Samsungs wanashida gani?

Hiyo chai simu utumie internet lazima ichemke Tena ukiongeza na joto la nje kama upo Dar au ukanda wa Pwani betri inaisha haraka haiwezi kukaa masaa 24 labda kama unaiwasha na kuizima na kuiwasha baada ya masaa kadhaa
Labda hiyo unayotumia wewe.
Mimi simu yangu haiwahi kuwa na huo ukanjanja.
 
Rejea niliposema matumizi ya kawaida.
Data ipo on full time
Sichezi game
Zaidi ya kubrowse twitter na jf

Nimezima background data app zisizo muhimu. Background data nimeipa Bluemail na Whatsapp.

Sasa kwa nini simu isikae chaji tu
 
Mkuu reyzzap umefafanua kwa weredi mkubwa kabisa. Ni kweli katika flagship kampuni haiwezi ku-compromise na design ya simu for the sake of battery. Kwa kuwa nakuona una uelewa wa simu naomba unisaidie kujua, Je Galaxy A22 inakaa na charge muda gani? Ninataka ku-upgrade kutoka kwenye hizi Tecno and co. Je camera yake ina kiwango kizuri? Binafsi nimeridhika na sAmoled tech, 90 hz refresh rate, OIS tech na miaka 2 ya software updates ila bado sijainunua kwa sababu sina uhakika na battery pamoja na camera yake.
 
Me natumia vivo v21 na ina battery 4000 mAh na inakaa na chaji siku nzima ...
 
Daa hii simu nimeiachia last week, Camera ni nzuri, battery ni uhakika siku nzima Data ON na unalala na charge, Display nzuri, kwa ufupi niliridhka nayo karibuni kwenye kila kitu, ukinunua wahi kuweka hizi Silicone cover zenye kama wax kwa chini mana inakwaruzika kirahisi.

Kati ya simu ambazo sikushauri uziwaze ni A21s, A12, A11, bora hata A10s ina camera na display nzuri practically, hizi A-series nimecheza nazo sana
 
Asante sana kwa ufafanuzi huo. Nimetatanika sana kati ya simu tatu za A22, Redmi note 10S na realme 8 kwa sababu they are around the same price range lakini sikuwahi kupata mtu ambaye ametumia simu hizi hasa kwa mazingira ya hapa nilipo.Lakini sasa nimehakikishiwa.
 
Hilo game la maleo limenifanya mpaka nimeuza galaxy S7 edge sababu ya chaji kuisha haraka nikicheza masaa mawili mfululizo simu inazima chaji alafu inakua ya moto balaa sasa nimekamata galaxy A12 sasa nacheza mpaka hamu inaisha na bado nakuwa nimebakiwa na% nyingi tu za matumizi mengine

Sent from my SM-A127F using JamiiForums mobile app
 
Kaka sasa unafeli yani A10s ubora wake ni upi mpaka iishinde A12 au A12 body design yake ilivyo kaa vibaya ndio unaiona ni simu ya hovyo mpaka ukaishusha kwa A10s angalia specification mwenyewe kisha ujisahihishe

Galaxy A10s

Display 6.2 PLS IPS
720×1520 pixels

13 mp
1080p

2/3 RAM
helio p22

4000 mAh

Storage 32gb



Galaxy A12

Display 6.5 PLS IPS
720×1600

48MP
1080p

4/6 RAM
helio p35

5000 mAh

Storage 32/64/128

Sent from my SM-A127F using JamiiForums mobile app
 
H
Siwezi tumia simu ambayo si flagship and current ndo tatizo. Nimeshazoea premium features so mi ni mwenzo wa Samsung S series au Iphone tena current versions.
hivi kwa iphone 11pro max na xs max ukaaji wa chaji maana naona watu wanaipondea sana.
 
mi naulizia kati ya iphone 11 pro max/ xs max na oneplus 9RT 5G.

Na kwa hapa bongo kuna sehemu duka la 1+ wenye unboxing phone
 
Hii samsungs sijui ni kampuni gani!

Nakushauri hachana na makumpuni feki ya kichina kama Samsungs, Dunia tunafahamu Samsung tu.
 
Hivi simu gani ipo vizuri hapo?? Kuna ka itel kamoja kalikuwa balaa,, hakawezi kukutoa mchezoni ..labda istuck ila utacheza hadi uleave room mwenyewe,, nikaja jarbu na samsung moja unashangaa imerudi home yenyewe...
 
Hivi simu gani ipo vizuri hapo?? Kuna ka itel kamoja kalikuwa balaa,, hakawezi kukutoa mchezoni ..labda istuck ila utacheza hadi uleave room mwenyewe,, nikaja jarbu na samsung moja unashangaa imerudi home yenyewe...
Simu ikiwa na ram kuanzia gb3 unacheza vizuri bila kugandaganda

Sent from my SM-A127F using JamiiForums mobile app
 
Habari waungwana ,asee nna Samsung A22 ambayo ni mpya ,,ila inatatizo la kutoweza kukubali line ya halotel ,line zingine zinasoma ,,line ha halotel inasoma ilaninaweka ''emergency calls only"
 
Hiyo samsung anayotumia mtoa mada itakuwa fake sio Samsung A ninazozijua yangu huwa nacharge nikienda kulala toka 2019 ipo mzigoni sijawahi jutia.niliiweka kabatini nikairudia A70
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…