~!~Sambusa ni tamu bwana~!~

Salamu na watolea,malenga mlio tukuka.
Javini nimekaribia,pumzi nimeshashusha.
Mwito kuuitikia,Kijijini umetoka.
Sambusa yaleta jaa,mengine nayo kadhalika.

Mbona mna kondeana,wakati vyote chakula?
Bado mna kasumba,vyakula kunyanyapaa?
Mdomoni vyaingia,tumbo kwenda vimbisha.
Chooni enda vitupa,muda ukishafika.

Kula tena tatamani,hamu wala haitoisha.
Sambusa zilizo nona,kwa mafundi wakupika.
Kumi kumi wakikupa,kuvimbilwa si ugonjwa.
Takula tena na tena,hamu haitoisha.

Mihogo nenda chimbua,na jikono kuiweka.
Tia nazi na mafuta,katu shibe haitaleta.
Jaribu ya kuchemsha,au mdomoni kutafuna.
Bara hata Jang’ombe,kote nenda tafuta.

Matunda yana hadaa,machoni yana pendeza.
Mtini utapopoa,nyumbani nenda vundika.
Utakula kwa madaha,mchanyato ulopendeza.
Tumbo kwenda vuruga,chooni taenda harisha.

Mtabadilisha majina,vyakula mnavikweza.
Shibe ita walevya,njaa itawalegeza.
Vitumbua utatamani,upate japo na togwa.
Sambusa na vinevyo,majina hayo manjonjo.
 
Sandaaaaa!!! nimekupata mkuu!

Kama vyote ni vyakula, cha kwangu miye sambusa,
Napecha hicho kukila, na macho nikipepesa,
Usilete masihala, nakula nanesa nesa,
Kuleni mvipendavyo, cha kwangu miye sambusa!

Mfanowe sijaona, sambusa sitoziasi,
Tangu siku za ujana, nafyonza kama nanasi,
Vingine sitaki tena, hata muite polisi,
Kuleni mvipendavyo, cha kwangu miye sambusa!

Mguu chini naweka, kwa Rehema nitakwenda,
Nenda nkichekacheka, nikiruka kama konda,
Kama mwehu napayuka, likinidondoka denda,
Kuleni mvipendavyo, cha kwangu miye sambusa!
 
Mnajifanya wajanza, mnoghani tungo hizi
mwanakijiji wa kwanza, kwa tambo amebarizi
ajidahi atufunza, anatupa simulizi
Hivi kweli ni sambusa, ile ya nyama na ngozi?

Amsifia mpishi, yule wake la azizi
Utamue hauishi, akilapo hamalizi
Tena aleta uzushi, kutafuna sio kazi
Mundu sio bwege miye, joto jiwe kwisa jua

Akaja na mama yetu, Bi mkubwa wa Mbalizi
Muhogo chakula chetu, asijifu pandikizi
kavuna shambani kwetu, kapora yeye ni mwizi
E mama kula muhogo, utaona utamue

Kwatungo nilikataa, sitengee chipukizi
Muhogo hautafaa, kwanini ale mzizi?
Mwenzangu anashangaa, aniona mie chizi
Hivi kweli ni muhogo, ule wa chipsi dume?

Na huyu ndungu amani, manju wa kizi mkazi
Katujia akighani, kitumbua kala juzi
Na wala haoni soni, amelamba waziwazi
Si mkweli mlaghai, hana bao hana jipya

Nimeyanena maneno, bila nguvu ya hirizi
Kama kweli mna meno, kuleni bila ajizi
Matunda ni safi mno, mdomoni utelezi
Tunda langu bustani, sio fumbo ni chakula
 
Maharage

Sambusa na vitumbua, ni kwa ajili ya chai,
Onja na utatambua, vyote havina uhai,
Muhogo nao hauna, zile ladha anuai,
Maharage ya chumvi, kwa utamu tajilamba!

Maharage mengi, harage moja na likiwa dogo linaitajwe? kaharage au kiharage!

PM
 
hahaha haya yalikuwa masiku mazuri sana ktk jukwaa la lugha. Mzee Mwanakajiji njoo utupe raha huku
 
Dah aiseeh uzi wa sikunyingi lakini nimeenjoy sana. Kweli hii ndo ilikuwa jamii forum.

Hawa watu wamepotelea wapi?
 
Aisee, watu mpo nondo kwa mashairi! Yaan mnatiririka hadi raha!
 
Dah aiseeh uzi wa sikunyingi lakini nimeenjoy sana. Kweli hii ndo ilikuwa jamii forum.

Hawa watu wamepotelea wapi?
Acha tu mkuu Jf ilikuwa na watu enzi zile....hata kukomenti ulikuwa unajishauri, Kama huku jukwaa la lugha hakuna jambo lingeulizwa lilakosa majibu..wengi siwaoni kabisa siku hizi
 
Aisee, watu mpo nondo kwa mashairi! Yaan mnatiririka hadi raha!
hahaha sanaa ya ushairi ina raha yake kwa kweli,Yaani unasoma majibizano mpaka nawewe watamani uwe sehemu ya uandishi, jukwaa la lugha limefifia sana natamani haya masiku yarejee
 
hahaha sanaa ya ushairi ina raha yake kwa kweli,Yaani unasoma majibizano mpaka nawewe watamani uwe sehemu ya uandishi, jukwaa la lugha limefifia sana natamani haya masiku yarejee

Ilikuwa burudani kwa kweli. Yaani najaribu kuvuta picha ndio nimekaa ukumbini, wanapanda stejini kila mtu kumjibu mwenzake, yaani ni burudani sana.
 
We acha tuu mkuu,mi hakuna kitu napenda kama mashairi na kwa kasi ya ajabu hata diwani zimepungua, kukuta waandishi wapya wa diwani zenye kueleweka si jambo jepesi
 
Mkuu ktk kiwango cha hali ya juu kabisa. Lete vitumbua hivyo kesho tunywee chai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…