Samwel Sitta kulipuka Jumatatu!

Samwel Sitta kulipuka Jumatatu!

Eee bhana eee ! Mbona ccm imekufa haraka namna hii jamani ? Unajua bhana , mimi nilijua ni kweli itakufa , lakini nilijua itakufa 2015 na sikutegemea ife 2014 !
 
this is the moment we're waiting for.someone call 911.
 
Dah naona huu ndo wakati wa wanaccm kuuza sura ok na mimi ngoja niwahi akitoka Six zamu yangu.
 
Wapi Madada Pacha Simiyu Yetu na Simiyu Voice,Ritz,Msalani,Ifweero,Dada Hamida,Mwekundu,Chamviga et al.
buku7 ktk issue kama hizi ukiwakuta ktk thread moja, wanakosoana hata wenyewe kwa wenyewe.ile team spirit waliyokuwa nayo siku zile haipo tena.
 
Matumizi ya media kwa wingi kuliko vikao vya chama ni ugonjwa wa wote wawili,CHADEMA na CCM..Japo kuna tofauti kidogo

1.Chadema wanatumia accounts feki sana na ni wazee wa keyboard zaidi,wanaogopa ukijitokeza tu hadharani kama CCM lazima usutwe na kutishiwa na mmiliki wa chama,mkwe wa mwenyekiti! So nawaelewa hawa wanaotumia fake accounts! Naelewa wanachoogopa.

2.CCM wanashindwa kutumia vikao kumuita na kumuhoji na ikiwezekana kama ana kosa apewe onyo kama sio kusimamishwa uanachama Lowassa kwa kuwa wanajua ile theory ya "mwaga mboga nimwage ugali"itatumika(hii ni hypothesis yangu) nahisi Lowasa ana maovu mengi ya wenzake kuliko waliyonayo against yeye ndo maana wanaogopa kumuita kikaoni,nafsi zinawasuta,wanakosa ile moral authority ndo maana wanapunguza machungu kwa kujidai wanaropoka kwenye media na kuitisha press conferences zisizoisha!

Kwa kifupi tunasema Chadema na CCM "same shit,different toilets"
 
Spika wa zamani Samwel Sitta anatarajiwa kutoa ya moyoni siku ya Jumatatu kuhusu kinachoendelea ndani ya CCM.

Taarifa kutoka watu wa karibu na kiongozi huyo aliyejipambanua kama mpiganaji wa vita dhidi ya ufisadi zinaeleza atazungumzia hali halisi iliyopo ndani ya CCM na huenda akatangaza vita zaidi dhidi ya ufisadi ndani ya chama hicho.

Waziri huyo wa Afrika Mashariki anasifika kama mtu asiyemumunya maneno na huenda akawasha moto mkubwa ndani ya chama hicho atakapozungumza.

Kwa sasa ndani ya CCM kuna mvurugano mkubwa kutokana na vita ya madaraka ambapo kwa wiki moja makada watano katika makundi mawili yanayoparurana wametuhumiana na kushambuliana mbele ya vyombo vya habari huku kila kundi likitumia kila silaha kushambulia lingine.Makada hao ni John Malecela,Paul Makonda,Richard Kyabo,John Guninita na Hamis Mgeja.

Alieleza vizuri kuhusa kuchagua kiongozi asiye na sifa za ufisadi katika sala za wakristo za mkesha wa mwaka mpya nadhani ni hayohayo. Matamko yaliyotolewa ni kwamba kila mtu ana mtu wake anayetaka awe Rais ndio sababu kushambuliwa EL. Kwa hiyo 2015 kutakuwa na kumegeka kwa CCM maana wale watakaoshinda katika kura za maoni watatoka.
 
Sitta ndo ana haki kujivunia CCM, wananchi tunatambua mchango wake. Lakini Lowassa angezidi kula hela za Watz huku akiwapumbanza kwa kuwaaminisha kuwa mchapa kazi.

Mkuu hujui Sitta, Mwakyembe, na Ole Sendeka ni baadhi ya wafuasi wa mtandao uliopangwa mathubuti kwa ajili ya kumharibia EL asigombee uraisi 2015, wakampiga na RICHMOND na walifanya hivyo kwa kua EL tangu kitambo alikua ameshaandaa timu yake na baraza la mawaziri na hao ni baadhi ya waliokiwa nje ya mpango wa EL. Walijua atakufa na presha na mawazo maskini mzee wa watu kakomaa hadi afya yake imerudi...EL for presidency!!!
 
Ningemshangaa sana kama angekaa kimya kwa kudhalilishwa hivi.Ningemuona muoga.

Bado Joseph Msukuma wa Geita na Jesca wa Iringa

Hivi Mary Chatanda bado tu ?

Halafu wanawake wa CCM ni waoga.Vijana na wazee wameonyesha kusimama kidete kwenye hili swala.Nawashangaa akina Shelukindo wapo kimya.Hivi Anna Kilango ni coward kiasi hiki?
hao wengine bado wanaanda matamko tuvute subira hakuna atakae baki mradi wailshaajiita wapambanaji ngoja tuwasubiri ila kuwakusha ni muhimu, wasije wakajisahau
 
Hivi hiki chama hakina mkubwa?Ni kama familiya ya Kambale,watoto wa kiume,watoto wa kike,baba na mama wote wana ndevu!

CCM eleweni hayo marumbano na mipasho yenu haimbomoi Lowasa wala kumjenga Sitta bali yanakibomoa chama! Ni aibu kwa mtu kama Malecela anajipambanua kuwa ni mkongwe badala ya kutumia taratibu za chama naye anaingia kwenye marumbano ya kwenye makorido.

Wananchi tumechoka kusikia Lowasa lowasa,tunataka kusikia kiinua mgongo cha wabunge,kupanda kwa umeme,mapigano ya wakulima na wafugaji.Sitta kama unaongea ongelea hayo!
 
Mkuu Ritz mzee wa kuchochea kuni wiki hii sijamuona kabisa au kaishiwa kuni tumsaidieee! Tunamsubili M/kiti uvccm naye alipuke na yule dogo kwa kulipuka lazima ccm iwe chaliii labda asiruhusiwe kutoa tamko!!! JK yy kesho lazima atoe tamko yaani ni mwendo wa matamko mpaka ccm ziwe 2 mwaka huu
anasikilizia upepo!
 
Hivi Zitto alichanga ngapi au yeye alichanga Chauma.?

hapo Zitto ndo anasahaulika mazima, hata zile dolari za kuchukuliwa Ujerumani na "baby" Andrea kwishney kabisa maana hawawezi kuzima moto kwenye nyumba ya jirani ilihali yao ya makuti ndo kwanza imetiwa petrol!
 
Ningemshangaa sana kama angekaa kimya kwa kudhalilishwa hivi.Ningemuona muoga.

Bado Joseph Msukuma wa Geita na Jesca wa Iringa

Hivi Mary Chatanda bado tu ?

Halafu wanawake wa CCM ni waoga.Vijana na wazee wameonyesha kusimama kidete kwenye hili swala.Nawashangaa akina Shelukindo wapo kimya.Hivi Anna Kilango ni coward kiasi hiki?

Chochea kuni ahaaaa kibanda cha ccm kinaungua...
 
Ccm hawajielewi,wapinzani na wenyewe walikuwa hawajielewi kidogo sasa wameshtuka toka kwenye usingizi wa pono,haya tusubirie tamthilia itaendelea vipi.
 
Sasa CCM this is too much. Hebu fanyeni kikao mtoe tamko la chama, tumechoka na haya matamko ya vijiweni
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom