Samsung "A series" ni simu zenye ubora hafifu; kuwa makini

kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
7,815
2,000
Kwa wale wanaotaka kubadili brand na kwenda brand maaarufu kama Samsung kuweni makini hasa kwenye Samsung A series". Ukifuatilia kwa makini utagundua kampuni ya Samsung wametoa A series kwa ajili ya wateja wanaotaka kumiliki brand ya Samsung ila bajet yao ndogo ila kiukweli Samsung A series inazidiwa ubora na simu nying za "low end".

Samsung wametoa A series ambazo bei zake zipo chini around 320k-370k kwa A10s na A20s. Simu hizi nimezitumia na zina madhaifu yafuatayo:

1.Dispaly" ki ukweli display zake ni low quality ukilinganisha na brand nyingine za Samsung kama "S series" ukiingalia display bila kuangalia jina unaweza jua Tecno au Infinix.

2. Network hizi simu zina 4G ila hazina kasi kabisa. Unaweza washa data na isirespond mpaka urestart simu ndo inakubali.

3.haina "Front flash" ni ajabu Samsung kutoa simu ya 370k haina flash ya mbele. Sahau kupiga selfie usiku.

4. Camera hafifu hizi simu zina camera hafifu ambapo ukipiga kwenye giza inatoa picha yenye rangi ya maziwa hivyo kuharibu ubora wa picha. Picha za usiku sahau kabisa.

5. Kwenye box lake imeandikwa "FOR AFRICA"

Samsung walichojitahidi hasa ni uwezi wa Betri ambayo kwa wastani inakaaa vizur na chaji.

NB: Kama ubataka kubadili brand ya simu kwenda Samsung ni bora ukatafuta brand nyingine kama "S series" ila sio "A series". Utachofaidi ni brand ya "SAMSUNG tu"

20201206_113116.jpg
 

kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
7,815
2,000
Flash ya camera ya mbele ipo na inatumia mwanga wa screen yote may be hujaona kale kaflash kenyewe ukajua haina, by the way hii cm n nzur labda ukiniambia display ntakubali. Ila vingne NO😄
Nimeseha hazina front flash we unasema ipo inatumia mwanga wa screen... sijajua unapinga nini hapo.Nimetumia zote A10s na A20s na nina uhakika na nilichokiandika
 

miminimkulimaakachekasana

JF-Expert Member
May 29, 2017
3,285
2,000
Mkuu A series ni ambayo imekuwa ranked chini ya S series kwa hiyo iko vizuri sema kuna zile chini Ya A 30 zina specs za Entry level labda ndivyo maana umeona sio za kijanja
 

danielhipoliti

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
397
500
Aisee iyo A10s nilipo iona mara ya kwanza ile shape ya mbele nilijua kama sio infinix itakua Tecno

Ila display yke ni ovyo kabisa amna tofauti na Tecno
Arafu bei ni juu kuliko ubora wake
 

kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
7,815
2,000
Aisee iyo A10s nilipo iona mara ya kwanza ile shape ya mbele nilijua kama sio infinix itakua Tecno

Ila display yke ni ovyo kabisa amna tofauti na Tecno
Arafu bei ni juu kuliko ubora wake
Sure mkuu Infinix ya 280k ina ubora zaidi kuliko Samsung A10s ambayo inauzwa 320k
 

kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
7,815
2,000
Aisee iyo A10s nilipo iona mara ya kwanza ile shape ya mbele nilijua kama sio infinix itakua Tecno

Ila display yke ni ovyo kabisa amna tofauti na Tecno
Arafu bei ni juu kuliko ubora wake
Sure mkuu Infinix ya 280k ina ubora zaidi kuliko Samsung A10s ambayo inauzwa 320k
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom