Samwel Sitta kulipuka Jumatatu!

Samwel Sitta kulipuka Jumatatu!

Greenwhich

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
1,337
Reaction score
968
Spika wa zamani Samwel Sitta anatarajiwa kutoa ya moyoni siku ya Jumatatu kuhusu kinachoendelea ndani ya CCM.

Taarifa kutoka watu wa karibu na kiongozi huyo aliyejipambanua kama mpiganaji wa vita dhidi ya ufisadi zinaeleza atazungumzia hali halisi iliyopo ndani ya CCM na huenda akatangaza vita zaidi dhidi ya ufisadi ndani ya chama hicho.

Waziri huyo wa Afrika Mashariki anasifika kama mtu asiyemumunya maneno na huenda akawasha moto mkubwa ndani ya chama hicho atakapozungumza.

Kwa sasa ndani ya CCM kuna mvurugano mkubwa kutokana na vita ya madaraka ambapo kwa wiki moja makada watano katika makundi mawili yanayoparurana wametuhumiana na kushambuliana mbele ya vyombo vya habari huku kila kundi likitumia kila silaha kushambulia lingine.Makada hao ni John Malecela,Paul Makonda,Richard Kyabo,John Guninita na Hamis Mgeja.
 
Apasuke na kuweka wazi nyaraka za richmond awe na mwakyembe
 
Ningemshangaa sana kama angekaa kimya kwa kudhalilishwa hivi.Ningemuona muoga.

Bado Joseph Msukuma wa Geita na Jesca wa Iringa

Hivi Mary Chatanda bado tu ?

Halafu wanawake wa CCM ni waoga.Vijana na wazee wameonyesha kusimama kidete kwenye hili swala.Nawashangaa akina Shelukindo wapo kimya.Hivi Anna Kilango ni coward kiasi hiki?
 
Sitta ndo ana haki kujivunia CCM, wananchi tunatambua mchango wake. Lakini Lowassa angezidi kula hela za Watz huku akiwapumbanza kwa kuwaaminisha kuwa mchapa kazi.
 
CCM vipande vipande,mwenyekiti wa chama tawala aonyeshe njia na mfano kwa vyama vya upinzani!
 
Asisahau kuzungungumzia TEMBO wetu,wanaisha jamani!

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Haya mazingaombwe ni mpaka 2015!

Magazeti yatauza sana safari hii
 
Wapi Mwakyembe, Wapi Ridhwani, Wapi Hussein Bashe? Nao waje uwanjani kuongeza mashambulizi zaidi.
 
Mkuu Ritz mzee wa kuchochea kuni wiki hii sijamuona kabisa au kaishiwa kuni tumsaidieee! Tunamsubili M/kiti uvccm naye alipuke na yule dogo kwa kulipuka lazima ccm iwe chaliii labda asiruhusiwe kutoa tamko!!! JK yy kesho lazima atoe tamko yaani ni mwendo wa matamko mpaka ccm ziwe 2 mwaka huu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom