Ile haki ya kula chakula kwa shilingi elfu 2 kwa siku, si dhana ya kufanyia mzaha. Tanzania, inapaswa kumuheshimu mkulima kwa jasho analovuja na kutuwezesha kununua vyakula kwa bei che. Tukianza kilimo cha mazao ya biashara bila kukumbuka mazao ya kula, gharama za chakula zitapanda sana, haswa kwa watu waishio majini na haki ya kula tutaipoteza.
Nchi ambayo, haina viwanda vya kutosha hata ya kutengeneza vya kula vya makopo, kujaribu kujikita katika uzalisha wa mazo yasio ya biashara, ni dalili za njaa kwa taifa letu.Wakulima hawatalima tena kuwalisha watu wa mijini. Watalima chao kinachowatosha na kuzalisha kingine kwa biashara. Watoto wao watakuwa manamba kwenye ardhi yao - kuhakikisha wanapata kipato.
Unayoyasema sita, yaweza yasionekane sasa kwa kuwa akili zetu zimejikita kibiashara zaidi na kuchoshwa na umaskini wetu! Lakini faida ya mafuta ya mimea kwa tanzania ni ipi?