Samsungs wanashida gani?

Faida ya S Pen ni ipi?
 
Kawaida masaa mangapi kwa matumizi ya kawaida ?

Mfano mimi natumia Oppo , bat ni 4230mah, full time data matumizi ya kawaida nafikisha masaa 36 na ushee
Hio battery natumia within10hrs naimaliza kabisa ..nyie ni wale mnàsema full data on kumbe mmewasha na hamtumii. Hakuna simu hata hizi zenye 5000mah inaweza kaa 16hrs ikiwa inatumika ..nyie labda hamtumii simu...yangu ina 4000mah mwanzoni íkiwa mpyà ilikuwa inatumia 7% kwa lisaa mtandaoni bila screen kuzima hata kidogo muda wote ni ku scroll tu

2hrs ndo unajikuta imebaki 86% bila screen kuzima .. on WiFi ilikúwa 5% kwa lisaa

Imagine namna inakaa na chaji kwa matumizi heavy screen haizimi ila bàdo unafuta chaji vizuri tu. Kwa ulaji huo means ikiwa imejaa hadi ibaki 10%unatúmia 2hrs sasa how mtu anasema simu imekaa karbu siku mbili kwa data ...hio simu yako inabd ulete uone ñamna inatumika
 
Nyie hamtumii simu et ..hio simu unayosema inakaa masaa24 data on embu weka mb ingia insta weka stop watch, ukitoka nenda youtube kula video kadhaa tumia kama lisaa tu screen isizime afu kumbuka ilikuwa ina % ngap na imebaki ngap ndo uje ulete mrejesho kama inaweza kaa hayo masaa
 
True niliwah soma sehemu muda kidogo why simu hizi high end hazina battery kubwa ... sababu zilikuwa nyingi sana na zote ziko nje ya uwezo wao..ila kusolve hio kitu wakaweka fast charging kama hizi 18w yani hata kama battery haikai sana ila ukipata penye umeme ni dk 50 tu Ngoma ipo full kabisa
 

mimi nashangaa mkuu.

hawa ndio wale wanaowasha na kuzima data.mtandao anaoinga ni whatsapp na facebook,mwanga anaweka 35% mpaka juani hapandishi.
wakati kwa utaratibu huo hata iphone na samsung ukifanya hivi utaipenda.

juzi nimeshika infinix hot 11 sijui nambiwa inakaa na charge balaa,nikapeleka 100% mwanga nikaanza kusurf maeneo mbali mbali,ndani ya dakika 20 iko na 95%
na hapo sijaplay hd video wala kucheza migemu ya sifa.
 
Balaa tupu

Mwaka juzi simu hii hii yenye 4000mah..kuna game laitwa maleo tunacheza online hadi umalize ñi kama 20-25min muda huo wote inatumia 4% ..hivo hadi nimalize 20% ni kama game tano online ..kabla ya hapo nilikuwa nacheza na simu moja ukicheza round mbili ya tatu lazima ukae kwenye chaji ndo úcheze

Haya kuna mtu ana smart 5 kachaji j3 leo anakwambia ina 73% muda huu 😁 wakati simu hio hio nilitumia siku mbili mfululizo kila siku namaliza chaji ila mwenye nayo leo siku ya tatu ina 73%😁
 

Ingekuwa smartphone ni kubwa zina space ya kutosha kwa nyuma ningeweka hizi mbili tu
 
nazo unazichaji vipi
Kwa hapo zilivo hio samsung haiwezi chaji hizo battery japo zote ni lithium ion kama original battery ya simu utofauti ni capacity tu kwa sababu ya

1. Ili simu hio ianze peleka chaji inabdi saketi original ya battery iwe kwenye simu kisha ndo uchukue zile waya zinazoenda kwa battery uweke hapo ..sababu kwenye battery kuna terminal tatu moja kwa ajili ya information za battery hivo simu ikikosa taarifa za battery hio haitachaj.

Solution kuna njia mbili za kuichaji hio battery

1. Kuidanganya hio simu kuwa inachaj battery yake kwa kufunga bms original ya battery yake kati ya simu na hizo battery

2. Utumie module za kuchajia kama tp4056 nk
 
Battery inachukua space na inaongeza uzito. S na Note series ni flagships ambapo lazima ziwe na uzito wa kawaida. Ukitaka battery kubwa basi chagua mid range phones kama A series au realme.
 
Battery inachukua space na inaongeza uzito. S na Note series ni flagships ambapo lazima ziwe na uzito wa kawaida. Ukitaka battery kubwa basi chagua mid range phones kama A series au realme.
Ila chanzo cha watu kusema simu hazikai na chaji ni kwakuwa hawanunui mpya.
Kama hiz S series za Samsung mtu anachukua S8,S8 au S10 huko anadanganywa mpya wakati kwa sasa hiwezi pata mpya bongo hapa ndio tatizo linapoanza
 
Kati ya simu zinakaa na chaji ni iphone, sasa hiyo ya kwako sijui umetengeneza mwenyewe?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…