GE2025 Samia anashindana na nani kwenye Urais?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,564
Reaction score
7,326
Eti wadao mimi sijaona mgombea mwingine wa Urais akifanya Kampeni, Je nauliza Samia anashindana na nani?

1760769902443.png

Au watu Millioni 60 nchi nzima hakuna mtu anayeweza kuchuana na Samia. Maana kuanzia kwenye vikao vya CCM Samia hakupata mshindani, tumekuja kwenye Kampeni bado hatuoni mshindani wake.

Sasa maana ya demokrasia ni nini, mfumo wa vyama vingi una kazi gani, kama mtu anagombea peke yake... si bora turudi kwenye utawala wa kifalme tu, tumchague Samia kuwa Malkia wa Tanzania tujue moja. Maana malkia au mfalme ndio hawanaga upinzani. CCM imekuwa kama ufalme uliofunikwa na kivuli cha demokrasia
 
Nasikia kuna vyama 17 vimeshiriki, na vimetoa ahadi kedekede, ahadi lukuki, ni wewe tu sasa itakua hujakutana nao huko na kusikiliza maudhui.
 
Hapo anashindana na kivuli chake tu. Hakuna kingine.
Angekuwa na uwezo wa kupambana na pia kujiamini, asingemfunga Lissu kwa hila!
 
Sa100 anashindana na wagombea ambao ni size yake, waliomzidi uwezo wote wamewekewa zengwe wasishiriki hasa Lissu ndio hatakiwi kabisaaa!.
 
Eti wadao mimi sijaona mgombea mwingine wa Urais akifanya Kampeni, Je nauliza Samia anashindana na nani?

Au watu Millioni 60 nchi nzima hakuna mtu anayeweza kuchuana na Samia. Maana kuanzia kwenye vikao vya CCM Samia hakupata mshindani, tumekuja kwenye Kampeni bado hatuoni mshindani wake.

Sasa maana ya demokrasia ni nini, mfumo wa vyama vingi una kazi gani, kama mtu anagombea peke yake... si bora turudi kwenye utawala wa kifalme tu, tumchague Samia kuwa Malkia wa Tanzania tujue moja. Maana malkia au mfalme ndio hawanaga upinzani. CCM imekuwa kama ufalme uliofunikwa na kivuli cha demokrasia
Umejaribu kupata majibu kwa Ritz na Lucas Mushambwa
 
IMG-20251018-WA0015.jpg
 
Mbona wapo wengi tu,mmoja juzi akasema eti atakuwa anawawekea vocha raia wote wa tz,pia atawalipa mshahara

Na akaongeza kwa kusema kazi ya raia ni kuzaa tu serikali itatulea
 
Back
Top Bottom