Sanduku la Agano liko wapi?

Hoja ni kwamba sanduku lilikuwa na utukufu wa Mungu na waliokuwa wanaruhusiwa kulishika ni wana wa lawi hakuna mtu mwingine yeyote aliyeruhusiwa kulishika wala kuligusa, aliyethubutu kulishika/kuligusa bila kuruhusiwa alikufa hapohapo.

Je baadae utukufu wa Mungu uliondolewa na kila mtu akaruhusiwa kulishika/kuligusa na kulibeba ndio maana likaweza kubebwa na mtu yeyote asiyekuwa mulawi na kufichwa mahali pasipojulikana pasipokupata madhara yoyote ya kufa kama ilivyokuwa hapo awali?.

Isije ikawa sanduku la Bwana lilifichwa na Mungu mwenyewe kama alivyoificha busitani ya edeni kwa ajili ya usalama wa mwanadamu ili wasiendelee kufa kwa kuwa amri ya Mungu ilikuwa ni wana wa lawi pekee ndio walioruhusiwa kuligusa sanduku la Bwana, tofauti na hapo aliyethubutu kuligusa kama hakuwa mulawi hakuna adhabu nyingine aliopewa zaidi ya kifo.

Na hakuna mahali popote pale tunapoambiwa Kama Mungu alibadilisha amri yake ya kutaka wana wa lawi ndio watu pekee wanaoruhusiwa kuligusa sanduku la Bwana, na kuruhusu kila mtu yeyote aliguse pasipo kupata madhara yoyote.
 
Kipindi nilivyokuwa nasoma mchungaji wetu alituambia ipo ethiopia sijui kanisa la orthodox ....niko tayari kukosolewa maana ilikuwa ni mda kidogo hata baadhi ya details nimesahau
lilifikaje ethiopia? kuna connection gani kati ya utawala wa Babylon na wa-ethiopia ? yawezekana hawa wa-ethiopia ndiyo wakawa wana halisi wa Israel na wengi wao walikuwa utumwani Misri

Mawasli ni mengi....
 
Na: Alex E. Bubelwa.

KUHUSU LILIKO SANDUKU LA AGANO!
Sanduku la Agano lilitengenezwa na fundi aliyeitwa Bezaleli mwana wa Huri kwa maelekezo toka kwa Mungu kama alivyomwagiza Musa, ilikuwa ni kama mwaka mmoja tangu walivyokuwa wametoka Misri. Kuhusu ukubwa wake na jinsi kilichotengenezwa tafadhali soma mwenyewe katika (Kutoka 25:10-22).

Baada ya kutengeneza, vitu vilivyokuwa vimewekwa hapo mwanzo ni kama vilivyoorodheshwa kwenye (Waebrania 9:4)

"..... na sanduku la agano lililofunikwa kwa dhahabu pande zote, mlimokuwa na kopo la dhahabu lenye ile mana, na ile fimbo ya Haruni iliyochipuka, na vile vibao vya agano;.." (soma pia Kutoka 16:33).

Sanduku la Agano lilikuwa ni ishara ya uwepo wa Mungu katikati ya wana wa Israeli. Lilikuwa linahifadhiwa katika hema maalum ilotengenezwa kwa ajili yake, wakati Israeli wakiwa jangwani ni katika hema hiyo Musa alikuwa anakwenda kuongea na Mungu.
Sanduku hili lilikuwa lina utisho mkuu mno, haikuruhusiwa mtu asiyekuwa kuhani kuligusa au kulikaribia, kama angelikaribia angekufa. ( 1Sam 6:19). Waisraeli wakati wanaingia nchi yao ambayo wakati ule iliitwa Kanaani, waliobeba hilo sanduku walipofika mto Yordani maji yalijitenga wakavuka kwa miguu.

