Sarafu Moja E.A.C : Ripoti Yatoka, Mabishano Makali Yazuka

Naonavyo mimi, sarafu 1 kwa EAC ni mapema mno... Tuna mengi ya kurekebisha kabla hatujafika huko. Pia, bado hizi nchi wanachama hatuaminiani, tunaishi kwa kuviziana na kwa mashaka mno, sarafu 1 inaitaji uaminifu sana, sasa kwa ujanja ujanja wa wakenya, tamaa ya m7 na kagame, hatuwezi tengeneza strong monetary union. Hili swala tungesubili kwanza. Afteral, mbona tunakuwa na haraka mno??

Hawa wazee wanataka kuiona sarafu moja kabla hawajafa so , wana harakisha
 
Hawa wazee wanataka kuiona sarafu moja kabla hawajafa so , wana harakisha

Hata mimi nina wasiwasi bado na hii jumuiya kwanini wanawahi sana kuwa na sarafu 1? Nadhani kweli muda wa sarafu 1 ni bado sana wangetazama mambo mengine,
Pili hawa wawakilishi wetu wanatakiwa wawe makini sana hapa,maana hawa wakenya mimi siwaamini kabisa,nashkuru kuwa tz imekataa ardhi yake kuingizwa kwenye jumuiya,maana hawa wakenya wangehamia tz wote kwa sababu ardhi kwao hakuna, wawakilishi wa tz kuweni makini sana na hawa kenya na rwanda,halafu hivi hii jumuiya haitoa adhabu kwa wanachama wanao sapoti machafuko kama uganda na rwanda?
Sarafu 1 kwanza tungefanya kura ya maoni kabla ya kuipitisha vinginevyo hapa tutakuja kuvuruga uchumi wetu mpaka tutajuta
 
Hii ni jumuiya ya waafrika wa mashariki au ni jumuia ya US na hawa "wakoloni" wanaorudi kwa mlango wa nyuma?

Je waafrika mashariki ndio wameunda hii jumuiya au tumeundiwa hii jumuiya kutimiza malengo ya wenye mali?

Wafadhili wakuu ni GIZ, shirika la maendeleo la ujerumani.
 
Hata mimi nina wasiwasi bado na hii jumuiya kwanini wanawahi sana kuwa na sarafu 1? Nadhani kweli muda wa sarafu 1 ni bado sana wangetazama mambo mengine,
Pili hawa wawakilishi wetu wanatakiwa wawe makini sana hapa,maana hawa wakenya mimi siwaamini kabisa,nashkuru kuwa tz imekataa ardhi yake kuingizwa kwenye jumuiya,maana hawa wakenya wangehamia tz wote kwa sababu ardhi kwao hakuna, wawakilishi wa tz kuweni makini sana na hawa kenya na rwanda,halafu hivi hii jumuiya haitoa adhabu kwa wanachama wanao sapoti machafuko kama uganda na rwanda?
Sarafu 1 kwanza tungefanya kura ya maoni kabla ya kuipitisha vinginevyo hapa tutakuja kuvuruga uchumi wetu mpaka tutajuta

Morons, whats so special about Tanzania that Kenyans are waiting to troop in??????? No wonder every Kenyan gets a ban herei f they cannot see this type of hate speech but are quick to judge the rejoinders.
 
Kazi ya ukusanyaji documents ndio naimalizia. Ripoti iliyosainiwa sijaipata, nimeipata ambayo haijasainiwa. Katika kusaini kauli ya Msole(Signatory wa Tanzania) yamshtua Mutua(Signatory wa Kenya)asimama kabla ya kumalizia kusaini......vituko vingine havikupaswa kuwepo.
 
Wafadhili wakuu ni GIZ, shirika la maendeleo la ujerumani.

I feel pity kuona ishu ya uhisani..hawa jamaa sio wajomba zetu ni lazima wana lengo nyuma ya pazia.Tufike mahala tukatae kutegemea 'ufadhili' hata kwenye mambo mazito kama haya.
 
Mabishano makali yamezuka katika mjadala unaoendelea Katika Makao Makuu ya Jumuiya Ya Afrika Mashariki Huko Arusha katiya Kenya na Rwanda. Hoja ikiwa ni wao wanataka kuwe na sarafu moja ya jumuiya, lakini waendelee kubaki na sarafu zao kama kawaida huku Rwanda ikisisitiza USD iwe ndio hela ya jumuiya na kila mmoja abaki na sarafu yake. majadiliano yatakayodumu kwa siku sita mfululizo yanalenga kuikomboa Afrika Mashariki kiuchumi. Tofauti ya mikopo toka IMF kwa nchi mojamoja jinsi ya kuulipa mkopo huo kwa pamoja, ni moja kati ya masuala yaliyojadiliwa.

Sudan ya Kusini ambaye mara zote yeye huwa mgeni mwalikwa na "Mtazamaji" tu (Observer) safari hii kaambiwa asubiri kwanza hadi wao wakubaliane mambo ya msingi. Kenya imetunisha misuli baada ya Tanzania kuitunishia misuli kuhusu suala la ardhi. hivi punde nita-attach nakala ya ripoti yote na mchakato mzima jinsi ulivyokuwa.

Siku ya Tano leo hamna attachments huyu jamaa feki
 
Siku ya Tano leo hamna attachments huyu jamaa feki
Mpinga Shetani naomba kuwa mvumilivu na naomba nipe siku ya mwisho leo, wewe na wanajamii wote, Kesho na-kamilisha....Nimeshazi-scan na kuzituma kwenye email yangu tayari kwa ku-attach...vumilia kwani si unajua majukumu ni mengi sana, si JF tu muda wote. Naomba vumilia ndugu yangu.
 
Thanda hiyo documents iko wapi ss
Nimei-scan najaribu kuiattach naona haikubali. Niliihifadhi katika TIFF wataalamu wakaniambia inabidi iwe katika PDF, asante kwa kunikumbusha...acha nim-consult Ben (Graphic Designer and IT Personell wetu hapa ili anisaidie.
 
Ungetumia Adobe prof. uiconvert toka tiff kwenda pdf is . By using Adobe prof. is just a simple task to convert from TIFF to Adobe. Just only right click on that TIFF doc and choose "convert to pdf" then just upload here jamvini
 
Back
Top Bottom