na makongamano na vitisho vya mara kwa mara. Mambo haya yanazua hofu kwa wananchi ambao kwa namna moja au nyingine watahoji kama waziri mkuu mstaafu anafanyiwa hivi sie akina ndugu wananchi itakuwaje?

Rais Kikwete alituasa kuwa hoja hazipigwi Rungu bali hujibiwa kwa hoja. Mtu mzito kama Jaji Warioba anapotoa shutuma nzito kama hizi kumtukana, kumdhalilisha na kumkebehi haisaidii. Mamlaka husika zinaowajibu wa kujibu na kufafanua shutuma hizi Kwaajili ya mustakabali mwema wa nchi yetu.
 
Zitajibiwa kwa utekaji na uuaji.
Tunatakiwa kuonekana na sio kusikika .
 
Sasa hizo hoja za huyo akili kubwa zitajibiwa na nani pale lumumba??Hao akili zao ndogo kama vile Gerson msigwa ndiyo unatarajia yule ajibu hoja???
 
Kwa waliopata nafasi ya kuyasikiliza mahojiano ya Jaji Joseph Sinde Warioba na mwandishi wa habari nguli, mzee wetu Jenerali Ulimwengu, watakubaliana na mm kuwa hayakuwa mahojiano ya kawaida.

Kwaajili ya kuweka kumbukumbu sawa ni vyema tukakumbuka Joseph Sinde Warioba ni mwanasheria aliyepata kuwa Jaji wa mahakama kuu, mwanasheria mkuu wa serikali, waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na mwenyekiti ya tume ya mabadiliko ya katiba.

Kwa muktadha huo sio mtu ambaye tunaweza kumpuuza na mambo yakaendelea kama yalivyo. Zaidi sana ni uzito wa madai aliyoyatoa katika mahojiano yake hayo. Ni ukweli kuwa mambo aliyoyasema, yasipojibiwa yataacha doa kubwa kwa nchi yetu.

Kwa mfano, Jaji Warioba ana hoji vyombo vya ulinzi na usalama vilikuwa wapi kwa kipindi chote cha miezi sita wakati vikundi vilivyopanga, vilivyoratibu na vilivyofadhili machafuko ya October 29 vikiingia nchini, vikitoa mafunzo na vikigawa hela kuchochea machafuko?

Hoja nyingine ni wasiwasi wake juu ya njia gani zitakazotumiwa na tume ya uchunguzi iliyopendekezwa kuwezesha kubaini muhusika mmoja mmoja wa mauaji ya October 29 ila awajibike kibinafsi? Kwa utaratibu huu, Jaji Warioba anasema mwisho tutarajie kuambiwa waliotekeleza mauaji ya wananchi ni watu wasiojulikana.

Jaji ameenda mbali zaidi kwa kuhoji uhalisia wa idadi ya vifo 518 vilivyoripotiwa na tume akidai watu wengi zaidi waliuawa. Hili si dai dogo, linahitaji kupata ufafanuzi kutoka kwa Jaji Chande na Tume yake.

Kubwa kuliko yote, Jaji anasema matokeo ya uchaguzi wa 2025 ni matokeo bandia yaliyotengenezwa na Tume. Hii ni tuhuma nzito sana, n vyema Tume ya uchaguzi ikafafanua takwimu za matokeo ya uchaguzi ili kukata mzizi wa fitna.

Mwisho ni madai ya ukiukwaji wa haki zake za kiraia ikiwemo kuzuiwa kutumia simu yake, kuzuiwa kushiriki mikutano na makongamano na vitisho vya mara kwa mara. Mambo haya yanazua hofu kwa wananchi ambao kwa namna moja au nyingine watahoji kama waziri mkuu mstaafu anafanyiwa hivi sie akina ndugu wananchi itakuwaje?

Rais Kikwete alituasa kuwa hoja hazipigwi Rungu bali hujibiwa kwa hoja. Mtu mzito kama Jaji Warioba anapotoa shutuma nzito kama hizi kumtukana, kumdhalilisha na kumkebehi haisaidii. Mamlaka husika zinaowajibu wa kujibu na kufafanua shutuma hizi Kwaajili ya mustakabali mwema wa nchi yetu.
warioba ni mzee mwenye chuki za wazi wazi kabisa dhidi ya tume ya jaji chande, lakini zaidi sana ana hasira sana dhidi ya viongozi wa kuu wa serikali sikivu ya CCM, hasa baada ya kua ana puuzwa kulingana na kutokuaminika kwake, lakini pia muendelezo wa uongo ambao ameendelea kuueleza maeneo tofauti tofauti dhidi ya serikali sikivu ya CCM,

kiujumla hana hoja na kwahiyo aendelee kupuuzwa kama ambavyo daima hupuuzwa 🐒
 
Mzee wa watu kakazia tu yanayojulikana dhahiri shahiri, lakini nyie machawa ndo mnaona ni hoja mpya. Facken. Huyo mnaemwita Mama yenu atuachie nchi yetu, na yeye akatumikie jela huko.
 
Akipatikana mwenye akili ya kuzijibu nitonye!
 
Lakini CCM wana Maprofesa na PhD za kutosho, kwanini unadhani hawamuwezi Jaji Warioba?

