Sanaa ya kifo

Samahani mshana Jr swali langu litagusia na imani kidogo.Umesema kifo ni kufaulu mtihani,m/Mungu anasema katika quran "kila nafsi itaonja umati" je m/Mungu ndiye aliyetunga mtihani huu?mauti yatawajia ghafla alikuwa hawajajiandaa je hayo mandalizi ni yapi? Nijibu hayo tuendelee
 
Kwa muktadha wa shule za elimu dunia kuna ratiba za mitihani na majaribio zinazojulikana! Halafu kuna ile ya kushtukiza...!
Vyovyote iwavyo hakuna ajuaye ni maswali gani yatakuwepo na atafaulu kwa kiwango gani. ..maandalizi tuyafanyayo ni ya msingi na ya jumla tu
 
Kuna mambo ambayo lazima upate kuyafahamu:
1. Mwanadamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu ( Mwanzo1: 26 ) " Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba". Kuumbwa kwa Mfano wa Mungu ni heshima kubwa sana, Hivyo kusema kuwa mwanadamu ni mpumbavu tu na hana chembe ya uelewa ni kudhalilisha utu wa mwanadamu
2. Kifo ni matokeo ya uasi wa mwanadamu kwa Mungu.Mungu alimuumba mwanadamu akiwa kamili, ila alipoasi kwa kula tunda alilokatazwa, ndipo kifo kikawa ni laana kwa huyu mwanadamu na hadi leo tunaona matokeo yake.
3. Wafu hawajui neno lolote, Mhubiri 9:5 " kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote..." ila wanasubiri hukumu ya mwisho. Hapo atakapo kuja Yesu Kristo atawafufua wafu na pamoja walio hai ili wapate hukumu kila mmoja kulingana na matendo yake. 1 Wathesalonike 4:16-
 
umefafanua vizuri sana kijana
 
Hebu soma ulichoandika hapo namba tatu kwamba wafu hawajui lolote.....lakini wanasubiria hukumu ya mwisho....!
Biblia takatifu ni neno linaloishi halipaswi kusoma kama kitabu cha hekaya
Ni sahihi kabisa wafu hawajui lolote kwakuwa ule ni mwili tu usiokuwa na ufahamu wowote
Tunapozungumzia ishu nzima ya wafu ni roho yake ambayo hiyo ndio server ya kila kitu na haifi milele
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…