Kwa wale wanaotaka kubadili brand na kwenda brand maaarufu kama Samsung kuweni makini hasa kwenye Samsung A series". Ukifuatilia kwa makini utagundua kampuni ya Samsung wametoa A series kwa ajili ya wateja wanaotaka kumiliki brand ya Samsung ila bajet yao ndogo ila kiukweli Samsung A series inazidiwa ubora na simu nying za "low end".
Samsung wametoa A series ambazo bei zake zipo chini around 320k-370k kwa A10s na A20s. Simu hizi nimezitumia na zina madhaifu yafuatayo:
1.Dispaly" ki ukweli display zake ni low quality ukilinganisha na brand nyingine za Samsung kama "S series" ukiingalia display bila kuangalia jina unaweza jua Tecno au Infinix.
2. Network hizi simu zina 4G ila hazina kasi kabisa. Unaweza washa data na isirespond mpaka urestart simu ndo inakubali.
3.haina "Front flash" ni ajabu Samsung kutoa simu ya 370k haina flash ya mbele. Sahau kupiga selfie usiku.
4. Camera hafifu hizi simu zina camera hafifu ambapo ukipiga kwenye giza inatoa picha yenye rangi ya maziwa hivyo kuharibu ubora wa picha. Picha za usiku sahau kabisa.
5. Kwenye box lake imeandikwa "FOR AFRICA"
Samsung walichojitahidi hasa ni uwezi wa Betri ambayo kwa wastani inakaaa vizur na chaji.
NB: Kama ubataka kubadili brand ya simu kwenda Samsung ni bora ukatafuta brand nyingine kama "S series" ila sio "A series". Utachofaidi ni brand ya "SAMSUNG tu"