Mwaka 967KK Sulemani alipojenga Hekalu, Sanduku la Agano lihamishiwa humo, lakini FIMBO YA MUSA na KOPO LA DHAHABU LENYE MANA (chakula ambacho Mungu aliwalisha Israeli jangwani) havikuwemo, zilikuwemo tu mbao mbili za mawe zilizoandikwa amri kumi. Ona maandiko yanavyoonesha:
(1 Wafalme 8:9)

"Hamkuwa na kitu ndani ya sanduku, ila zile mbao mbili za mawe ambazo Musa aliziweka ndani huko Horebu, BWANA alipofanya agano na wana wa Israeli, hapo walipotoka katika nchi ya Misri."
Hivi kopo lenye mana na fimbo ya Haruni ile ilogeuka nyoka na pia kuchipua vilienda wapi? Katika Biblia haijaelezewa popote, ila inasemekana karibu mwaka 1100KK enzi za kuhani Eli, Israeli walipomtenda Mungu dhambi akawaacha na hilo Sanduku la Agano likaporwa na Wafilisti mpaka Ashdodi, wakakaa nalo kwa muda wa miezi saba, ni kwa wakati huo vitu hivyo viliibiwa na hao Wafilisti! (1Sam 6:1).

Mfalme Yosia alitawala Yudea mwaka 641-609KK, wakati wa utawala wake ikiwa imebaki miaka zaidi ya 40 kabla Nebukadreza kuteketeza Hekalu lililojengwa na Sulemani, nabii Yeremia alitoa unabii kuhusu sanduku la Agano, kwamba utakuja wakati ambapo Wayahudi hawatakuwa nalo sanduku la Agano na wala hwatalitaja! Ona unabii kwa kinywa cha Yeremia :
(Yeremia 3:16)

".... siku zile hawatasema tena, Sanduku la agano la BWANA; wala halitaingia moyoni; wala hawatalikumbuka, wala hawatalizuru, wala hayatafanyika hayo tena."

Mwaka 586KK wababeli walipigana na Yuda, Wayahudi wakashindwa vita, huku wapiganaji na raia wasiopungua laki moja wakauliwa na waliosalia wakachukuliwa hadi Babeli, mali za Hekalu zikaporwa na hekalu lenyewe likateketezwa kwa moto.

Baada ya Hekalu kuteketezwa hatima ya Sanduku la Agano haikujulikana, na wala halikubebwa na Wababeli!
Baada ya miaka 480 kupita tangu Hekalu la Sulemani lilipoharibiwa, mwaka wa 100KK kitabu cha Wamakabayo (kimojawapo kati ya vitabu 7 vya deuterokanoni) kiliandikwa. Katika 2Wamakabayo 2:4-10 inaonesha kabla ya Wababeli kuishambulia Yerusalemu, Mungu alimwamuru nabii Yeremia alichukue Sanduku la Agano aende nalo mpaka mlima Nebo, alifiche kwenye pango.

Mlima Nebo uko katika nchi ambayo kwa sasa inaitwa Jordan, kuna umbali wa maili 29 tokea Mashariki ya mji wa Yerusalemu. Ni katika mlima huo Mungu alimwambia Musa apande aangalie nchi ambayo anawapa wana wa Israeli, na ndiko alikofia na mwili wake kuzikwa na Mungu mwenyewe, haukuonwa tena.

Ilikuwa ni kama mwaka 96BK, kwa mara ya mwisho Sanduku la Agano lilionekana kwa mara ya mwisho, aliyeliona ni Yohana mwana wa Zebedayo, wakati huo alikuwa kisiwani Patmo, miongoni mwa mambo aliyofunuliwa ni pamoja na sanduku la Agano ambalo aliliona likiwa ndani ya Hekalu la Mbinguni (Ufunuo 11:19).
 
- Sanduku hilo lilikuwa ni kama box la mbao lililotengenezwa na aina moja ya mbao inayoitwa (acacia wood) ; kwahiyo sanduku lilikua la kawaida tu
- Uwepo wa Mungu haukuwepo ndani ya sanduku bali ulikuwa juu yake katikati ya hao makerubi. ; ila Mungu aliweka nguvu yake(nuru)


kwasababu katika list ya vitu walivyovichukua sanduku la agano halikutajwa. ; Kwakua Mungu ni muweza wa yote
je? kama aliiondoa nuru yake juu ya sanduku na hizo sacred Symbols akafanya ikawa kitu tofauti?

hakuna mwanadamu anionaye na akaishi" Kutoka 33 : 20
- Sanduku hili lilikuwa likibebwa na wana wa Walawi pekeyake hakuna mwingine aliyeruhusiwa kulishika, yeyote -aliyedhubutu kulishika pasiporuhusiwa alikufa hapo hapo; 🙄🙄🙄

Mi naona kama tunauliza majibu
Marko 4:9 Kisha Yesu akasema, “Mwenye masikio ya kusikia, na asikie.”
 
