Sambamba na ujenzi wa bwawa la Mwalimu Nyerere, Serikali ianze kutafuta pesa za kujenga njia kuu ya umeme (Backbone)

Mikopo Chefuchefu

JF-Expert Member
May 15, 2017
3,373
6,756
Miradi hii ni ya gharama kubwa na utekelezaji wake huchukua miaka mingi.

Ni maoni yangu kuwa, sambamba na ujenzi wa bwawa la mwal Nyerere, serikali ingeanza kutafuta fedha za kujenga njia kuu ya kusafirishia umeme itakayopita magharibi mwa nchi hasa katika mikoa ya Lindi, Ruvuma, Njombe, Mbeya, Rukwa, Katavi, Kigoma, Geita na Kagera.

Hii itasaidia usambazaji wa umeme wa uhakika katika mikoa yote ya nchi yetu.
 
Miradi hii ni ya gharama kubwa na utekelezaji wake huchujua miaka mingi.
Ni maoni yangu kuwa, sambamba na ujenzi wa bwawa la mwal Nyerere, serikali ingeanza kutafuta fedha za kujenga njia kuu ya kusafirishia umeme utakayopita magharibi mwa nchi hasa katika mikoa ya Lindi, Ruvuma, Njombe, Mbeya, Rukwa, Katavi, Kigoma, Geita na Kagera.

Mkuu kwa sisi tuliokimbia umande shulen, embu tuelezee hiyo njia kuu una maanisha nini na ina faida gani kwa jamii na Taifa kwa ujumla
 
Hivi ule umeme wa gas tulioambiwa kua ukianza kutumia gharama za unit zitapungua , upo WAP?
 
Mkuu kwa sisi tuliokimbia umande shulen, embu tuelezee hiyo njia kuu una maanisha nini na ina faida gani kwa jamii na Taifa kwa ujumla
images.jpeg
images.jpeg

5R5A9183.jpg
 
Nafikiri wakati umefika kwa wizara yenye dhamana kuligawanya hili shirika hodhi la umeme ktk makampuni ambayo yatakuwa katika mafungu matatu ili yaweze kujiendesha kifaida, nashauri ifuatavyo;
1. Yawepo makampuni ambayo yatahusika na uzalishaji wa umeme tu, yaani ule utokanao na vyanzo vya maji, upepo, gesi na mafuta, mionzi ya jua, nishati za nyuklia na hata nishati nyingine mbadala
2. Yawepo makampuni ambayo yatahusika na usambazaji tu,
3. Yawepo makampuni ambayo yatahusika na uuzaji wa umeme tu tena kwa njia ya ushindani kutokana na gharama za uzalishaji na usambazaji wake.
 
Hii nadhani ifanyike wakati lile la Mwalimu nyerere likianza kazi...
Bwawa likikamilika, umeme hautakuwa na manufaa kwa kuwa hautaweza kumfikia mlaji.. Kwa capacity ya gridi ya sasa, sidhani kama ina uwezo wa kubeba kiasi kikubwa cha umeme..

So ni bora kujenga njia mpya taratibu taratibu angalau km 300 kwa mwaka.. Serikali ikipata Bilioni mia mbili 'hazina kazi' inajenga kidogo kidogo mwishowe line itakamilika.
 
Haya mambo yoote yapo chini ya wataalam na yatafanyika.kikubwa tupige kazi kwa bidii na tuzidishe maombi mungu azidi kutupa amani na utulivu ili tuzidi kupaa kimaendeleo.
 
Miradi hii ni ya gharama kubwa na utekelezaji wake huchukua miaka mingi.

Ni maoni yangu kuwa, sambamba na ujenzi wa bwawa la mwal Nyerere, serikali ingeanza kutafuta fedha za kujenga njia kuu ya kusafirishia umeme itakayopita magharibi mwa nchi hasa katika mikoa ya Lindi, Ruvuma, Njombe, Mbeya, Rukwa, Katavi, Kigoma, Geita na Kagera.

Hii itasaidia usambazaji wa umeme wa uhakika katika mikoa yote ya nchi yetu.
Hela atatoa wapi?

Ulaya?

China?

Uarabuni?

Wapi hasa?
 
Nafikiri wakati umefika kwa wizara yenye dhamana kuligawanya hili shirika hodhi la umeme ktk makampuni ambayo yatakuwa katika mafungu matatu ili yaweze kujiendesha kifaida, nashauri ifuatavyo;
1. Yawepo makampuni ambayo yatahusika na uzalishaji wa umeme tu, yaani ule utokanao na vyanzo vya maji, upepo, gesi na mafuta, mionzi ya jua, nishati za nyuklia na hata nishati nyingine mbadala
2. Yawepo makampuni ambayo yatahusika na usambazaji tu,
3. Yawepo makampuni ambayo yatahusika na uuzaji wa umeme tu tena kwa njia ya ushindani kutokana na gharama za uzalishaji na usambazaji wake.
Wazo lako ni zuri mkuu ila tu kwa sasa zipo kampuni za Privates IPPL zinazalisha umeme na kuuzia Tanesco, Ni wazi tanesco anajiendesha kwa hasara japo sijasoma recently financial report zake ila tu Bei aliyokuwa ananua tanesco ilikuwa kubwa kuliko anauzia wana nchi kutoka ktk izo private company, Hivo sio kila biashara inahitaji kuwe na Kampuni nyingi hapana ndio mana National Grid iko owned na Goverment ivo Grid ya Taifa hatuwezi kuingiza katika mikono ya watu kwa mgongo wa private investors Kwenye Swala la Generation na Transmission hapo tunahitaji Serikalo ndio imiliki hizo source na Miundombinu Sababy kubwa ni "SECURITY " Huku Distribution sasa ndio atleast unaweza tengeeneza Kampuni zaidi ya moja ili pawe na ushindani nalo litazamwe kwa umakini sana kuepuka sabotage, National Grid ni kitu sensitive na kinapaswa kumilikiwa na serikali 100% hata vita ikitokea kuna sehemu zinakuwa Guarded sana na miongoni mwa hizo sehemu ni power station Na Grid kwa ujumla leo ukilala ukaamka Nchi nzima iko kwenye blackout unafanyaje?
 
Back
Top Bottom