Samuel Sitta huwa anafikiriaje?

Anayoongea Mzee Sita huwezi kuyaelewa kama una akili za kitumwa tumwa. Wanasi-hasa wengi wanadhani kila mradi unaoletwa na wazungu unatatua matatizo yetu ya msingi na nikwamanufaa yetu. Akili ya mzee Sita inatizama mbele zaid ya 'fikshenz' za jatropha na nishat mbadala. Tusubili tuone...
 
Jana nilisikitika sana kumsikia kwenye redio Mh. Samuel Sitta akipinga wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika kilimo cha zao la janthropa. Zao hili linatumika kutengeza diesel ya mimea. Kuna wawekezaji wameonesha nia ya kuwekeza kwenye kilimo kikubwa cha zao hili na SS alikuwa anatoa maoni yake.


SS anadai kuwa uwekezaji huo, unaohitaji mashamba makubwa sana (e.g. heka 20,000) utakuwa ni uwizi wa ardhi ya waTZ. Anadai kwamba badala ya haya mashamba, tuwekeze kwenye uzalishaji wa umeme wa jua.
  • Hivi SS anajua kuwa teknolojia iliyopo hairuhusu uzalishaji wa umeme mwingi kutokana na jua? Mradi mkubwa kuliko yote ya umeme jua DUNIANI unazalisha MW 40 tu. Uwezo huu ni sawa na; nusu ya Mtera, au pungufu ya nusu ya IPTL, au moja ya tano ya Ubungo, au asilimia moja (1%) ya Steigler kama ikijengwa)
  • Hivi SS anashindwa kujiongeza na kuona kuwa mradi mkubwa kama shamba la heka 20,000 litazalisha ajira za maana za kutosha sehemu ambapo sasa hivi hakuna ajiri? Miradi hii italeta ajira za moja kwa moja kwa wataoajiriwa na haya mashamba (wataalama wa kilimo, watawala, madereva, wahasibu, watu wa tehama etc). Vile vile italeta ajira zisizo za moja kwa moja (wauza maduka, wahuduma wa nyumbani, mafundi gereji, mafundi ujenzi, walimu, polisi etc)
  • Hivi SS, ambaye anasafiri na ndege kila siku, anaweza kusema kweli Tanzania tunatumia ardhi yetu vizuri? Ukiruka na ndege kuelekea S. Africa, utaona kuwa ukishatoka tu juu ya anga ya DSM, Tanzania yote ni pori. Hii ni tofauti na unapokuwa juu ya S. Africa – unakuta kila sentimita imetumiwa na mashamba makubwa.
  • Huo mradi wa umeme jua, kuna mwekezaji gani wa maana ameonesha nia ya kuwekeza? Ni mwekezaji gani atae leta pesa yake ya maana kuja kuzalisha umeme huu mdogo ili awauzie shirika muflisi kama Tanesco? Tanesco imeshindwa kufanya biashara na IPTL, Songas wanalalamika, halafu ujilete na wewe upoteze hela yako – never. Labda Tanesco ibinafsishwe.
  • Mwisho, mradi wa janthropa utaongeza mauzo ya nje ya Tanzania. Hii itapunguza nakisi ya mizani ya balance of trade na kufanya shilingi yetu angalau isiwe inaporomoka tu kila siku.

hizo biofuel zitakazotengenezwa hazitatumika hapa bali zitapelekwa Ulaya! Halafu ina maana wewe huoni jinsi migogoro ya ardhi inavyojikita hapa nchini? Hawa wawekezaji kwanini wasinunue hizo jatropha toka wakulima wadogowadogo kama kahawa inavyonunuliwa toka wakulima huko Kilimanjaro, Arusha, Mbeya na Bukoba! Tumia fikra kidogo kuona kaburi tunalojichimbia haswa kwa kutumia ardhi bora kulima mimea ya nishati badala ya chakula
 
Back
Top Bottom