Samaki nilomla ni wa kichina nini??

Magulumangu

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
3,047
452
Wale waloishi au kukaa maeneo ya Dodoma mnajua samaki wa kule jinsi walivyona shombo, wale wa kanda yetu ya ziwa Victoria mnajua Sato na Chengu zinavyochengua, kwa wale wa Pwani mnajua pweza mtabiri alivyokamata, na kule kwetu kilimanjaro na kwingineko mwajua walivyo samaki wenu, swali sasa, Leo nimekula samaki asie na shombo nikajiuliza huyu samaki wa wapi jamani? Hata kidogo hana shombo, hata ingekuwa shombo ya ng,ombe ningeelewa lakini hana hata kidogo, je umeshawahi kula samaki asie na shombo hata kidogo? Nijuzeni wakulu au wangu wa kichina nini?
 
dah, hii ni PhD ya tafsida.

ni kweli mkuu, shombo la samaki lina raha yake. linaonyesha kuwa kitu ni natural, ni pure, yaani bado kuchakachuliwa. haya mapafyumu, ma udi na sijui madeodorant ndiyo yanayomaliza shombo! samaki bila shombo si samaki asilani. hata wa kichina shurti awe na shombo. kama huyo uliyemla hakuwa na shombo, basi hujala samaki mkwe wangu!
 
dah, hii ni PhD ya tafsida. <br />
<br />
ni kweli mkuu, shombo la samaki lina raha yake. linaonyesha kuwa kitu ni natural, ni pure, yaani bado kuchakachuliwa. haya mapafyumu, ma udi na sijui madeodorant ndiyo yanayomaliza shombo! samaki bila shombo si samaki asilani. hata wa kichina shurti awe na shombo. kama huyo uliyemla hakuwa na shombo, basi hujala samaki mkwe wangu!
Neno tafsda!!hadi raha kiswahili lugha ya kujivunia!!
 
mapishi gani hayo ya kumalza shomo lote? basi hayao mapishi hata mie siyataki, yamepitiliza! raha ya samaki shombo bwana.


Ni mapishi tu.
Kuna namna nyingi za kumwandaa samaki ila labda umezoe michemsho ya samaki, ha ha ha!

Kwa mfano samaki wa kuchemshwa na kutengeneza supu ana shombo zaidi, kuliko aliyechomwa kwenye mafuta bila spices kisha akaungwa na kutengeneza stew (kiingereza cha Tz wanaita Rosti).

Pia hiyo rosti inaweza kuwa na ladha tofauti kama wakati wa kumchoma kwenye mafuta, spices kama ginger (tangawizi) na cardamom (iriki) zilitumika. Huo ni mfano tu kwa kufuata mapishi ya kibongo, Sasa ukichanganya na mapishi ya kihindi, Kiitaliano, Kijapani, kichina, kiarabu, kipersia, au latin america, utashangaa unakula samaki mtamu tu lakini shombo hakuna kabisa.
 
Ni samaki huyu huyu tunaemfahamu au kuna samaki mwingine nyuma ya huyu?
 
Nanren tuko pamoja kweli?

Kelewa uzuri kabisaa.Kila kabila lina jinsi yake ya kuandaa samaki jamani! Ila bila shombo kiduchu sijui kama utajua kama ni samaki,beef au kitimoto.Manake hata shobo (aroma) ya kolekole tofauti na prawns!
 
Jamani hili ni jukwaa la mapenzi na mahusiano, kwa hakika mtoa thread hamaanishi biological fish, nadhani hapa samaki inasimama badala ya DEMU. Ni tafsida ya hali ya juu sana. Nilipokuwa mdogo nilikuwepo(bila ruhusa, kipindi nipo darsa la tano, achana na kizazi hiki enzi hizo hatukujua mambo mapema) kwenye kikao kimoja cha usuluhishi wa ndoa, "Mume akilalamika Mke hataki kutandika Kitanda, hataki nivute sigara", nilitoka nikiwa nimeelewa tofauti kumbe watu walikuwa wanashuluhisha mke kumbania mme tendo la ndoa, nilikuja jua baadaye sana.
 
raha ya samaki angalau kawepo kashombo kwa mbali wangugu.......... hata kama angekuwa wa kichina, sombo muhimu............. otherwise kwangu ni big nooo.................
 
Ni samaki huyu huyu tunaemfahamu au kuna samaki mwingine nyuma ya huyu?
na utamu wa samaki ukimla sharti umgeuze, wala upande 1 ukisha wambirua wamla na upande wapili,basi hapoo rrrraaahaaaa,hata shombo au vumba hulisikii unakula mpk miba.
 
chapa nalo jr, umeenda offtopic!
now back to topic...ukienda kutembea ufukweni mwa bahari unapata upepo mwanana wenye harufu ya bahari, na ndo raha ya kutembea ufukweni!
kama hamna harufu itakua swiming puli na sio bahari.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom