~^^~ Sambusa ni tamu bwana! ~^^~ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

~^^~ Sambusa ni tamu bwana! ~^^~

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mzee Mwanakijiji, May 3, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 3, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  sambus.jpg


  Sambusa ni tamu bwana,
  Nyingine hakuna tena,
  Wa kijiji ninanena,
  Vingine sijaviona! - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

  Ukishaonja sambusa,
  Vitumbua utasusa
  Na utatumia mapesa,
  Uje upate sambusa! - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

  Na zile zenye mafuta
  Ulimini zinanata,
  Na ladha ukishapata
  Waweza tangaza vita - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

  Zipo zenye nyamanyama
  Zaliwa Kijitonyama
  Hata ukenda Dodoma
  Sambusa hutojinyima - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

  Zipo zile zenye mboga
  Zilochumwa kama boga
  Wale wasio waoga
  Wazila hata Msoga! - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

  Zipo zenye vitunguu
  Zilotiwa karafuu
  Ukila mluzi huu
  Waimba "mikono juu" - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

  Na sambusa za Kihindi,
  Utazikuta Malindi
  Hata Mtwara na Lindi
  Zinapikwa na mafundi! - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

  Uonje 'zopikwa Tanga
  Ngonjera utazitunga
  Ukipata za Iringa
  Na baridi la Mafinga - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

  Beti zangu nazifunga
  Tungo nimeshazipanga,
  Sambusa sitojivunga
  Nayeya ninapuyanga
  SAMBUSA NI TAMU BWANA, HASA ZISIZOFANANA!

  Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
   
 2. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2010
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Mkuu kwa mafumbo! Imetulia.
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Zisizofanana wapi zipo
  Ewe malenga lojaa fumbo,
  Kila nfumbapo jicho,zanijia kufanana

  Hadi iitwe sambusa
  Si mradi iwe hasusa
  Ingekuwa vile rukhsa,basi mbona wangejirusha?

  Labda ninyambulie
  Ni kipi kitangulie
  je ni lile umbile, au ni kilichomo mle?
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,152
  Trophy Points: 280
  Ni sambusa hizi hizi zinazopatikana kwa mama lishe?
  Au sambusa zinazopatikana kwenye mti ulioota kwenye bustani ya eden?
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  May 3, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  hahahaha angalia picha BujiBuji...
   
 6. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #6
  May 3, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Ni ipi hiyo sambusa ,malenga wetu nijuze
  Ile ya kwa mama lishe au ya mama nyumbani
  Ile ya five star utamu ulokithiri kuing'ata kwa zako mbwembe au ya bibi kijijini ilopikwa asilia
  Malenga hebu nijuze ni ipi hiyo sambusa Ya kijiji au mji ipi waiongelea ?
   
 7. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #7
  May 3, 2010
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Babu sikuwezi! Mpaka SAMBUSA za kihindi? Hizo nahisi zina pilipili sana!
   
 8. Zemu

  Zemu JF-Expert Member

  #8
  May 3, 2010
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mwana unatisha kwa mashairi yako, unaonaje ukatengeneza kasingle? Ila nakuuliza kwa nini waisifia sambusa namna hii? Mbona hujasifia kitumbua? Hebu nipe mshairi ya kukisifu kitumbua kidogo Mwana.
   
 9. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #9
  May 3, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Teh teh teh
   
 10. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #10
  May 3, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mwanakijiji!!

  Sambusa ushasifia
  kidondani sijefia
  Zenye mboga na nyama
  Tanga na kijitonyama- Hala hala kaka yangu, sijezila zilooza

  Sambusa zile za nyama
  Kula hovyo ni kiyama
  Si zote zenye ubora
  zipo zenye matambara- Hala hala kaka yangu, sijezila zilooza

  Za mboga nazo si salama
  Wengi wameshalalama
  Mboga nyingi zimeoza
  Ndani wakasokomeza- Hala hala kaka yangu, sijezila zilooza

  Mwisho ninamalizia
  wasijekukuuzia
  Sidanganyike na ganda
  makini hata uganda- hala hala kaka yangu, sijezila zilooza.
   
 11. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #11
  May 3, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Haya malenga wa mtang'ata,
  Kama siyo kule Tanga,
  Mbona watupa kutanga?

  Sambusa ulotuwekea
  Kumbe zile tuzozoelea
  Ila kweli hukupotea, kutaka zisizofanana

  Kila nikicheki picha
  macho ninayafikicha
  Hizo ni sambusa au picha,

  Nijuavyo sambusa mie
  Shurti vyote vitimie
  Mtu asikupimie
   
 12. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #12
  May 3, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji weeeeee unamambo!!!!!!
   
 13. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #13
  May 3, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Alafu hizi sambusa zaliwa kwa kijiko au? maana kwenye picha naona kuna kijiko ati au ni kwa ajili ya kusevia tu alafu baada ya hapo hakina kazi?
  Mwana kijiji bana!!
   
 14. JM Aristotle

  JM Aristotle Senior Member

  #14
  May 3, 2010
  Joined: Mar 9, 2010
  Messages: 164
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmh! mimi chichemi...
   
 15. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #15
  May 3, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  kumbe JF ina malenga wengi... andikeni kitabu cha mashairi
   
 16. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #16
  May 3, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  i am very sure kwamba watu hawajamsoma huyu babu anachokihubiri na utamu wake kwa kupitia taswira ya SAMBUSA!
  lakini twende tu hivo hivo
   
 17. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #17
  May 3, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Ni nini kimekufanya, kuzipenda sambusa
  Mawazo nimetawanya, jibule nimelikosa
  Ni nyama imekufanya, kuisifia sambusa
  Tuambie ni kitu gani, kwenye utamu wa sambusa.

  Kama nyama upendayo, hata kababu wanaweka
  Au mboga waiwekayo, mpaka waweweseka,
  Ni sahani wawekeyayo, inayokupa mzuka
  Siioni tofauti, ya sambusa boflo bagia


  Labda ni umbo lake, hasa ukiliangalia
  Ndo chakula pekee, pembe tatu kuwekea
  Ncha chini uiweke, hisia zanisongea
  Hapo jibu nalipata, utamu wa hiyo sambusa
   
 18. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #18
  May 3, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Bujibuji kausoma, utenzi wako kwa dhati
  Ubongo wake ukakoma, pichayo alizatiti
  Mpangilio akasoma, akapata hatihati
  Watu hawali sambusa, na kijiko cha kizungu
   
 19. Moderator

  Moderator Content Quality Controller Staff Member

  #19
  May 3, 2010
  Joined: Nov 29, 2006
  Messages: 479
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  mnh,
  Babu hujaonjeshwa vileja, jaribu nakuambia hutoviacha.


  [​IMG]
   
 20. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #20
  May 3, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Hivi havizidi sambusa bwana ..hata sura inaonyesha vimezidishwa sukari....
   
Loading...