ManiTek TV
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 410
- 159
10/03/2013
Galaxy S Kuipiku iPhone?
Galaxy S Kuipiku iPhone?
Samsung ndio kampuni inayoitia tumbo joto Apple katika simu. Ingawa kama simu moja, kuanzia iPhone ya kwanza hadi ya sita yaani iPhone 5, simu hii imekuwa ikiongoza kwa mauzo tangu mwaka 2007. Lakini katika miaka minne iliyopita Samsung walianzisha familia ya Galaxy S, familia hii imekuwa ni tishio kubwa kwa ufalme wa iPhone katika mauzo. iPhone zimeshauzwa milioni 133.7 na Galaxy S zimeuzwa milioni 74.3.
Takwimu za awali zilionyesha kwamba huenda mauzo ya Galaxy S yakawa makubwa kuliko ya iPhone kwa mwaka 2012, lakini hatimae baada ya kutolewa kwa iPhone 5 mambo yalibadilika na iPhone kuendelea kushikilkia nambari moja katika mauzo. Wengi miongoni mwa wadau wa gajeti hasa washabiki wa Android wanadhani kwamba hatimae familia ya Galaxy itatwaa namba moja katika mauzo ya simu ulimwenguni kwa simu aina moja pekee, hivyo ni imani ya wadau hao kuwa hili litatokea miaka hii tuliyo nayo. Hebu tupitie ni nini hasa kinaweza kuifanya Galaxy S iwe juu ya iPhone na tuone kama iPhone wataweza kutetea taji lao kwa miaka mingi zaidi.
Kabla ya lolote kwa sasa takwimu zinaonyesha kwamba mwaka 2010 Apple walikuwa wameuza mara nne ya Galaxy S, yaani galaxy S ilikuwa kwenye wastani wa simu milioni 10 na Apple waliuza iPhone milioni 40. Ilipofka mwishoni mwa mwaka jana Samsung imeuza Galaxy S milioni 75.3 wakati Apple wameuza simu milioni 133.7, hivyo ni wazi kuwa Samsung inajitutumua vilivyo katika mauzo ya Galaxy S. Sasa tuingie kwenye mambo yanayowapa mafanikio Samsung:
Mosi, Uzuri wa simu za Galaxy S ndio jambo la awali linaliowezesha Samsung kuwa na mauzo mazuri duniani. Galaxy SII ilikuwa ndio simu nyembamba ya mwaka 2011 ikiwa na upana wa milimeta chini ya 7. Galaxy SIII nayo ilikuwa na umbile na ukubwa unaovutia mno.
Pili, Android imekuwa ikipiga hatua kubwa kimaendeleo kama OS, ambapo ingawa bado inaaminika kuwa na kasoro mbili tatu ukilinganisha na iOS, lakini bado Android Jelly Bean imekuwa ni OS iliyopiga hatua kubwa ukilinganisha na enzi zile za Android Donut, Eclair na Froyo. Tayari kampuni ya Google iko jikoni ikipika Android mpya itakayojulikana kama Key Lime Pie.
Tatu, Simu za familia ya Galaxy S zimekuwa zikitoka na matumizi mbali mbali ambayo huwezi kuyapata kwenye simu nyingine za Android. Mambo kama vile yaliyotoka kwenye SIII yaani Smart Stay, S Beam, Popo Up Play, Smart Alert na Direct Call yanaifanya Sammy ionekane ni kampuni yenye uvumbuzi wa hali ya juu.
Nne, Sammy (Samsung) inajitegemea zaidi kuliko Apple katika Hardware mbali mbali, wakati Apple wanachofanya ni kubuni (design) na kufungasha (Assemble) Samsung wanatoa wenyewe sehemu mbali mbali za simu kama vile skrini na mambo mengine.
Tano, Samsung ndio kampuni yenye bajeti kubwa zaidi miongoni mwa kampuni za elektroniki Duniani ambapo hutumia kiasi cha Dola za Kimarekani Bilioni 5 kila mwaka kwa ajili ya matangazo ya biashara tu. Kwa mfano Samsung walitoa tangazo maalum la kuiponda iPhone 5.
Hivyo sifa kama hizi zimekuwa zikiinyanyua Samsung mwaka hadi mwaka, kwa upande wa Apple wao wameweza kuwepo walipokuwepo na huenda wakaendelea kuongoza katika mauzo kwa sababu zifuatazo:
Mosi, iOS ni nguzo kubwa ya iPhone ambapo ni OS iliyoleta mapinduzi ya simu mwaka 2007 pale iPhone ya kwanza ilipotoka. iOS ina sifa ya urahisi katika utumiaji na hukubali amri za mtumiaji kwa heshima (very responsive). Kinyume na Samsung ambao wao hutegemea Google kwa maendeleo ya Android, Apple iOS ni yao wenyewe na iPhone ndio simu pekee inayotumia OS hiyo. Pia iOS ni platfomu inayoongoza kwa kuwa na Apps nyingi tena zenye ubora zaidi.
Pili, Kitengo cha ubunifu (design) kikiongozwa na Sir Jonny Ive kimekuwa kikiwaacha watu mdomo wazi kila wanapotoa gajeti mpya, umbile kama vile la iPhone 5 ambapo kuna ufito wa mng'ao kwenye nzunguko wa simu, tayari ufito huu umeshaigwa na simu mbali mbali kama vile HTC One.
Tatu, Apple wana fedha za kutosha (cash reserve), hivyo watakapoamua kufanya matangazo zaidi, ua utafiti zaidi basi fedha sio tatizo. Kuna wakati Apple walikuwa na fedha nyingi kuliko serikali ya Marekani. Hata hivyo serikali ya Marekani fedha ni tatizo sugu kwa sasa.
Nne, iPhone imekuwa simu ya aina ya peke yake, ukiangalia simu nyingine zote ama ni utitiri wa Android au utitiri wa Windows Phone. iPhone haina mwenza, ikitaka kutumia Siri basi lazima uwe na iPhone lakini ukitaka jambo lolote la Android sio lazima uwe na Galaxy S. Na pia ukitaka kutumia S Beam basi ukinunua simu yoyote mpya ya Samsung unaweza kupata jambo hilo.
Tano, ingawa wahenga wanasema "kutangulia sio kufika" Apple na iPhone yao wapo walipo kwa vile walitangulia. Kutangulia huko kukipewa nguvu ya kusonga mbele ya utafiti wa kuindeleza gajeti hiyo kumeifanya iPhone ibaki kuwa namba moja katika mauzo kwa miaka mingi sasa.
Usikose sehemu ya pili ya makala hii tutakapozungumzia udhaifu wa Apple katika miaka ya karibuni kwa upande wa iPhone.
Je Galaxy S4 itakayotangazwa siku 3 zijazo ndio simu itakayoifanya Apple iPhone ishuke hadhi?
Je mbali na mauzo ni ipi namba moja kwa sasa: Samsung Galaxy SIII au Apple iPhone 5?

Tafadhali weka comment kuhusu