Kwahiyo umeshusha nyuzi baada ya kumtazama Jamal kule Wasafi

Anyway kama alivyosema yule Mchunguzi wa kiyahudi

Sanduku lipo Makka 😂😂 nadhani pointi uliziskia pale ,

Tumsubiri Masih tu Yesu mtoto wa Maryam Aje Aseme sanduku Liko wapi
wala mimi sio mfatiliaji wa huyo jamaa, HOJA KWAMBA LIPO MAKKA NI UONGO MKUBWA.... makka lilifikaje kwa mfano...

Ukifatilia vzr utagundua LIMEPOTEA KIPINDI CHA yosia hadi kwa kina YEREMIA hapo....

kuhusu makka ni uzushi mkubwa usio na ushahidi au dalili zozote... kwanza jiulize lilifikaje makka,
 
Hoja ni kwamba sanduku lilikuwa na utukufu wa Mungu na waliokuwa wanaruhusiwa kulishika ni wana wa lawi hakuna mtu mwingine yeyote aliyeruhusiwa kulishika wala kuligusa, aliyethubutu kulishika/kuligusa bila kuruhusiwa alikufa hapohapo.

Je baadae utukufu wa Mungu uliondolewa na kila mtu akaruhusiwa kulishika/kuligusa na kulibeba ndio maana likaweza kubebwa na mtu yeyote asiyekuwa mulawi na kufichwa mahali pasipojulikana pasipokupata madhara yoyote ya kufa kama ilivyokuwa hapo awali?.

Isije ikawa sanduku la Bwana lilifichwa na Mungu mwenyewe kama alivyoificha busitani ya edeni kwa ajili ya usalama wa mwanadamu ili wasiendelee kufa kwa kuwa amri ya Mungu ilikuwa ni wana wa lawi pekee ndio walioruhusiwa kuligusa sanduku la Bwana, tofauti na hapo aliyethubutu kuligusa kama hakuwa mulawi hakuna adhabu nyingine aliopewa zaidi ya kifo.

Na hakuna mahali popote pale tunapoambiwa Kama Mungu alibadilisha amri yake ya kutaka wana wa lawi ndio watu pekee wanaoruhusiwa kuligusa sanduku la Bwana, na kuruhusu kila mtu yeyote aliguse pasipo kupata madhara yoyote.
mkuu ipo hivi israel waalipokuwa wanaasi MUNGU alikuwa anawaacha wanapigwa , na wapagani wanalibeba sanduku hawadhuriki


soma 1 SAMWELI KUANZIA SURA YA 2 LILIWAHI KUCHUKULIWA NA WAFILIST WAKALIPELEKA KWA mungu dagoni, baadae liliwaua wakiarirudisha
 
mkuu ipo hivi israel waalipokuwa wanaasi MUNGU alikuwa anawaacha wanapigwa , na wapagani wanalibeba sanduku hawadhuriki


soma 1 SAMWELI KUANZIA SURA YA 2 LILIWAHI KUCHUKULIWA NA WAFILIST WAKALIPELEKA KWA mungu dagoni, baadae liliwaua wakiarirudisha
Mtoa post uko vizuri unaandika ulichojifunza na kukielewa ukikupendeza nitakuomba tu share hoja Fulani inbox kuhusu sanduku hili Sina jawabu la uhakika
 
Patakatifu pa Mbinguni
Kuna nyumba mbinguni imejengwa,
Hekalu la Mungu aliye hai,
Maskani ya kweli, ambapo hatia
Huoshwa na damu ya thamani.
Muda mrefu tangu, Kuhani wetu Mkuu aliingia hapo,
Nani anajua udhaifu wa sura yetu,
Nani anapenda, kusikia sala ya watu wake,
Na kumtolea Mungu wetu vivyo hivyo.
Huduma ya kila siku aliyobeba,
Mpaka kumalizika siku za unabii;
Kisha akafungua mlango wa ndani,
Ili kuhalalisha mahali patakatifu.
Mbele ya sanduku la amri kumi,
Ambapo kiti cha rehema kimewekwa,
Akiwasilisha damu yake mwenyewe, anasimama,
Mpaka dhambi za Israeli zote zimefutwa.

- R. F. Cottrell.
 
Sanduku lilikuwa kielelezo kikuu cha patakatifu pote. Sheria iliyovunjika iliyomo ndani ya sanduku ilikuwa sababu pekee ya huduma zote za dhabihu, za kawaida na za mfano.


Wakati Bwana alitoa maelekezo ya kutengeneza patakatifu, maagizo yake ya kwanza yalikuwa "Watafanya sanduku la mti wa mshita; urefu wake dhiraa mbili na nusu, na upana wa dhiraa moja na nusu urefu wake, na dhiraa moja na nusu. ” 1 Ilifunikwa ndani na nje na safi
dhahabu, na taji ya dhahabu kuzunguka juu.

Capture 12.PNG
 
wala mimi sio mfatiliaji wa huyo jamaa, HOJA KWAMBA LIPO MAKKA NI UONGO MKUBWA.... makka lilifikaje kwa mfano...

Ukifatilia vzr utagundua LIMEPOTEA KIPINDI CHA yosia hadi kwa kina YEREMIA hapo....

kuhusu makka ni uzushi mkubwa usio na ushahidi au dalili zozote... kwanza jiulize lilifikaje makka,
lililokua Makka sio hili la agano ni lile la malaika jibril alilompatia Mtume.. na lilionekana mwaka 2015 wakati wa upanuzi wa msikiti ndipo viongozi wa kanisa la orthodox wakalifuata kwa escot ya meli za Mrusi mpaka kwenye Bara barafu la antactica.
 
Kuna Documentary niliangalia ya BBC/aljazera sina uhakika,wanasema lipo Ethiopia, kuna hekalu Fulani limewekwa huko ndani na huko anayeruhusiwa kuliona na kulilinda ni mtu mmoja tu na Mara nyingi hatoki nje.

Nje ya Hekalu hilo lina ulinzi mkali sana na hata mwandishi mwenyewe kwanza ilibidi apate ruhusa ya kufika huko na hata alipofika aliongea na mtu mmoja tu aliyekuwa nje ndio akamweleza hayo yite na wala hakuruhusiwa kusogea karibu na uzio wa Hekalu.
Mimi pia nimeona documentary kama hiyo. Inasemekana liko Ethiopia kwenye kanisa moja dogo la kale. Pembeni yake Haile Sellasie alijenga kanisa lingine kubwa.

Anayeingia kwenye chumba lilipo hilo sanduku ni mtu mmoja maalum. Akishachaguliwa mtu wa kuingia kwenye hicho chumba huwa haruhusiwi tena kutoka hekaluni kwenda uraiani mpaka anakufa, na pia haruhusiwi kuongelea details za hilo sanduku.

Mtu mwingine atachaguliwa pale anapofariki huyo anayelitunza au anayelitunza akiwa hawezi tena kiafya. Watu wote waliokwisha fanya hiyo kazi hupata matatizo ya macho kutoona
vizuri mara baada ya kuanza hiyo kazi.

Ngoja niitafute hiyo documentary niitazame tena, very interesting. I will share the link or upload it kwa jinsi nitakavyoipata.
 
Mimi pia nimeona documentary kama hiyo. Inasemekana liko Ethiopia kwenye kanisa moja dogo la kale. Pembeni yake Haile Sellasie alijenga kanisa lingine kubwa. Anayeingia kwenye chumba lilipo hilo sanduku ni mtu mmoja maalum. Akishachaguliwa mtu wa kuingia kwenye hicho chumba huwa haruhusiwi tena kutoka hekaluni kwenda uraiani mpaka anakufa, na pia haruhusiwi kuongelea details za hilo sanduku. Mtu mwingine atachaguliwa pale anapofariki huyo anayelitunza au anayelitunza akiwa hawezi tena kiafya. Watu wote waliokwisha fanya hiyo kazi hupata matatizo ya macho kutoona vizuri mara baada ya kuanza hiyo kazi.
Ngoja niitafute hiyo documentary niitazame tena, very interesting. I will share the link or upload it kwa jinsi nitakavyoipata.

Hapa kuna interesting story (ya 2021, sio zamani) kuhusu waethiopia wanavyopigana kulilinda hili sanduku SOMA HAPA
Umeeleza vema ukiipata tuwekee mkuu
 
Back
Top Bottom