Samuel Sitta huwa anafikiriaje?

The Stig

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
1,113
1,105
Jana nilisikitika sana kumsikia kwenye redio Mh. Samuel Sitta akipinga wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika kilimo cha zao la janthropa. Zao hili linatumika kutengeza diesel ya mimea. Kuna wawekezaji wameonesha nia ya kuwekeza kwenye kilimo kikubwa cha zao hili na SS alikuwa anatoa maoni yake.


SS anadai kuwa uwekezaji huo, unaohitaji mashamba makubwa sana (e.g. heka 20,000) utakuwa ni uwizi wa ardhi ya waTZ. Anadai kwamba badala ya haya mashamba, tuwekeze kwenye uzalishaji wa umeme wa jua.
  • Hivi SS anajua kuwa teknolojia iliyopo hairuhusu uzalishaji wa umeme mwingi kutokana na jua? Mradi mkubwa kuliko yote ya umeme jua DUNIANI unazalisha MW 40 tu. Uwezo huu ni sawa na; nusu ya Mtera, au pungufu ya nusu ya IPTL, au moja ya tano ya Ubungo, au asilimia moja (1%) ya Steigler kama ikijengwa)
  • Hivi SS anashindwa kujiongeza na kuona kuwa mradi mkubwa kama shamba la heka 20,000 litazalisha ajira za maana za kutosha sehemu ambapo sasa hivi hakuna ajiri? Miradi hii italeta ajira za moja kwa moja kwa wataoajiriwa na haya mashamba (wataalama wa kilimo, watawala, madereva, wahasibu, watu wa tehama etc). Vile vile italeta ajira zisizo za moja kwa moja (wauza maduka, wahuduma wa nyumbani, mafundi gereji, mafundi ujenzi, walimu, polisi etc)
  • Hivi SS, ambaye anasafiri na ndege kila siku, anaweza kusema kweli Tanzania tunatumia ardhi yetu vizuri? Ukiruka na ndege kuelekea S. Africa, utaona kuwa ukishatoka tu juu ya anga ya DSM, Tanzania yote ni pori. Hii ni tofauti na unapokuwa juu ya S. Africa – unakuta kila sentimita imetumiwa na mashamba makubwa.
  • Huo mradi wa umeme jua, kuna mwekezaji gani wa maana ameonesha nia ya kuwekeza? Ni mwekezaji gani atae leta pesa yake ya maana kuja kuzalisha umeme huu mdogo ili awauzie shirika muflisi kama Tanesco? Tanesco imeshindwa kufanya biashara na IPTL, Songas wanalalamika, halafu ujilete na wewe upoteze hela yako – never. Labda Tanesco ibinafsishwe.
  • Mwisho, mradi wa janthropa utaongeza mauzo ya nje ya Tanzania. Hii itapunguza nakisi ya mizani ya balance of trade na kufanya shilingi yetu angalau isiwe inaporomoka tu kila siku.
 
Ukiona hivyo ujue anajua kilichoko nyuma ya huo mradi wa kilimo alafu hawezi kusema (POLLU.....)
 
wizi mtupu,mzee sitta kaushtukia..mmesahau kule mbarali walisema hivyo hivyo matokeo yake mchele ambacho ni chakula kikuu tanzania uzalishaji ukadrop ile mbaya na mbolokabuli yenyewe haikuzalishwa wala nini,waongo bwana wanakujaga na gia hiyo ili wapate ardhi tu

sometimes haya mambo ni zaidi ya tujuavyo tuliyopo nje?
 
Hivi SS, ambaye anasafiri na ndege kila siku, anaweza kusema kweli Tanzania tunatumia ardhi yetu vizuri? Ukiruka na ndege kuelekea S. Africa, utaona kuwa ukishatoka tu juu ya anga ya DSM, Tanzania yote ni pori. Hii ni tofauti na unapokuwa juu ya S. Africa – unakuta kila sentimita imetumiwa na mashamba makubwa.....