PhD na uprofesa wa viongozi wa CCM au viongozi wa Serikali, wala usikupotezee muda. Wengi wao ni madokta na maprofesa bandia. Ndiyo maana kuna wakati dokta au profesa wa CCM anatoa kauli mpaka unaona ni aheri mtu aliyeishia form 4.

Haishangazi, kwa sababu wengine wanazipata PhD kwa maelekezo au kwa kutumia hela, wakiwapa watu wawaandalie na kuwafanyia research eti wao wapo busy.

Niliwahi kusimliwa na mzee mmoja ambaye alimfundisha nJakaya alipokuwa UDSM. Akasema kuwa hakuweza kufanya vizuri, alitakiwa kurudia mwaka ili kuona kama atamaliza, cha ajabu ni kwamba alienda chuoni na barua toka ikulu, kuwa kama kiongozi wa vijana wa TANU YOUTH LEAGUE, ana majukumu mengi, hivyo wampe minimum pass ili amalize chuo. Idara wakakaa wakajadiliana, wakampa minimum pass kwenye masomo aliyotakiwa kurudia kuyasoma baada ya kufanya sup, na kufeli. Na hivyo ndivyo alivyomaliza masomo yake UDSM.
 
warioba ni mzee mwenye chuki za wazi wazi kabisa dhidi ya tume ya jaji chande, lakini zaidi sana ana hasira sana dhidi ya viongozi wa kuu wa serikali sikivu ya CCM, hasa baada ya kua ana puuzwa kulingana na kutokuaminika kwake, lakini pia muendelezo wa uongo ambao ameendelea kuueleza maeneo tofauti tofauti dhidi ya serikali sikivu ya CCM,

kiujumla hana hoja na kwahiyo aendelee kupuuzwa kama ambavyo daima hupuuzwa 🐒
Kuhusu Jaji Warioba kuwa na chuki binafsi na viongozi wa chama chetu sidhani kama kuna ukweli.
Warioba kuamini na kusimamia anachokiamini ndio tabia yake. Na kusema ukweli hajaanza leo.
Kwaajili ya kumbukumbu tu, Jaji Warioba alishawahi mbishia, Mwl Nyerere na Hayati Sokoine kuhusu sheria ya uhujumu uchumi kwa hoja kuwa inaenda kinyume na haki za binadamu.
Kwenye katiba mpya kadhalika, msimamo wake ulitofautiana kabisa na ule wa bunge la katiba pamoja na ule wa chama na akaendelea kuamini anachokiamini.
Kwamba shutuma zake ni ukweli au sio ukweli hilo ni jambo linalomuhitaji mwenyewe kuthibitisha. Angalau tunaweza kusemea tu tabia yake.
 
PhD na uprofesa wa viongozi wa CCM au viongozi wa Serikali, wala usikupotezee muda. Wengi wao ni madokta na maprofesa bandia. Ndiyo maana kuna wakati dokta au profesa wa CCM anatoa kauli mpaka unaona ni aheri mtu aliyeishia form 4.

Haishangazi, kwa sababu wengine wanazipata PhD kwa maelekezo au kwa kutumia hela, wakiwapa watu wawaandalie na kuwafanyia research eti wao wapo busy.

Niliwahi kusimliwa na mzee mmoja ambaye alimfundisha nJakaya alipokuwa UDSM. Akasema kuwa hakuweza kufanya vizuri, alitakiwa kurudia mwaka ili kuona kama atamaliza, cha ajabu ni kwamba alienda chuoni na barua toka ikulu, kuwa kama kiongozi wa vijana wa TANU YOUTH LEAGUE, ana majukumu mengi, hivyo wampe minimum pass ili amalize chuo. Idara wakakaa wakajadiliana, wakampa minimum pass kwenye masomo aliyotakiwa kurudia kuyasoma baada ya kufanya sup, na kufeli. Na hivyo ndivyo alivyomaliza masomo yake UDSM.
Hizi tuhuma unazozitoa ni nzito sana comrade. Ingekuwa vizuri zisithibitishwe kwa hear say.
 
Akipatikana mwenye akili ya kuzijibu nitonye!
Huyu hapa Tlaatlaah eti ndo akili kubwa ya Chawa wa Lumumba wote eti na majibu yake ni haya (msome👇tena?

"...warioba ni mzee mwenye chuki za wazi wazi kabisa dhidi ya tume ya jaji chande, lakini zaidi sana ana hasira sana dhidi ya viongozi wa kuu wa serikali sikivu ya CCM, hasa baada ya kua ana puuzwa kulingana na kutokuaminika kwake, lakini pia muendelezo wa uongo ambao ameendelea kuueleza maeneo tofauti tofauti dhidi ya serikali sikivu ya CCM

kiujumla hana hoja na kwahiyo aendelee kupuuzwa kama ambavyo daima hupuuzwa 🐒..."

Hii Chawa Tlaatlaah haijui kabisa kunyamaza Ili kuficha ujinga wake. Usishangae kuwa tayari hata kukana jinsia yake!!

Hizi ndo akili kubwa za CCM Lumumba B7000 kwa siku..!!
 
Back
Top Bottom