GE2025 Samia aahidi ujenzi wa mabweni shule za sekondari Bahi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,039
Akiwa wilayani Bahi mkoani Dodoma leo Jumanne Septemba 09, 2025 kwenye muendelezo wa kampeni zake kuelekea uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa wanafikiria kujenga mabweni kwa shule za Sekondari Wilayani Bahi, kama sehemu ya kuendeleza elimu bora kwa wanafunzi wa kike na kuwaepusha na changamoto mbalimbali za kijamii.

Soma pia: CCM itatoa elimu bure kutoka shule ya awali hadi chuo kikuu ifikapo 2050, hii itawafanya watoto wengi wa masikini kusoma mpaka mwisho wa akili zao

Dkt. Samia ameyasema hayo wakati akieleza mafanikio yaliyopatikana kwenye awamu yake ya kwanza kama Rais wa Tanzania akisema serikali ya awamu ya sita ilijenga shule 14 za msingi wilayani Bahi na hivyo kufanya jumla ya shule za msingi kuwa 86 pamoja na ujenzi wa shule 3 za sekondari, huku pia serikali ikikamilisha ujenzi wa chuo cha VETA ambacho kwasasa kina wanafunzi zaidi ya 156 wakijifunza fani mbalimbali ikiwemo ufundi umeme, kompyuta, ufundi umeme pamoja na ufundi wa magari.

Dkt. Samia amesisitiza kuwa katika chuo hicho wamedhamiria pia kuwa na mafunzo ya kilimo kwa vijana, kama sehemu ya kukabiliana na fursa za kilimo zilipo nchini na kwenye masoko ya kitaifa na kimataifa.
 
Back
Top Bottom