Suala sio kuwepo kwa mapori au ardhi kubwa,la msingi hapa ni kuangalia matokeo hasi ambayo yatatokana na kilimo hiki.Ujerumani wamesitisha utumiaji wa mafuta ya mimea kuendeshea ndege zao kwa sababu ya uhaba wa chakula na ardhi kuwa finyu.Unaweza kuona ni sawa kwa sasa kuruhusu kilimo cha namna hiyo lakini katika nchi yetu ambapo uzazi umekuwa si wa mpango,idadi ya watu inaongezeka kila kukicha,ukosefu wa ardhi katika miaka ya baadaye ni vita.Hata NYERERE aliona mbali ndio maana akaacha kuruhusu uchimbaji wa madini.
 
SS is damn right, keshaona nyuma ya pazia ya huo mradi kuna nini ili kupinga lazima apinge in indirect way. Hayo yote uliyosema The stig mh. SS anayafahamu bt kuna ufisadi ndani yake hapo.
 
Na wewe uwe unafikiria kila siku huwa tunalalamika kwamba ardhi inaibiwa na kupewa wawekezaji kwa kisingizio cha kusema kwamba wananchi watafaidika lakini wapi? Jamani huyu kaliona hilo na ndo maana anakataa. Acha tufe na umaskini wetu lakini ndani ya ardhi yetu. Kama wana nia ya kuwekeza kwanini wachague kutumia ardhi na si solar?
 
SS is damn right, keshaona nyuma ya pazia ya huo mradi kuna nini ili kupinga lazima apinge in indirect way. Hayo yote uliyosema The stig mh. SS anayafahamu bt kuna ufisadi ndani yake hapo.

Tumwangalie na yeye ktk nyuma ya pazia lake siyo kwamba anafanya yote haya kwakuwa anataka uraisi na anatumia hizi njia kwakujipatia umaarufu wa kisiasa?
 
Kama sita una uchungu na nchi yako na uko kwenye chama ambacho kinachofanya mambo ambayo yanazorotesha Taifa onyesha uzalendo kwakuwahama na kwenda shm yenye mwelekeo ama kuanzisha chama chako
 
Tumwangalie na yeye ktk nyuma ya pazia lake siyo kwamba anafanya yote haya kwakuwa anataka uraisi na anatumia hizi njia kwakujipatia umaarufu wa kisiasa?

tukiendelea mchezo huu ulioanzishwa na mafisadi wa kumhusisha na mbio za urais yeyote aliye tayari kuzuia maovu kabla hayajatokea wazalendo wengi wataogopa kujitokeza,wataamua kukaa kimya na utakua ushindi wa wezi wa rasilimali za nchi hii,tuache mara moja kutumika na mafisadi bila kujijua
 
Mzee sitta ana busara sana! Sio kama mkenua meno vasco da gama!
 
Kwa jinsi nilivyosikiliza hoja ya Mhe. Samwel Sitta, alilokuwa anaghusia lina mantiki kubwa sana. Kwa Watanzania suala kubwa kwa sasa ni upatikanaji wa uhakika wa chakula kwa wananchi wote.

Inabidi kuwa makini sana na hawa wawekezaji wanaotaka kuchukua maelfu ya ekari za ardhi ya Watanzania kwa kisingizio cha kuzalisha mazao kwa ajili ya nishati. Ni vizuri tukajikumbusha mambo waliyofanya akina Chavda ya kujifanya kuwekeza kwenye ufufuaji wa mashamba ya mkonge lakini kilichotokea alitumia hati za mashamba hayo kujichotea mamilioni ya fedha kutoka benki na kutokomea kusikojulikana huku akiacha mashamba yaliyolengwa yakibadilika kuwa mapori.

Sitta anaonesha wasiwasi wa Watanzania kugeuzwa kuwa vibarua baada ya ardhi yote/sehemu kubwa ya ardhi kunyakuliwa na wanaojifanya wawekezaji.
 
Nishamzarau 6, ko kila anachongea ni kwa manufaa yake na genge lake. Hakuna msafi ndani ya magamba yote yanaigiza tu. Huyu mze ni mchumia tumbo. Hakuna cha mana siku izi toka kwa 6
 
The Stig Umepotoka tafakari tena ndugu yangu!
labda nikupe hint tu!

1.Hawa jamaa wakija hawapewi mapori wakime, ila wanachukua mashamba ya wakulima wetu wadogowadogo( naamini unalijua hili)
2. Kama ni hela za kigeni na mauzo, unaweza kuniambi Tanzanite. dhahabu, samaki mwanza na Gold zinachangia kiasi gani kwenye uchumi wetu?
 
Back
Top Bottom