Sarafu ya sh 500 haina ubora!

Sarafu ya sh 500 haina ubora!

anakuwasha nini!? kwani yeye ndio fundi wa kutengeneza hizo fedha!!? Lawama za kitoto hizi.

mbona unaweweseka? wewe unadhani ni nani wa kulaumiwa wakati yeye ndiye kiongozi mkuu wa nchi? unadhani BoT walifyatua hizo sarafu feki bila kumshirikisha mkuu wa nchi?
 
Hizi sarafu huwa nashindwa kuelewa ubora wake, sarafu ya shilingi 200 zinaisha kama soli! Mpaka mtu unaona hata noma kumpa mwenye duka...
 
Km issue ilikuwa ni uchakavu wa noti za tshs 500/= kwa nn sasa BOT wasingetengeneza noti nyingine za thamani hiyo zenye ubora zaidi ya hizi noti zilizopo ktk mzunguko?
Navyojua mm ni kuwa nchi ikiwa na sarafu yenye thamani kubwa,basi uchumi wake upo mashakani.
Viongozi wa bongo espcly ma-CCM ni mafisadi ya kutosha.
 
Hii nchi mpaka tunyonge mtu hadharani ndo watajifunza na kuacha upuuzi!!!
 
99%mambo ni ya wizi tu mtu asipoiba hajawa Mjanja.
 
KWA TREND HII YA BOT; UCHUMI WA TANZANIA ULALE MAHALI PEMA PEPONI.

Siungi mkono hoja ya Benki kuu (BOT) kufuta noti ya Sh.500/= na kuifanya sarafu. Huu ni wendawazimu mkubwa katika sekta ya uchumi "the most unpleasant economic decision" kwa sababu zifuatazo;

MOSI; fedha yoyote inapobadilishwa kuwa sarafu kutoka noti ni kuishusha thamani. Hii ni kwa sababu kiuchumi inabadilika matumizi na kuanza kutumika zaidi ktk sekta ya uchumi mdogo km wa wauza njugu mtaani, mama lishe, na maeneo mengine yasiyozalisha sana kiuchumi (less productive sector).

Maeneo yenye uzalishaji mkubwa (lead productive sector) yatashindwa kuitumia fedha hii kwa kuwa tu ni ya sarafu. Kw mfano kuanzia sasa haitakua rahisi kukuta sarafu hizi za 500/= maeneo kama Airport, Migodini au Supermarket.

Hiki ni kiashiria cha kushuka kwa thamani kwa fedha hiyo. (Indicator for currency devaluation).

Hivi hatujiulizi kwanini Marekani hadi dollar moja ni ya noti sisi 500/= tunaweka sarafu?? Dollar moja ina single digit lakini ipo kwenye noti, sisi tunalazimisha kuweka 500 kwny sarafu wakati ina tripple digit. Tunaforce Galloping inflation.

PILI; unapotengeneza sarafu ya pesa kubwa ina maana sarafu zinapotea na kujiondoa ktk mzunguko wa fedha. So tutegemee siku si nyingi sarafu za sh.100/= na sh 200/= hazitakuwepo tena mtaani.

Ikifikia hatua hii ujue nchi imeanza kuyumba kiuchumi na mfumko wa bei umevuka kiwango cha kawaida (extention from Moderate inflation to Galloping inflation).

Wenzetu Kenya hadi sarafu ya sh.10 inatumika. Ukienda Nairobi, Mombasa au maeneo mengine ya Kenya utata watoto wakinunua madafu, ice cream au matunda kwa sh.10.

Hapa kwetu sarafu ya sh.10 ilikufa na Nyerere. Ya sh.5 ikaenda na Sokoine. Ya sh.20 na 50 zimemfuata Kawawa. Sasa benki kuu wanalazimisha sarafu ya sh.100 na ya sh.200 zikamfuate Karume mahali pema peponi. Noti ya sh.1,000/= nayo inakaribia kwenda ahera maana BOT wameleta sarafu ya sh.1,500/=.

TATU; BOT kuwa wametoa hoja mufilisi kuwa wamefuta noti ya Sh.500/= na kuireplace kwa sarafu baada ya kugundua noti hiyo inachakaa haraka sn na inadumu kwa muda mfupi mno kwenye mzunguko.

Hoja hii ni mufilisi kwa sababu solution ya noti kuchakaa mapema si kureplace sarafu bali ni kuimarisha noti hiyo kwa kuitengeneza kwa material imara zaidi.

Hivi noti ya 10,000/= nayo ikichakaa mapema BOT wataleta sarafu instead?? Huu ni wendawazimu.

Mojawapo ya sifa za fedha imara ni uwezo wa kukaa kwny mzunguko muda mrefu (durability). Sasa fedha inapopoteza durability dawa sio kubadili muundo wake (changing of currency format is not a solution for impermanency)

Lakini hata hivyo BOT wameonesha hawakufanya utafiti wa kina kabla ya kuleta sarafu ya 500/=. Wanasema zinachakaa haraka ukilinganisha na noti nyingine. Hii ni hoja dhaifu sana kutolewa na mtu anayejiita Profesa wa uchumi Benno Ndullu.

Yani Profesa Ndulu anataka noti ya 500/= na ya 10,000/= zidumu kwenye mzunguko kwa muda sawa?? Yani 10,000/= ikidumu miaka miwili, 500/= nayo idumu miaka miwili. Bila shaka hapo ndo ataona noti ya 500/= haichakai haraka.

Hii ni "akili ndogo kujaribu kutawala akili kubwa". Noti ya 500 haiwezi kulinganishwa na noti nyingine kwenye mzunguko kwa sababu ina frequent circulation. Yani ktk uchumi noti yenye thamani ndogo huwa inazunguka zaidi kuliko ya thamani kubwa.

Hivyo noti ya 500/= inaweza kupita kwenye mikono ya watu 2000 ndani ya mwezi mmoja wakati ile ya 10,000/= imepita kwenye mikono 20 tu kwa mwezi.

Hii ni kwa sababu mzunguko wa noti hizi hutegemea matumizi. Ya 500/= itazunguka kwny daladala, wauza magazeti, vijiwe vya kahawa etc, wakati ile ya 10,000/= itazunguka Supermarket, Airport, hoteli kubwakubwa etc.

Hivyo ni dhahiri kuwa noti ya 500/= itaanza kuchakaa mapema kuliko noti ya 10,000/= au ya 5,000/= au noti nyinhine kubwa. Sasa cha ajabu Profesa Beno Ndulu hajui hili na badala yake ameona solution ni kuleta sarafu. Aibu gani hii kwa mtu anayejiita Profesa wa uchumi kushindwa kujua vitu common km hivi ambavyo hata muuza machungwa wa Keko anavijua??
 
Lengo la kubadilisha noti ya shilingi 500 kuifanya sarafu ilikuwa ni kutokana na noti hizo kuchakaa mapema kutokana na mzunguko mkubwa. Sasa kama hii sarafu ya 500 ambayo tunategemea pia itakuwa na mzunguko mkubwa imetengenezwa kwa viwango duni kama ulivyoandika basi itachakaa mapema zaidi ya ile noti ya 500. Sasa hapo BOT watakuwa wamefanya nini cha maana?



Nasubiria majibu ya vituko toka BOT. Usishangae ukaambiwa kuwa kupiga kutu kwa hiyo sarafu mpya ya jero ni moja ya alama ya ubora kwani nakumbuka wakati BOT walipobadili noti na watu kulalamika kuwa noti mpya zilikuwa zinachakaa mapema na zinatoa rangi na kuchafua walleti na mifuko yao Gavana alisema kuwa kutoka rangi kwa hizo noti ni moja ya alama ya ubora!

Nime ikumbuka mikeka ya mzee BW. mkapa kulikuwa hakuna sababu ya kuitoa
 
Huu ni Uzushi mtupu.
Kila Sarafu ikiingia watu lazima watajifanya wao wataalam saana.
Zilivyoingia Shilingi mia watu walisema haya haya ya ubora.leo zinapeta.
Shilingi kumi hadi leo zipo na mfumo huo huo.
Haya maneno tumeyazoea.
 
Huu ni Uzushi mtupu.
Kila Sarafu ikiingia watu lazima watajifanya wao wataalam saana.
Zilivyoingia Shilingi mia watu walisema haya haya ya ubora.leo zinapeta.
Shilingi kumi hadi leo zipo na mfumo huo huo.
Haya maneno tumeyazoea.

mkuu, usiropoke ovyo. sarafu za senti 50, shilingi 1, 5, 10 na 20 zimetengenezwa kwa madini ya fedha. shilingi 100 na 200 zimetengenezwa kwa madini ya bati. Haya madini hayapambani na oxygen wala maji. Sasa iweje safari hii watumie chuma kama sio hujuma za makusudi?

Na hakuna mtu aliyewahi kulalamikia ubora wa sarafu za zamani. Usiropoke bure kama huna ushahidi.

Mimi sijawahi kuona sarafu ikitengenezwa kwa madini ya chuma. Haya maajabu yanawezekana Tanzania tu, nchi ya kusadikika!
 
Nime ikumbuka mikeka ya mzee BW. mkapa kulikuwa hakuna sababu ya kuitoa

Yeah! Mbona ile mikeka ya mkapa ilikuwa haichakai ovyo? Ni bora basi wangeturudishia ile mikeka ya Mkapa kuliko kututengenezea hizi kutu.
 
Si walituambiA kuwa wanatuletea golden coin??
 
Mlizipata wapi sarafu hizo? Mbona bado kutolewa na mmeanza kufoka na kutoa mapovu?

unaambiwa sarafu imetengenezwa kwa madini ya CHUMA husikii? kama hujui jambo ni bora ukae kimya?

chuma hupambana na oksijeni katika uwepo wa unyevu na kutengeneza kutu na chuma kikishapata kutu hakifai kwa matumizi yoyote. wewe hilo hulioni? au ushawahi kusikia sarafu za nchi yeyote zimetengenezwa kwa chuma? mkuu, utachekwa!
 
Back
Top Bottom